Msaada wa dawa au namna ya kuondoa mvi

MrIsidori

Senior Member
Apr 3, 2014
191
83
Naomba yeyote mwenye dawa ya kuondoa mvi anijulishe kupitia humu malipo hayatakuwa na shida.
 
Wanajamvi naomba kufahamu sababu zinazosababisha mtu kuota mvi katika umri mdogo. je kuna dawa ya kuondoa tatizo hilo?
 
Wanajamvi naomba kufahamu sababu zinazosababisha mtu kuota mvi katika umri mdogo. je kuna dawa ya kuondoa tatizo hilo?

mara nyingi huwa ni hereditary tu mkuu na usithubutu sijui utake kuziwekea dawa kwani ndiyo zitakuwa nyingi mithili ya hayati mandela.
 
Mwenyewe nina nyingi mpaka naogopa

Sasa unaogopa nini kiongozi? Au kwa vile huna busara ndo maana unaogopa? Maana mvi mkuu zinaendana na busara na hekima, hivi viwili vikikosekana ni hatari sana lazima uogope!! Hivyo nakushauri ujitahidi kuwa na busara tu pamoja na hekima!!
 
Woga umetokana na umri, unajua jamii wana imani fulani, wakiona mvi wanajua huyu mtu ni mzee, ila swala lsa hekima na busara inanitosha kwakiasi...
 
hivi mtu unaogopa kuwa na mvi kwa nini, zinauma huko kichwani? zinasababisha ukosefu wa nguvu za kiume hapana. sasa kwa nini watu wanaogopa kuwa na mvi. mi ninazo toka nipo form two na sijawahi hata kuzifikilia na huwa naacha afro yangu kwa raha zangu. tujifunze kukubali maumbile yetu, kama una pua kubwa ipende, kama una kipara kipende na kama una mvi zipende na zikubali tu.
 
Habari,

Mi ni kijana, ninayefanya kazi katika kampuni yangu binafsi,

Sina umri mkubwa ila nimeanzaa kuota mvi kwa mbali toka npo chuo,

Ila naona kwa ss znaanza kuongezeka,

Naomba ushauri wenu ili miweze kizidhiti,
Kwani sizipendi na zinanifanya niwe nanyoa nywele mara kwa mara..

Maoni yenu tafadhali.
 
Haina dawa mkuu..ziache tu...mvi na kutoka KIPARA BORA NN?ziache tu..
 
Back
Top Bottom