Dawa ya watu wasiojulikana

Dawa ya watu wasiojulikana

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
947
Reaction score
690
Mwaka 2012 nikiwa ninaishi eneo moja hapa Dar es salaam, nilivamiwa na watu wasiojulikana wapatao 15 nyumbani kwangu saa nane usiku. Nilipambana na watu hawa wasiojulikana kwa dk 20-30 ili kuinusuru familia yangu ambayo naipenda sana. Namshukuru Mungu aliyenisaidia nikaweza kuwasambaratisha watu hawa wakiwa na silaha nzito na mimi kuumizwa kidogo lkn familia inabaki salama.

Baada ya tukio hili majirani ambao walikuwa waoga sana kiasi kwamba walishindwa kujitokeza kunipa msaada haswa baada ya mtikisiko mkubwa wa sauti ya bunduki nzito zilizopigwa na watu Wasiojulikana, walifika na kama kawaida yetu Waafrika wakanipa pole na kunisifia jinsi nisivyoweza kujiokoa na kuiokoa familia yangu.

Haukupita muda mrefu watu wasiojulikana wakarudi tena, safari hii kwa jirani yangu ambaye siku navamiwa hakutoka wala hakufika kunipa pole, jirani huyu ana nyumba ya kupangisha ina wapangaji takribani wanne na familia zao. Miongoni mwa wapangaji wale walikuwepo wanajeshi wawili. Kisa hiki kinachekesha kidogo, wale wanajeshi pamoja na wapangaji wengine walipekuliwa na kuibiwa kila kitu na walirushwa kichura na wamama kutembea kwa magoti huku wakiwa uchi kabisa. Nakumbuka mmoja wa wapangaji alikuwa ni nyumba ndogo ya OCD ya kituo cha polisi kilichopo karibu na eneo husika

Baada ya tukio hili la pili watu walianza kuhama mtaa na wakwanza walikuwa ni mwanajeshi na familia yake. Usiku ule wa tukio, walifika Polisi baada ya wasiojulikana kuondoka. Kwa macho yangu niliweza kuwaona watu hawa wasiojulikana nikiwa ndani ya nyumba yangu nikichungulia dirishani.

Baada ya mwezi mmoja tena watu wasiojulikana walivamia nyumba ya mwanajeshi mwingine na ktk kupigana nao mwanajeshi alipasuliwa jicho na wasiojulikana wakabeba kila kitu na kutokomea.

Katika matukio yote hayo na mengine yaliyofuatia hapo baadaye Polisi wetu hufika na kuanzisha upepelelezi ambao kamwe haukuwahi kutupa jibu la matukio ya aina hii.

Kama jamii sisi wenyewe tuliamua kukaa na kupanga mikakati ya jinsi ya kupambana na watu wasiojulikana.

Jamii ilinichagua mimi kuwa mwenyekiti wa kikosi kazi cha kupambana na watu hao.

Nilianza kazi mara moja na niliitisha kikao cha wakazi wote nikaomba wanipe timu ya watu nitakaoshirikiana nao. Baada ya hapo kwa pamoja tuliweza kuweka mikakati thabiti na tukaingia kazini.

Moja ya njia tuliyoitumia kupambana na watu wasiojulikana ilikuwa ni ulinzi jamii. Tulifanya doria na kumkamata yeyote aliyedhaniwa kuwa njia zake hazipo wazi kwetu. Tukikukamata ulikuwa unachezea kichapo cha jamii na hadi tunakukabidhi kwa Polisi utakuwa umetoa siri zote na kutupeleka kwa kwa wenzako wasiojulikana.

Niseme wazi kuwa dawa ya watu wasiojulikana siku zote sio Polisi bali ni jamii husika kwa ujumla wetu.

Katika utendaji kazi wetu tulifanikiwa kujua kwamba kati ya watu wasiojulikana wapo mapolisi, wanajeshi, raia wa kawaida matajiri kwa maskini.

Watu wasiojulikana wapo katika ngazi zote, wapo wanaotumwa na vyama vyao, wapo wanaotumwa na dini zao wapo wanaojituma wenyewe nk

Dawa ya watu wasiojulikana ni jamii kwa pamoja kuwasaka na kuwashughulikia, kamwe tusijidanganye kwamba wapo Polisi au jeshi litakaoweza kudhibiti watu hawaa wasiojulikana.

Tuamke kabla hawajaja kwako, leo ni Lisu kesho ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatuletea hadithi eti walikuwa na silaha nzito na wewe hujatuambia ulikuwa na silaha gani halafu ukawashinda AMAAAAAAZING
 
Mrema alisaidia kudhibiti watu wasiojulikana kwa ushirikiano kati ya Polisi na jamii husika.
 
Back
Top Bottom