Dawa ya wivu nini?

Dawa ya wivu nini?

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957
KWA UFUPI

Tamati hapa nafika, wahairi nijibuni,

Nipate kupumzika, ndoa yangu kuthamini,

Natamani kuachika, ila watoto jamani,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani

Mhariri langu swali, litue kwako mezani,

Inahofu yangu hali, jibu liwe makini,

Kimara wala si mbali, makazi yangu Jijini,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani.

Ndoa iso muhali, kuoana kwa hisani,

Wazazi walikubali, tufunge ndoa nyumbani,

Tukafunga Kihalali, Na wasia kutupeni,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani.

Ghafla kabadilika, mume wa ubani,

Kutwa anakarahika, si mchana si jioni,

Jambo asilo hakika, aniweka hatiani,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani.

Moyoni nasononeka, nyumba kukosa amani,

Mawazo yamenifika, raha kamwe sioni,

Jikoni ninapopika, ametulia pembeni,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani.

Kazini ninapotoka, hima nipite chumbani,

Nieleze kwa hakika, ratiba yangu njiani,

Nani alonitamani, kutaja niwe makini,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani

Hodi jirani kafika, ajighubika chumbani,

Nia yake muafaka, asikie yasemwani,

Kisha anapoonoka, maswali tele kinywani,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani.

Nisije kubabaika, bzipo mwilini,

Hapo ndipo huridhika, mume wangu wahisani,

Pumziye humshuka, kama atoka mbioi,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani,

Waungwana natabika mume, huyu mume gani?

Unyumba ulo hakika, ninampa kwa yakini,

Hila za kila dakika, atabuni kitandani,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani,

Penzi letu mashakani, wawili tulimo ndani,

Nusura yaitajika, wahisani nijibuni,

Wapi alipokwazika, kuniweka kifungoni,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani,

Tamati hapa nafika, wahairi nijibuni,

Nipate kupumzika, ndoa yangu kuthamini,

Natamani kuachika, ila watoto jamani,

Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani,

MAGDALENA MAREGESI (SIWEMA),

SIMU 0713 840996 Dar es Salaam

chanzo.DAWA YA WIVU NINI? - Swahilihub



 
That's yo best companion on earth. Shikilia huyo huyo. Wengine tukienda bar tunarudi siku ya pili yake hatunaga wivu....
 
As i am a professional docta, dawa ya wivu ni metakelfin za italy na hedex... Try it wadau mtakija kunipa feedback...
 
Back
Top Bottom