EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,320
Ally Issa Masoud (46) mwenye nasaba ya Tanzania na raia wa Canada kwa miaka nane amehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela huko Canada kwa kosa la kusafirisha kilo 4.7 za heroin zilizokuwa kwenye begi lake. Bw. Msoud alikubali kosa lake Julai mwaka jana na kuhukumiwa Jumanne, March 7, 2017. Alisema alisafirisha dawa hizo baada ya kuhaidiwa Dola 5,000 za Canada.
Hata hivyo, Jaji Alanna Murphy amempunguzia miezi 19.5 kwenye adhabu yake kutokana na muda aliokaa rumande. Hivyo atakaa jela miaka tisa na miezi kadhaa. Pia Jaji ameamuru Bw. Masoud atoe sample ya DNA kwa ajili ya databank ya Canada. Jaji ametoa amri kwa Bw. Masoud kutomiliki silaha kwa muda wa miaka kumi baada ya kumaliza kifungo chake.
Mahakama iliambiwa kuwa Bw. Masoud aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Halifax, Canada, Februari 14, 2016 na ndege ya Shirika la Ndege la Kimataifa la Canada akitokea London. Alikamatwa baada ya scan ya passport yake ya Canada kuonyesha kuwa alikuwa anatafutwa kwa kutolipa pesa za matunzo ya watoto wake.
Bw. Masoud aliwaambia maafisa wa uhamiaji uwanjani hapo kuwa safari yake ilianzia Tanzania. Hata Hivyo, baada ya mahojiano zaidi iligundulika kuwa safari yake ilianzia Rwanda. Maafisa hao walikuwa na taarifa za heroin kuingizwa Canada kutokea Rwanda; hivyo waliamua kulichunguza zaidi begi la Mosoud na kukuta dawa hizo za kulevya.
Katika ushahidi wake, Bw. Masoud aliiambia mahakama kuwa alirudi Tanzania mwaka 2013 baada ya kuachana na mke wake huko Canada. Alisema akiwa Tanzania hakuwa na pesa na aliwa-miss watoto wake na hivyo kuamua kurudi Canada mwaka jana.
Alisema wakati akisafiri kupitia Rwanda alifuatwa na mwanaume mmoja kwa jina Dean and kuhaidi kumpa Dola 5,000 za Canada kuleta begi lilokuwa na heroin nchini Canada. Bw. Masoud alisema mpango ulikuwa yeye kupokea bahasha yenye fedha hizo baada ya kumkabidhi begi hilo mtu mmoja ambaye anamsubiri uwanjani hapo.
Aidha Bw. Masoud aliiambia mahakama kuwa hakujua jina la mwisho la Dean au uraia wake, lakini alihisi anatokea Afrika Mashariki. Pia alidai hakujua kama dawa hizo za kulevya zilitoka wapi na zilikuwa zinaelekea wapi.
Hata hivyo, Jaji Murphy hakukubaliana na maelezo yake kuwa alikuwa hajui mpango mzima. Kwa mfano, Jaji alisema hakuchukua hatua stahiki kujua alichokuwa anasafirisha. Jaji alisema kuwa Masoud alikuwa anajua anapeleka dawa za kulevya Canada na hivyo kumtia hatiani kwa kosa la kujaribu kuingiza dawa za kulevya Canada kinyume na sheria.
Chanzo: Heroin courier caught at Halifax airport handed 11-year prison sentence - Local Xpress