Dawa za mapenzi ni kweli?

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642
Habari?,rejea thread yangu yenye kichwa: JAMANI MAPENZI YATANIMALIZA NISAIDIENI PLS (nimeshndwa kuicopy hapa kwa kuwa natumia simu hvyo yeyote anaweza kunisaidia). Jaman nimembembeleza,nimeomba na kujishusha sana asiniache kwa kuwa nampenda sana lakini imeshindikana na jana kanitumia msg NISAMEHE KWA YOTE WANGU ILA BORA KILA MMOJA AWE UPANDE WAKE nilipomuuliza kwanin?,akajibu,SINA FURAHA KTK RELATION YETU NA NINAOGOPA FURAHA ISIPORUDI NTAKUWA NIMEPOTEZA MUDA WAKO. Kiukweli nimeumia sana,nmeshndwa kula toka jana asbh na sijalala usiku kucha,kiufupi nateseka sana mpaka nimefikiria kujidhuru..nikaona hapana bora nijaribu kwa hawa WAGANGA wa kienyeji pengine watanisaidia kurudisha penzi langu. Jamani hivi kweli dawa hizi zinafaa?,nisaidieni nifanye nini nateketea mwenzenu.
 
Kuachwa si ajabu wala wewe si wa kwanza wala wa mwisho.

Puuza tu, mwisho hisia zako zitapungua kwake na utapata mwengine.

Dawa ya mapenzi ndio naisikia kwako
 
Acha kujisumbua kwa waganda ndugu yangu, hawana lolote, tena usipoangalia watakutaka hata wewe ili wafanye mambo yao!!!! Mapenzi yanategemea pande mbili, moja ikishaanza kudhoofu ya pili nayo itachoka with time. Nakushauri upuuze jambo hilo alafu jiweke buzy na mambo mengine ya muhimu huku ukifutilia mbali kumbukumbu za zamani. Usikurupuke kutafuta replacement/mbadala.....Omba kwa Mungu utapata kitu bora zaidi ya huyo. Usijilaumu na wala usimlaumu sana kwani hoja yake pia in msingi. Si vyema kulazimisha mapenzi!!! Relax
 
Pole sana kakangu, huyo dada atakuwa amekuchoka na tayari keshapata mwingine. Hivyo vuta moyo konde, jaribu kuwa busy na shughuli zako fanya mazoezi kuuchosha mwili wako. Baada ya muda Mungu atakusaidia na utamsahau kabisa.

Usiende kwa mganga wa kienyeji kwani mapenzi hayalazimishwi utapoteza hela na muda wako bureeee
 
Naomba mwenye experience ya waganga wa mapenzi ampe maneno machache tu kilimtokea nini. Kuna mmoja nimesikia kama kasema aliliwa na mganga japo hakuwa wazi.
 
wakuu nashukuru sana kwa mawazo yenu nimepata kitu cha kuanzia mpaka sasa,natakiwa kuukubali ukweli japokuwa ni mchungu na unaumiza sana tena sana.
 
Hebu amini kuwa maisha yataendelea tu hata bila ya yeye, kwani kabla hujamfahamu uliishije?
 
Kwanza nakupa pole sana ila tambua huwezi kulazimisha penzi,najua kuachwa kunauma sn ila cha kufanya ikubali hiyo situation yani nataka nikwambie amekufanyia feva kubwa sana kukuacha siku moja utakuja gundua na utatamani umtafute na kumshukuru kwa alichokufanyia!

Kubali huyo hakuumbwa kwa ajili yako na ilikuwa lazima atoke maishan mwako na mwenye nafasi yake apate kuingia,jikeep busy,fanya mambo yako ukiamin yeye alikuwa ni sehemu ya mapito yako tu kuelekea kwenye mafanikio,mwombe mungu akukutanishe na aliyemuumba kwa ajili yako.

Achana na na habari ya waganga hakuna dawa ya mapnz dunian ingekuwepo hata MMU isingekuwepo coz na matatizo ya mapnz na mahusiano yasingekuwepo,tambua kwenye mapnz hata tajiri analia japo ana pesa,dawa zingekuwepo angetumia pesa zake kuweka mambo sawa na asingelizwa na mapnz hata siku moja..
 
so sory jamani,kuachwa naskiaga kunauma! pole jipe moyo mungu ni mwema,yupo aliekuandikia akue wa maisha yako vumilia!
 
mkuu hamna haja ya dawa ya mapenzi.achana na mawazo hayo.tafuta mwingine.huyo kashaota mabawa.but pole sana mkuu.
 
nawashukuru wote kwa mawazo na encouragement yenu..nafarijika sana ila ukweli roho inauma na amani haipo kbs
 
Kajoleee! Kwanza kabisa mshukuru huyo mpenzi wako kwa kukuambia ukweli na kuijali furaha yako ambayo ingepotea milele kwa kung'angania kuwa naye.

Piga hatua mbele, kaza macho, angalia kulia na kushoto utamuona wa kukufurahisha milele. Hakuna dawa ya mapenzi.
 
mkuu nakushauri
1)jiweke busy sana na kila ikitokea ukamkumbuka jaribu kutafuta kitu cha kufanya
2) hiyo ni bora kutokea mapema kumbuka mungu sometimes huwa anawahepusha viumbe vyake na matatizo ambayo ungeweza kuja kuyapata in future.
3)chukulia kuachwa ni jambo la kawaida tu na wala hautokufa kwa kuachwa kwani hukuzaliwa nae na ukifa pia utazikwa peke yako
4)kama wewe mfanyakazi hii ndio fursa ya kuongeza juhudi katika kazi na kama mwanafunzi ndio muda sahihi wa kukomaa na kitabu
5)ukifanya hivyo vitu hapo juu itachukua muda mfupi sana utamsahau usiwe idol fanya kitu all the time
6)ungefukuzwa kazi hapo ingekuwa inshu maana inaendana na maisha ya kila siku ila kama mwanamke au mwanaume kukuacha hiyo siyo inshu inahitaji muda tu.
7)kula bata zako wala usijute kuna watu bilioni 7 wote hao wameisha mpaka ulie sana.enjoy mtu wangu utapata mwingine.
 
Back
Top Bottom