Dawa ya kuondoa umaskini ni Elimu bora.Hii ya sasa ifumuliwe

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Bila shaka wengi watakuwa wanajiuliza maswali mengi bila majibu kuwa ni kwa nini pamoja na utajiri mkubwa wa rasilimali katika nchi yetu, bado kuna idadi kubwa ya watu wanaishi maisha ya umaskini mkubwa.

Tatizo ni Elimu duni.

Mfumo huu wa elimu inayotolewa nchini, imeshindwa kuamsha ari ya ubunifu kutoka kwa wasomi wetu ili kuweza kujibu maswali ya changamoto zilizopo.

Nini kifanyike?
Kukaa na kufanya tathmini upya kuhusu mfumo huu wa sasa iwapo una tija au la!
Ni nani aliyefanya utafiti kuwa mtoto umuweke shule ya msingi kwa muda wa miaka saba huku ukimfundisha mambo ambayo hata akimaliza, ni chini ya asilimia kumi tu atakuwa anayakumbuka. Wakati mtoto huyo huyo, ukimfundisha ufundi wowote, kwa muda huo,atakuwa na uwezo mkubwa sana na kuwa mwenye ubunifu wa hali ya juu.

Au ni nani alisema mtu asome O level miaka minne halafu aende A level miaka miwili?

Nani alifanya utafiti juu ya elimu zinazotolewa katika vyuo vyetu kama kweli zina toa wahitimu wenye tija?

Leo hata ukiongea na wasomi wengi hasa wanaosoma masomo ya sayansi, watakwambia wanasoma mambo mengi sana magumu yasiyo na tija kwenye taaluma zao. Masomo hayo yapo kuleta ugumu wa kupata tu vyeti ili isije kuonekana kuwa elimu ni rahisi.Lakini kiukweli, hayawasaidii kabisa katika utendaji wao wa kazi.

Kama tusipoamua kufanya maamuzi magumu na makini,tukaendelea kuthamini vyeti badala ya matokeo ya elimu, tukaachana na mifumo ya kizamani ya elimu, itakuwa ni ndoto kwa nchi yetu kuagana na umaskini.
 
Mkuu huu ni mjadala muhimu sana na mzito pia, bila elimu bora umasikini hauwezi kutokomezwa. Watawala wanachezea sana elimu yetu watakavyo, nakumbuka nilipokuwa kidato cha pili waliunganisha physics na chemistry likawa somo moja "Physics with Chemistry" na mwezi mmoja kabla ya NECTA ya form two wakazitenganisha tena na tukatakiwa kufanya mtihani kivyake kwa kila somo.

Kuna mambo lazma yaborehwe kwenye hii elimu ya sasa ili iendane na uhalisia wa kumudu chalenge za maisha kwa wahitimu, Ukiangalia masomo ya Advance hata Chuo na college zote bado yanamjenga mhitimu kuwa tegemezi, muoga wa maisha mwenye kusubiri ajira, asiye jiamini na asiye kuwa na mbinu za kumudu maisha yake kwa kutumia ujuzi aliosomea
 
Hoja yako ni ya msingi sana sana:
Natamani sana huu uwe mjadara wa kitaifa. Tunazeekea shule kupewa maarifa finyu sana na kuzidi kuwa tegemezi.

1. Tunahitaji sana technical skills katika ngazi ya chini na Kati
2. Tunahitaji elimu Bora ya kilimo Cha mazao, misitu, uvuvi na ufugaji
3. Pia tunahitaji elimu ya sayansi mwendana na Kasi ya dunia
Hatuhitaji Kila mtu afike chuo kikuu. Wachache waende wawe chachu ya mabadiliko huku chini.
Tunahitaji mjadala mpana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wanasomesha watoto wao nchi kwenye mifumo mizuri ili waje kututawala sisi, CCM haitaki watanzania wapate elimu bora maana wataanza kudai haki zao za msingi.
 
Back
Top Bottom