Dawa za asili zasababisha mtindio wa ubongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za asili zasababisha mtindio wa ubongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Aug 24, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Ijumaa, Agosti 24, 2012 05:39 Na Pendo Fundisha, Mbeya

  UTUMIAJI wa dawa za asili kwa wajawazito ni moja ya changamoto inayosababisha watoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo na kupasuka kwa kizazi wakati wa kujifungua.

  Akizungumzia tatizo hilo mjini hapa juzi, Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoani Mbeya, Prisca Butuyuyu, alisema wajawazito wamekuwa wakitumia dawa za asili kutoka kwa waganga wa tiba za asili zinazodaiwa kuwawezesha kujifungua salama.

  Alisema tatizo hilo limekuwa kubwa na hali hiyo inatokana na jamii kukosa elimu ya afya ya uzazi, kwa kuwa ukweli uko bayana kuwa wajawazito wengi wanaotumia tiba hiyo hawaponi.

  Akitaja baadhi ya vifo vya wanawake hao waliobainika kutumia dawa hizo, alisema mwaka 2010 kulikuwa na vifo sita vya wajawazito vilivyotokana na akina mama kuzitumia.

  Alisema mbali na vifo hivyo, pia utafiti umebaini kuwa asilimia kubwa ya watoto waliozaliwa na wanawake waliotumia dawa hizo hugundulika kuwa na matatizo ya akili.

  “Unaweza tatizo hilo usilione kwa wakati huo, lakini jinsi mtoto anavyokua ndio matatizo ya mtindio wa ubongo yanavyojitokeza pamoja na mtoto huyu kuonekana msumbufu,” alisema Butuyuyu.

  Aidha, alisema maandalizi mabaya ya wanandoa juu ya kupata mtoto imeelezwa kuwa ni tatizo linalosababisha jamii ya Watanzania kupata watoto wasio na akili.

  “Wazazi wanapaswa kujiandaa vema mara wanapohitaji watoto, kwa kuwa kipindi hicho ni kipindi cha kutoruhusu migogoro, ikiwa na mjamzito kuepuka hasira za mara kwa mara,” alisema Butuyuyu.

  Alisema ni vema katika kipindi hicho wanandoa hao wakatumia zaidi vyakula vyenye virutubisho na kupumzisha akili, hali itakayosaidia upendo kutawala ndani ya mioyo yao na mtoto mwenye akili kuweza kupatikana.

  Alisema bado tabia ya wanawake wajawazito kujifungulia nyumbani kwao imekuwa ikiongezeka na asilimia kubwa hufa kwa sababu hawapatiwi matunzo wanayostahili.

  “Wakunga na waganga wa tiba za asili ni kwamba hawawezi kumudu kutibu matatizo yanayojitokeza baada ya kujifungua kama vile kutokwa na damu nyingi,” alisema Butuyuyu.

  Alisema wajawazito wenye matatizo hawapelekwi haraka katika hospitali za wilaya na mikoa na hali hiyo hutokana na ukosefu wa usafiri wa kuaminika kutoka vijijini na hata wanapofika hospitalini hali huwa ni mbaya na hata kusababisha kifo.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mmmmmhhhh mbona kule traditional med muhimbili wanatushauri hii kitu vipi iwe na matatizo.. praaaaaaaaa so mixed up na mambo hizi za kibongo!
   
 3. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Labda zile dawa za asili anbazo hazijafanyiwa utafiti wa kitaalam na kuruhusiwa kutumika ndio zenye madhara hayo.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Muhimbili wana kitengo cha utafiti wa tiba za jadi. Ni lazma ku-establish dozi ambayo itatibu bila kuleta madhara makubwa ya muda mfupi na mrefu mwilini. Na dozi ni function ya kipimo na muda. Huwa najiuliza dawa unaambiwa uchemshe unywe glass moja mara mbili kwa siku 5, what about concentration? Manake unajipimia fungu la mizizi (kuna watu wana mkono kama chepeo!), unaweka kwenye sufuria size yoyote unatia maji unayojiskia, na unaamua mwenyewe kama imeiva ama la! Hii ina-affect concentration.
   
Loading...