Dawa za kupunguza mwili

Manchid

JF-Expert Member
May 29, 2016
218
469
Naomba kufahamishwa kama madawa nazani yatakua ya kichina ambayo watu wanatumia kupunguza mwili je yana madhara yoyote kwa mwili? Na kipi bora kati ya kufanya mazoezi ili upunguze mwili na kutumia hayo madawa?
 
Mkuu Fanya mazoezi na punguza kumeza sana chakula hasa vyakula vyenye calories nyingi

There is no way around, sadly

Hao wazungu na wachina wanaowatengenezea hizo dawa ndo wanaongoza kwa kufanya mazoezi
 
Piga tizi/zoezi sana ..tembea ..kimbia na ule milo mitatu kwa siku ...mlo mkubwa asabuhi ..jioni mlo mdogo na hakikisha hulali tu baada ya kula dina ...jipe masaa machache kabla ujalala
 
Ukiamka asubuh kitu cha kwanza kabisa kunywa maji ya uvuguvugu glass mbili,alaf uwe unafanya mazoez.punguza vyakula vya sukari,punguza vyakula vyenye mafuta,pia penda kunywa maji kwa sana ,kwasababu unapokunywa maji sana hamu ya kula inapungua na hapo unaweza kukonda,jaribu ivo ndani ya mwez tu na utaona mabadiliko
 
dawa ya kupunguza mwili ni kuacha kula na hakuna dawa nyingine yeyote

kwanini utumie madawa ya kichina wakati unaweza kujizuia kula kwa wiki 1 tu na utapunguza pounds za mafuta na kilo,

mazoezi yanajenga mwili na siyo kupunguza mwili,njia pekee ni kufanya diet na kutokula vyakula vyenye mafuta.

nikimuona mtu anatafuta dawa ya kupunguza mwili huwa namshangaa sana
 
Back
Top Bottom