mkuu ni mawazo mazuri,lakini kama la kuhamisha makao makuu Dodoma linasuasua itachukua muda.Eneo la Kariakoo liwe na bidhaa moja tu ya biashara mfano bidhaa za nguo maduka ya simu na vifaa vya simu yahamishwe mfano Pugu maduka ya vifaa vya ujenzi yote yahamie mfano Tegeta Vipodozi yote yaende mwenge...... vifaa vya kilimo Tandika..... posta yoote kusiwe na maduka zaidi ya maofisi na maduka ya nguo tu... maduka ya furniture yote yaende Keko.. tukiweza hili misongamano na foleni zitakwisha Dar tuige nchi zingine basi..... ingawa Madiwani na mameya wote waliopo ni mizigo...
Aisee, kipi kimekufanya ufikirie hili?
Jana sababu ya hofu ya maandamano ya Sheikh Ponda
watu walifunga mapema maduka,
posta na Kariakoo
matokeo yake foleni ikawa nafuu mno
na wengine hawakukumbana na msongamano kabisa
so maduka ya kariakoo na posta ndo chanzo cha vurugu yote ya mifoleni
yakipunguzwa tu,mji utakuwa tofauti mno
The Boss, dawa ya kuondoa foleni ni KUYAONDOA MAGARI barabarani. Hili ni suala la MIUNDOMBINU. Nilikwishamuelimisha Mwakyembe kuhusu solution. Hebu Google "Kuala Lumpur Monorail" kisha nenda kwenye "images" uone jinsi wenzetu walivyofanikiwa. Kwao foleni wanaisikia kwenye vyombo vya habari tu!
Hofu ya vurugu ILIYAONDOA MAGARI barabarani. Umeona hapo? Kumbe hujui kusoma kati kati ya mistari?
The Boss, dawa ya kuondoa foleni ni KUYAONDOA MAGARI barabarani. Hili ni suala la MIUNDOMBINU. Nilikwishamuelimisha Mwakyembe kuhusu solution. Hebu Google "Kuala Lumpur Monorail" kisha nenda kwenye "images" uone jinsi wenzetu walivyofanikiwa. Kwao foleni wanaisikia kwenye vyombo vya habari tu!
Kwa maoni yangu mimi ni train ziwe kila upande wa dar es salaam..
Na then serikali iongeze bei ya ku park gari mjini mfano sh 5000 kwa saa na iwe strict kweli kweli uone watu wangapi wataenda na magari binafsi mjini....
... Kaka, nasupport wazo lako. Nyongeza ya mbinu nyingine katika kupunguza msongamano ni kuwepo kwa shift pattern kwa wafanyakazi kwenye ofisi nyingi za serikali zilizopo district centre na hata kwenye kampuni binafsi. Mfano, pawepo watu wanaofanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi, wengine saa 4 na wengine saa 6 mchana.
Nina imani kwamba mpangilio kama huo ukiwepo karaha ya foleni za kuelekea mjini asubuhi au kutokea mjini nyakati za jioni itapungua.
Kupunguza foleni Mandela hadi Mbezi malori yatoke bandarini kuanzia saa nne usiku
Mimi ningeweza ningesema wale ambao hawajaajiriwa
mfano wamama wa ferry watoke saa tatu
wakati wenzao wa serikalini wakiwa tayari wao maofisini
na vyuo pia vianze saa tatu
so wa asubuhi wanakuwa ni wafanyakazi zaidi..
kuliko now,unakuta mtu wa benk na mama ntilie wa ferry wote wako saa kumi na mbili barabarani
full vurugu..
... Soko la samaki Ferry lihamishiwe Msasani bhana. Serikali inunue kiwanja kimojawapo huko ufukweni hata kwa billioni 5 hivi na kujenga soko jingine huku waki phase out shughuli za pale Ferry. Pale pabakie kivuko tu. Walipoamua kuimarisha lile soko kwa mamilioni walifanya makosa kwa maoni yangu, walitakiwa walifunge. Na ile incident ya moto nayo ingelitumika kama sababu ya kulifunga jumlajumla na kuondoa shombo la samaki eneo sensitive kama pale.