Dawa ya Ubaguzi hii hapa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
DAWA YA UBAGUZI NI KUBAGUANA

Na, Robert Heriel

Kama kuna njia muhimu ya kuondoa ubaguzi basi ni kubaguana. Ubaguzi utadumu daima dawamu endapo watu hawatabaguana.

Kubaguana ndio njia sahihi kabisa ya kuondoa ubaguzi duniani. Hatuwezi kuondoa ubaguzi kwa makongamano, hatuwezi ondoa ubaguzi kwa kujipendekeza kwa wanaotubagua, hatuwezi ondoa ubaguzi kwa njia ya kuandamana. Maandamano hayajawahi kuondoa ubaguzi na hasa ubaguzi wa rangi.

Ubaguzi wa Rangi utaendelea kudumu kwa sababu watu hawabaguani, kundi fulani ndio linabagua kundi jingine. Endapo Makundi yote yangebaguana basi ubaguzi ungeisha zamani sana.

Siku zote wanaopinga ubaguzi ni kundi dhaifu, kundi duni ambalo linalazimisha usawa. Kundi linalojipendekeza kwa kundi lijionalo bora.

Kujipendekeza ni moja ya vichochezi vya ubaguzi, mtu anayejipendekeza hutengeneza mazingira ya kujidunisha, hatimaye hujikuta kwenye kundi la wanaobaguliwa.

Wazungu wataacha kuwabagua Waafrika siku Waafrika watakapoacha kujipendekeza, siku waafrika watakapoanza kuwabagua wazungu ndio siku hiyo hiyo ubaguzi utaisha.

Napenda nikiona mtu akibaguliwa, hasa muafrika akibaguliwa na mzungu. Wazungu ni watu bora kwa sababu wanatubagua Waafrika, ubaguzi ni sehemu ya akili kwa kiumbe kilichostaarabika, kiumbe chenye nafasi ya juu kwa viumbe wengine lazima kiwe kibaguzi.

Tunabaguliwa kwa sababu, tumeshindwa kuwabagua wazungu. Tumeshindwa kubagua tamaduni zao, ati Taikon dini yangu ni Mkristo, huo kama sio upungufu wa akili ni nini. Nimezibagua dini, mila, desturi, majina yetu, lugha zetu alafu nikibaguliwa ati nilalamike.

Ubaguzi utaisha siku tutakapozibagua na kuzitupilia mbali dini zao, mila na desturi zao.

Wewe unajipendekeza kwa Mzungu alafu akuchekee, wewe utakuwa mwehu kweli. Yaani mzungu ajipendekeze kwa mambo yangu aache yake alafu mimi nimuone anaakili, nitamuona mjinga wa mwisho. Na mjinga lazima abaguliwe.

Hata mimi nabagua majitu majinga, yaani jitu linamuamini mgeni zaidi ya ndugu yake hilo si jinga. Linastahili kubaguliwa.

Hapa nchini tuu, yapo makampuni ya kigeni ambayo huwalipa watu wao mishahara mikubwa zaidi ya mara nne ya mishahara wanayowalipa wazawa wa nchi hii hii kwa nafasi ile ile, elimu ile ile na ujuzi ule ule.

Lakini usishangae kampuni la kitanzania likiwalipa wageni pesa mingi zaidi ya watanzania wenyenye. Mfano
Mzungu atalipwa 4,0000,000 Level ya masters
Mswahili atalipwa 1,000,000 level ya masters
Kwa nafasi ile ile.
Ikiwa unabagua watu wa kwako mwenyewe na kumpendelea mgeni unadhani mgeni atakupenda zaidi ya kujiona bora kuliko watu wakweni, mwishowe utabaguliwa.

Usishangae hata kwenye miradi mikubwa ya serikali, wapo Watanzania wenye uwezo wa kuendesha miradi mpaka kumalizika lakini hawapewi nafasi, wanaopewa ni wageni. Kwa nini usibaguliwe na hao hao unaowapa nafasi.

Mtu anakubagua pale unapompa nafasi ya kukubagua. Ubaguzi wowote huja kwa kujipendekeza hasa kwa watu msiofanana.

Ili usibaguliwa basi unapaswa ujitambue, ujipende, upende watu wa kwenu, upende utamaduni wenu, upende dini zenu, upende michezo yenu, upende taifa lako, upende wanawake wenu, upendo kila kitu kinachokuhusu, uridhike na hali yako, uridhike na yale yaliyo yakwenu.

Kitendo cha kupenda mambo yasiyoyako tayari unajiweka kwenye hatari ya kubaguliwa. Na mimi kama Taikon nitakubagua tuu hata kama watu watasema nini.

Mimi siogopi kumbagua mtu mjinga, mpuuzi, mtu asiyejitambua, mtu anayedharau mambo yake. Mtu wa hivyo lazima abaguliwe, ni mpumbavu tuu.

Ati uandamane kupinga ubaguzi loooh! Nyie mtakaoandamana ni wapuuzi na wapumbavu.

Ubaguzi unaondolewa kwa kufanya kazi upate pesa, kujitafutia elimu isiyo na shaka, kuthamini dini na miungu yenu.

Wewe unapinga ubaguzi wa rangi, wakati hata dini uliyonayo inakubagua. Hakuna Nabii au hata kiongozi wa dini katika kitabu cha dini yako aliyeandikwa.
mungu wao alikubagua ndio maana hakuona umuhimu wa kumchagua Nabii yeyote mweusi, bado ujione unaakili. Acha ubaguliwe.

Ubaguzi unaondolewa kwa kubaguana. Kila mtu afuate yake, kila mtu aishi kwake, kila mtu atumie mali zake, kila mtu aseme lugha yake.

Kama kuna kuhitajiana, basi hiyo iitwe biashara. Na sio ati mahusiano ya msaada. Yaani mmoja anamuhitaji mwingine zaidi. Hapo ubaguzi lazima ujitokeze.

Ubaguzi unatokana na kundi au jamii moja kujiona bora kuliko jamii au kundi jingine. Kubaguana ni matokeo kila kundi linajiona bora kuliko kundi jingine. na hapo ndio mwisho wa Ubaguzi, watu watakaa meza moja na kufanya suluhu.

Huwezi fanya suluhu na mtu anayekubagua, atakuona mwendawazimu. Kwanza mpaka anakubagua tayari anakuona kama mnyama. Sasa atakusikiliza kama nani? Paka? au mbuzi? mbwa je? Mtu anayekubagua anamuona mbwa wake ni bora kuliko wewe, alafu afanye suluhu na wewe.

Dawa ya ubaguzi ni kubaguana, hilo likitokea basi ubaguzi utakuwa umekwisha.

Napenda kusikia watu wajinga wakibaguliwa, hiyo ndio njia ya wao kuwa na akili.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
umetumia hisia kali sana kuelezea kile kilichomo moyoni mwako. lakini tukumbuke kuwa mwenye njaa atazidi kujipendekeza kwa mwenye chakula. udhaifu watu ndio chanzo cha kila kitu, lakini pia tukumbuke ubaguzi wa mweusi kwa mweusi ni mkubwa hata kuliko hata wa mtu mweupe kwa mweusi.
 
Itategemea na ubaguliwa wapi ili nawewe ubague.
Niko Minnesota kwenye hiki chuo niko mtu pekee kutoka Tanzania na wawili kutoka Afrika mashariki, na watano tu kutoka Africa!
.
TUTAWEZANA kweli kuwabagua wazungu ambao ni wengi achana na other people of color kama Wahindi, na Walatin
 
umetumia hisia kali sana kuelezea kile kilichomo moyoni mwako. lakini tukumbuke kuwa mwenye njaa atazidi kujipendekeza kwa mwenye chakula. udhaifu watu ndio chanzo cha kila kitu, lakini pia tukumbuke ubaguzi wa mweusi kwa mweusi ni mkubwa hata kuliko hata wa mtu mweupe kwa mweusi.

mbinu ni zile nilizo eleza, ili uepuka ubaguzi sharti ujifunze kubagua. Ukijitambua huwezi baguliwa, ukijitambua huwezi kuwa masikini, huwezi kufa njaa, Afrika wanakufa njaa kwa sababu hawajitambui.
 
Itategemea na ubaguliwa wapi ili nawewe ubague.
Niko Minnesota kwenye hiki chuo niko mtu pekee kutoka Tanzania na wawili kutoka Afrika mashariki, na watano tu kutoka Africa!
.
TUTAWEZANA kweli kuwabagua wazungu ambao ni wengi achana na other people of color kama Wahindi, na Walatin


Waafrika wanabaguliwa kwa sababu ya kutojitambua hilo tuu
 
Nakwambia, huwezi mbagua mtu anayejitambua. Kwanza hana muda na wewe. Na ili ujitambue lazima uwe na akili.

Ukiona mtu anakubagua ujue amekudharau, ameona hujitambui. Sasa hapo ujiulize hujitambui kwenye nini?
Kumbuka kila mtu ana namna anavyomuona mwingine huwezi kuzuia asione anavyoona.Mzungu anaweza akaona sura ya nyani akimtazama mtu mweusi kutokana na picha aliyojiwekea akilini.
Ulimwengu wa kibaguzi unaanzia ndani ya mtu na siyo nje yake.
Kumbuka hatuoni kilichopo nje yetu ila kile kilichopo ndani yetu" katika ulimwengu wetu ndicho tunachokiona" kwa mfano hata simu yako unayoiangalia sasa hivi taswira yake inafanyika ndani yako kwenye sehemu ya jicho " retina" na kisha unasema nimeona.
Haya tunayoyaona kwa nje yana misingi halisi ndani " kwenye ulimwengu wa kifikra" na siyo kwenye ulimwengu wa vitu.Tukisema tubague tunavyoviona kwenye ulimwengu wa vitu sidhani kama tutakuwa tumegusa sababu chanzi.
Ubaguzi wa rangi ni matokeo ya ubaguzi uliopo kwenye fikra za watu na sidhani kama rangi nyeusi au nyeupe zina tatizo kama akili za wanadamu na picha za kiakili zinazozalishwa ndani yao.
Tukibagua vinavyoonekana "vitu" mfano rangi n.k tumeacha sababu chanzi " rootcause ambayo ndiyo inayosukuma ubaguzi sina uhakika kama tutafika popote.
Dunia leo inahitaji kurekebisha ndani kuliko nje " inner engineering" kama ni kurekebisha vitu vya nje wanadamu tumerekebisha sana lakini tatizo hatujarekebisha ndani.
Tunapaswa kurekebisha ulimwengu wetu wa ndani " wa kifikra"ili tuweze kuona vitu katika uhalisia wake lasivyo tutarekebisha sana Kaka.
 
Piga keleleeeeeee, nikanyage bahati mbaya, nikupige ngumi makusudi.
 
Back
Top Bottom