Dawa za mswaki sio rafiki kwako, fanya maamuzi magumu

Kuna tooth paste inayotengenezwa na forever loving company kwa kutumia mwalovera haina sumu hata kidogo,..na inatib vitu vingi mf: fiz kutoa dam au kinywa kutoa haruf mbaya kila wakat
 
njia nyingine ya kutengeneza dawa ya meno unahitaji kuwa na limao na bankingpowder chukua limao kisha kamua upate maji yake kisha changanya na vijiko 2 vya banking powder kisha changanya mpka mchanganyiko uwe kama ujiuji
done....
 
Mkuuu hata matunda ukichunguza sana yana kemikali,embe la 1800 na 2015 ni tofauti kabisa hivo hivo kwa kila kitu,kemikali ipo katika kila kitu na muungu ameumba mwili wetu katika umbile bora kabisa..kwaiyo inaweza zikawa zina madhara ila kwa kupigia mswaki hazina kabisa madhara..labda uwe unaila hyo dawa tube nzima kila siku ndo maybe itakuletea madhara
 
Daaah hujaitendea haki kabisa fani yangu ya chemia,hasa ulivyo chambua hizo compositions

nkipata mda ntarudi kuelimisha zaidi
 
Dawa ya meno ✅
Dawa ya mswaki.

Kila kitu kina madhara tu bwana, bata ukimchunguza sana huto mla
 
Sina choyo mkuu.Tengeneza dawa yako ya mswaki kwa kutumia ingridients zifuatazo:1.vijiko sita vya mafuta ya nazi mazuri 2.Vijiko sita vya baking powder nzuri 3.Matone 25 ya mafuta ya mkaratusi au grapefruit 4.Kijiko kimoja cha unga wa stevia.Stevia ni mmea ambao ukipondwa unatumika kama sugar substitute.Stevia inatumika pia kwenye vidonda vya moto,maumivu ya tumbo na wakati mwingine inatumika kama contraceptive.Changanya vitu vyote vizuri kwenye chombo mpaka upate rangi ya cream.Weka kwenye kichupa kisichoingiza hewa kwa urahisi na funga vizuri tayari kwa kutumia itakapo hitajika.

Well
Mafuta ya nazi ni triglycerides ambayo ikifunjwa vunjwa unapata glycerine hii ipo ndani ya dawa ya meno

Baking powder ni sodium bicarbonate ambayo itakuja kuleta sodium hydroxide ilioko ndani ya dawa ya meno ya kisasa

Stevia ina stevial a glycosides which is up to 150 times the sweetness of sugar.

Hiyo ni kwauchache ila hiyo eucalyptus na grapefruit zote zina chemical

Tofauti ni kwamba hiz umezichukua zikiwa fresh na dawa ya meno teyar ishatengezwa na ina viwango stahik, unaeza sema chemical zimebalance vizur

Yote kwa yote mwanadamu huwez kuepuka kemikali. Kemikal ndo hutuacha tuichi
Chakula tunachokula ni kemikali na mwili hufanya kazi kwa mipambano ya kikemikal (chemical reaction) .

Tuzingatie matumiz ya chemical wala tusiogopeshane
 
Hivo vitu vikichanganywa kwa pamoja haviendelei kuexit kwenye mchanganyiko kama vilivo... Kuna reaction inatokea end product ndio hio dawa.. Sasa ijadili end product kimadhara na sio vitu vilivotengeneza kwani havipo tena ndani yake
 
Ndo mana wanasemaga tusimeze,unasafishia meno kisha unaitema

Tutumie nini sasa mbadala wa hizi dawa za meno?
 
ni kweli hivyo ulivyovitaja vinaweza kuwa sumu, lakini yapasa tukumbuke itakuwa sumu iwapo utaitumia kwa kiasi gani. na karibu kila kitu kikitumika katika viwango vya kupindukia ni sumu, ndio maana hata katika maandiko matakatifu kula kupita kiwango chako ni dhambi pia, hata huo mkaritusi ni sumu pia iwapo utapitiliza viwango. ndio hivyohivyo hata majani ya chai mnayachambua hivyo. YEEEEE WAJAMENI tutaacha kula kabisa!!!!!!!!
 
Daaah tunauawa ukute hii ni brand special for third world country (product adaptation )
 
Back
Top Bottom