Dawa za Kulevya: Nape aasa "Tusiwahukumu watu kwa Tuhuma, kubomoa brand ya mtu/taasisi ni sekunde"

Aache taratibu zifuate mkondo wake. Angekuwa anathamini brands and names, angesha hakikisha Ray C na Chid Benz (walioharibu brands and names zao kupitia madawa) wanasaidiwa kwa kuwakamata wale wanaowauzia.
Hakika umenena
 
Baba Rizi aliwahi kukiri mara kadhaa kukabidhiwa orodha ya majina ya hawa watu lakini ndio kama hivyo akapotezea hadi leo.

Moja kati ya wapambanaji ambao nyota yao ilizimwa ghafla baada ya kuingia kwenye hii vita ni Amina Chifupa (Rest In Eternal Peace) na hadi leo yale majina yaliyo kabidhiwa pale magogoni hatusikii chochote.
 
Hakuna aliye mzuia kuendelea lakin ni kwa wenye akili pekee ndio wanaweza kuona dosari ilipo lakin kwa watu wa jamii yako ni ngumu sana kuliona tatizo.
 
Nape anaogopa round itafika kwa wale vijana wake wa WASAFI anaanza kuweka defensive mapema kuwa mpole mh. waziri.


RAY C , NANDO , CHID BENZ n.k walikuwa na majina makubwa sanaa, sasa hv wako wapi?? Zilianza tetesi km hv hv km akina wema wanavyotuhumiwa, unataka wawe mpk addicted???

Waziri acha woga WASAFI nao itafika tu arobaini yao hata km sio kipindi hiki cha makonda.
 
Juhudi yoyote ya kuzuia utumiaji na usambazaji hata iwe ndogo vipi, ni juhudi sahihi!

Hata akikamatwa msambazaji mmoja hiyo ni achievement!

Makonda kaonyesha uthubutu wa hali ya juu, leo IGP katoka kwenye lindi la ukimya na kuact, hii ni juhudi ya makonda!

Tumuunge mkono makonda, vita havina falsafa, wala kulemba lemba, vita ni vita mura!
 
Well said Bw Waziri, Busara ni muhimu kuliko kujitafutia umaarufu binafsi.

Busara ipi imekiukwa! Tuwaache kisa wametupigia kampeni? Nani asiyejua nn wasanii (baadhi yao) wanavyohusika kuhusu tuhuma hizo? Busara itumike jamii iangamie kwa kuendekeza kupigiwa kampeni na wasanii? Upuuzi mtupu!! Nyerere, Mwinyi, sia hakika kuhusu Mkapa, kama walipigiwa kampeni na wasanii!! Huko ni kufilisika kisiasa kutegemea kushinda kwa kutumia wasanii!! Wema kaguswa, naam kaguswa! Msumari umeingia, kama hana hatia atatoka Mr. Waziri.
 
Kwa mtazamo wangu namuomba MH. Nape amuache kijana Mh. Makonda aendelee kuchapa kazi. Kama angekuwa analinda hiyo brand au brands angechukua hatua za dhati kabisa kuhakikisha wasanii hawajiingizi kwenye madawa ya kulevya.
Kuwapeleka watu rehab sio suluhisho. Ni sawa na kuokota maiti mtoni na kwenda kuwazika bila kujiuliza nini kinawaua hao watu??
My take: kama waziri mwenye dhamana angekuja na suluhisho la kuwataja mapapa ambao anafikiri ndio wanao wabebesha ngada wasanii. Sina hakika ninawasi wa kwamba katika utajaji huu pengine tutasikia mengi ambayo yanawahusu wakuu. Na ninashauri tuendelee kumwombea MH.RAISI ili wiki inayoanza apate ujasiri wa kuwataja Manyangumi na Mapapa wa Unga kwani amepata sehemu ya kuanzia.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Paulo Makonda endelea kaka usirudi nyuma. Wanyonge wengi na ndugu zetu wengi wameteketea kwa sababu ya ngada. Twende mdogo mdogo tutafika. Lakizima kiazi kizikwe ndo kiote.
 
Aseme kama ni miongoni mwao,Maana anataka iwe siri kuwajibisha wakati kila mtu anajua fulan anatumia na fulan hatumii

Suala hapa sio watumiaji

Hapa ufanisi nikunasa suppliers, Transpoters na mabosi.

swali unawezaje kuwapata wahusika na ushahidi ukiwa umesha-wa-alert kwamba utawa-search siku yoyote?

kuwa-alert sio kuwapa upenyo wakujiaandaa kuficha ushahidi?
 
So kwa hoja yako hawa wasambazaji wadogo wasibugudhiwe tudeal na wasambazaji wakubwa tu?
 
Ukiwa huna ndugu yako úwa ambaye anateseka na haya madawa ya kulevya lazima uone kuna uonevu kwa wanaotajwa kuhusika,ila cku yakimpata mwanao au mtu wako wa karibu ndio utaona umhim wa kuanzishwa kwa vita hii....
 
Hebu hili swala aachiwe makonda mwenyewe.
Haswaaaa. Hawa wengine ni wale wale. Brand ooo hakuna Makonda piga mzigo tunakuombea lala usingizi mungu akutie nguvu mpaka kieleweke Dkt.JPM wasikilize wanaoweweseka ndg ndio kwanza first episode
 
Hakuna aliye mzuia kuendelea lakin ni kwa wenye akili pekee ndio wanaweza kuona dosari ilipo lakin kwa watu wa jamii yako ni ngumu sana kuliona tatizo.
Hakuna vita isiyo na dosari ndugu wacha vita iendelee kushindwa na kushinda hayo ni matokeo tu lakini uthubutu kwenye hili ni jambo la msingi mno mno mno
 

Hii ni mifano hai kwamba mtu maarufu ukimdhalilisha bila ushahidi sio sawa.Huyu alishawahi kuwa Miss Tanzania.Baba yake ni mtu maarufu sana nchini.Lazima ujiridhishe kabla ya kumdhalilisha.
Watu kama hawa ilitakiwa wakamatwe wakati ushahidi usio na shaka umeshapatikana na moja kwa moja anafikishwa mahakamani.
Hii ya kusema upelelezi unaendelea ina maana ushahidi bado haujakamilika na huenda akawa hana hatia.

Naunga Mkono sana Kauli ya nape kwamba Watu waliojijengea umaarufu kwa gharama kubwa wafanjiwe utafiti wa kina kabla ya kutangazwa hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…