Dawa ya mwarobaini, faida na hasara zake

Dawa ya mwarobaini, faida na hasara zake

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,887
Reaction score
27,528
Wadau wa JamiiForums,

Kwa anayejua tafadhali mmea huu wa Muarobani. Nimepata taarifa kuwa unatibu magonjwa mengi sana, naomba anijuze na kinachotumiwa ni nini; Mzizi, Majani au Gamba lake?
 
Neemtree.jpg





Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India na Burma. Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame.

Jina “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mibegu ya mwarobaini imekuwa ikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu huko nchini India na hivi sasa inatumiwa katika sehemu mbalimbali duniani likiwemo bara la Afrika.

Wanasayansi wa nchi za Magharibi hutumia pia mti huu kwenye tiba na utafiti. Mwanzoni mwa mwaka 2005, serikali ya India ilipeleka kesi mahakamani kupinga hatua ya mamlaka ya leseni ya Ulaya (European Patent

Office
) kutoa leseni kwa Wizara ya Kilimo yaMarekani na kampuni ya kimataifa ya WR Grace kumiliki haki ya kutengeneza na kuuza dawa ya ukungu inayotokana na mwarobaini.

Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.

Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni. Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.

TIBA YA MUARUBAINI
1.TIBA
hii hutunza meno na kuondoa harufu mbaya mdomoni. Kwa watu wanaopenda kula vitu vyenye sukari kama maziwa na mikate ambavyo vikiganda mdomoni husababisha sukari na kuathiri. Wapenzi na wapenda soda ambazo zina kiasi kikubwa cha sukari, wanatakiwa kutumia mwarobaini.

Miswaki: Tumia tawi dogo kutoka kwenye mti huu ambalo lina kemikali ya asili na kusafisha au kutunza fizi za meno.

Magamba ya mwarobaini hutumiwa kutengeneza baadhi ya dawa za meno zinazouzwa madukani.

2. Hutunza ngozi

Mwarobaini ni mzuri katika kutibu magonjwa mengi ya ngozi yanayoambukiza na yasiyoambukiza.


Unaweza pia kuutumia katika kutibu madhara yatokanayo na chakula au dawa.
Oga: Kwa asili, Wahindi wengi huoga maji ya moto yaliyolowekwa majani ya mwarobaini ili kuweka kinga kwenye ngozi zao.


Mafuta: Chukua gramu 100 za mafuta ya ngozi ya kawaida uongeze gramu 10 za mafuta ya mwarobaini, paka utaona mafanikio.

3.Vidonda vya kuungua vilivyochunika:
Chukua majani ya mwarobaini kiganja kimoja kisha changanya na maji lita moja, chemsha kwa dakika 20. Baada ya hapo chuja yakiwa bado ya moto kisha yapooze, osha sehemu iliyoungua. Maji haya yanasaidia kuzuia maambukizi.
 
Thanks mzee kwa ufafanuzi.
 
Dose zake zikoje? pia nimeshawahi kuambiwa kuwa mafuta ya muarobaini ni dawa nzuri kwa meno yanayouma,mafuta haya yanapatikana wapi?
 
Habari wadau kwa kipindi kirefu nimekua nikisikia habari ya mwarobaini kuwa unatibu magonjwa zaidi ya 40 nilicho taka kujua magonjwa hayo ni yepi na yanatibika kwa muda gani pia madhara ya matumizi ya mwarobaini ni yepi mwenye kujua tafadhari anijuze.
 
Habari wadau kwa kipindi kirefu nimekua nikisikia habari ya mwaroini kua unatibu magonjwa zaidi ya 40 nilicho taka kujua magonjwa hayo ni yepi na yanatibika kwa muda gani pia madhara ya matumizi ya mwarobaini ni yepi mwenye kujua tafadhari anijuze
Neem_%28Azadirachta_indica%29_in_Hyderabad_W_IMG_6976.jpg

Maua na majani


Neem_%28Azadirachta_indica%29_in_Hyderabad_W_IMG_7006.jpg

Maua


800px-Azadirachta_indica%2C_leaves_%26_fruits.JPG

Matunda mabichi na majani




Neemfruit.jpg

Matunda mabivu



364px-Neem_tree_seeds.JPG

Makokwa

Mwarobaini
(Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India naBurma. Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame.


Jina "mwarobaini" linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mibegu ya mwarobaini imekuwa ikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu huko

nchini India na hivi sasa inatumiwa katika sehemu mbalimbali duniani likiwemo bara la Afrika.


Wanasayansi wa nchi za Magharibi hutumia pia mti huu kwenye tiba na utafiti. Mwanzoni mwa mwaka 2005, serikali ya India ilipeleka kesi mahakamani kupinga hatua ya mamlaka ya leseni ya

Ulaya (European Patent Office) kutoa leseni kwa Wizara ya Kilimo ya Marekani na kampuni ya kimataifa ya WR Grace kumiliki haki ya kutengeneza na kuuza dawa ya ukungu inayotokana na mwarobaini.


Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa

kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.

Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni. Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.
Ukitaka kujuwa zaidi kuhus Mwarubaini bonyeza hapa.
MWARUBAINI NI MTI WENYE KUTIBU MARADHI MBALI MBALI.
 
nashukuru mkuu ila sijaona side effect za mti huu kwani kuna mdau flani alinambia eti ukipendelea kutumia mwa40 una madhara kwa ini, kwani uwa napo utumia siyo mara kwa mara ila napo tumia tu mwili uwa nausikia mwepesi sna pia baada ya nusu saaa ivi uwa naendesha balaaa
 
Wakuu habarini za asubuhi?

Kwa muda mrefu mimi nilikua nasumbuliwa na maleria mara kwa mara. Yaani ilikuwa haiwezi kuisha mwaka bila kuugua maleria. Baadae nikaja kushauriwa nichemshe majani ya mwarobaini kisha ninywe maji yake. Baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza, nilipitisha miaka minne bila kuugua maleria! Hadi siku moja nikahamua tu kwenda hospitali kupima maleria bila hata kuumwa maana niliogopa isije ikawa inajikusanya ikaniua kwasababu mimi huwa situmii neti. Lakini kwa mshangao daktari akaniambia sina maleria kabisa. Tangu hapo nikajijengea utaratibu wa kunywa walau glasi moja ya maji ya mwarobaini kila baada ya kama miezi sita hivi na hadi leo sijawahi kuugua maleria zaidi ya flu flu hizi za kawaida.

Swali langu sasa ni kwamba kuna wakati niliwahi kusikia kwamba muarobaini una athari mwilini na kwamba madaktari hawashauri utumike kama dawa. Naomba kama kuna daktari / mtaalamu yoyote anaeweza kuainisha athari hizo anisaidie.

Asanteni.

NB: Kama swala hili limewahi kujadiliwa pia ntafurahi nikipewa link
 
mi kiukweli sijui madhara yake, ila toka niko mdogo kama form 3 hivi, baba yangu alikuwa anamake sure tunakunywa mwarobaini mara 2 kwa siku (asubuhi na usiku) na kiukweli sijawahi kuumwa malaria wala magonjwa ya ajabu ya kulazwa hadi leo, namshukuru Mungu pia cause some things just cannot be explained
 
Niulize dawa mwarobaini dozi yake inakuwaje?majani mangapi unachemsha
 
Nawa ya muarobaini inauwezo wa kutibu almost magojwa yote kuanzia kwa binadamu, mimea na wanyama.

Lakini hii ni dawa ambayo inamadhara kama utatumia over dose.

Mara nyingi muarobaini haifanyi kazi ya kuua vijidudu. Hufanya kazi ya kuua kizazi ja vijidudu. Pale inapotumika iwe kwenye binadamu, mimea au wanyama hufanya kazi za kuafect vijidudu vya magonjwa vishindwe kuzaliana baada ya kuua kizazi chake. Na vidudu vingu huwa na short life span so vinapokufa vinashindwa kuacha generation yao.

Disadivantage ni kuwa utu anayetumia sana muarobaini anaweza poteza kizazi pia.
 
muarobaini unatibu
arengi, homa, fangasi,moyo
Shinikizo la damu, sukari
Athari ya kutumia muarobaini bila ya ushauri wa daktari unaweza kuhalibu ini lako..
 
muarobaini unatibu
arengi, homa, fangasi,moyo
Shinikizo la damu, sukari
Athari ya kutumia muarobaini bila ya ushauri wa daktari unaweza kuhalibu ini lako..
Asante am addicted nakula sana vijiti vya muarobaini kiasi kwamba baadhi ya watu hufukiri nakula mrungi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom