Dawa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa.

Discussion in 'JF Doctor' started by Kennedy, Oct 24, 2012.

 1. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,270
  Likes Received: 2,945
  Trophy Points: 280
  Wana JF na Ma dr nawasalimu wote. Napenda kufahamishwa kuhusu baadhi ya dawa mfano Ampiclox umeandikiwa 1x3 ikiwa na maana asubuhi kidonge kimoja,mchana kimoja,na jioni kimoja.Kuna dawa za maji kama Cophydrex nayo unaandikiwa kijiko 1x3 inakuwa kama hiyo dawa ya kwanza kuitaja. Swali langu kwa ma dr na wataalam usiku wa huwezi endelea na dozi mpaka asubuhi?Yaani jioni ukinywa saa sita usiku unakunywa tena mpaka dozi itakapokwisha.
   
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kennedy,salaam
  Unaaanisha kuwa baada ya kunywa jioni(mara ya tatu) uendelee kuitumia tena usiku?
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hii ina maana gawa siku ya masaa 24 kwa tatu na utapata masaa nane!! Kwa mantiki hii kama utaanza saa 12 asubuhi, then saa 8 mchana, then saa 4 usiku ambao ni muda mzuri kwa dawa ya TDS (Three times a Day). Kwa mantiki hiyo if yiu choose kuanza saa 2 asubuhi then 2nd dose ni saa 10, 3rd dose saa 6 usiku kama utakuwa macho. Ndo maana nyindi za TDS anza either mchana saa 8 au saa 4 usiku, etc!! Huu ndiyo utaratibu kwa antibiotics nyingi na zingatia masaa otherwise ugonjwa unakuwa unatibika nusu nusu na mwisho waweza kuwa chronic.
   
 4. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,270
  Likes Received: 2,945
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana yangu mkuu.
   
 5. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,270
  Likes Received: 2,945
  Trophy Points: 280
  Ndiyo namaanisha hivyo Mkuu,usiku unaweza endelea na dawa hata ukaweka alarm clock ikuamshe,napenda kujua utaratibu huo unakubalika kitaalam?
   
 6. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Kennedy,

  Siku ina masaa 24, na dawa(dawa nyingi) daktari anaandika kulingana na uwepo wa masaa 24 katika siku.Hii ikiwa na maana anafanya hesabu(KULINGANA NA DOZI INAYOHITAJIKA) yaani dawa mtumiaji atumie kila baada ya masaa 24, au masaa 12, au 8 au 6...Hivyo basi hufanya hivi;

  a)1x1 (Humaanisha kila baada ya masaa 24)
  b)1x2 (kila baada ya masaa 12)
  c)1x3 (kila baada ya masaa 8)
  d)1x4 (kila baada ya masaa 6)

  Sasa kwanini daktari anakuamvia kunywa mara tatu? anamaanisha alifanya hesabu katika masaa 24 ya siku, dawa aliyokupa unatakiwa kutumia kila baada ya masaa 8..yaani masaa ya siku nzima ukigawanya kwa masaa ya kutumia dawa YAANI 24/8= 3...so kwa wagonjwa wengine(NI NGUMU kuelewa au kukumbuka) so unapomueleza tumia asb, mchana na jioni ni nafuu.


  KUJIBU SWALI LAKO:
  Si vyema kutumia zaidi ya dozi(kumvuka kila dawa ina madhara)..hivyo unaweza kuathiriwa na madhara ya dawa, ongezeko la dawa mwilini, n.k

  Sijui kama umeelewa mkuu?
   
 7. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,270
  Likes Received: 2,945
  Trophy Points: 280
  Nashukuru mkuu.
   
Loading...