Dawa ya kiungulia nini?


N

Nsagali

Member
Joined
Mar 4, 2011
Messages
90
Likes
1
Points
0
N

Nsagali

Member
Joined Mar 4, 2011
90 1 0
habari wandug wana JF nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini
 
kamili

kamili

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Messages
836
Likes
221
Points
60
kamili

kamili

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2011
836 221 60
habari wandug wana JF nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini
Tumia vidonge vinavyoitwa Omeprazole kimoja kwa siku kwa muda wa miezi miwili mfululizo kitakwisha kabisa, hata kabla ya muda huo.
 
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,574
Likes
31,823
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,574 31,823 280
Kiingulia ni acidity iliyozidi kifuatia kula kitu chenye acidity. Maharage yakilala yana ferment hivyo kutengeneza more acidity state hivyo ukiyala vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton vyenye kazi ya kuyeyusha wanga vinatoa acid nyingi ukichanganya na ile ya maharage matokeo yake ni kiungulia.

Dawa ya kiungulia ni kunywa alcalinine yoyote au base ili kuineutralize ile acid na kutengeneza chumvi na maji hivyo kutokuwa na madhara tena.

Dawa ya kawaida sana ni vidonge vya magnesium tricilicate au actal. Majivu yakichanganyika na maji yanatengeneza alcaline solution ambayo pia inaneutralize ile acid. Tatizo la majivu hakuna kipimo sahihi ukizidisha, hata ile acid ya kawaida ya kusaga chakula inakuwa neutralized hivyo chakula kinashuka kilivyo.

Usipotafuta suluhisho la kudumu kuicontrol hiyo acid tumboni kwako, inaweza kumungunya mpaka ngozi laini ta tumboni hivyo kusababisha vidonda vya tumbo vinaitwa ulcers.
 
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Messages
8,065
Likes
283
Points
180
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2011
8,065 283 180
Meza Omeprazole au Lansoprazole.
 
Riwa

Riwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2007
Messages
2,599
Likes
247
Points
160
Riwa

Riwa

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2007
2,599 247 160
Meza Omeprazole au Lansoprazole.
Mkuu hapo naona unataka kuua 'panya' kwa 'gobole'....Nadhani Pasco katoa ushauri mzuri zaidi, Omeprazole au Lansoprazole kwa kiungulia is too much.

Nsagali pia jaribu kuepuka hivyo vyakula vinavyokupa kiungulia, kwani unajiweka katika risk ya kupata vidonda vya tumbo.
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,237
Likes
87
Points
135
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,237 87 135
habari wandug wana JF nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini

Nsagali, mwili unakuambia unaishiwa maji.
ukifikiri kutaka kula chakula fulani au ukikiona chakula na kukifikiria kula au unapokaribia chakula mezani, tumboni kuna kitu kinaitwa 'haidrokroliki aisidi' hutentengenezwa ili kusaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. lakini haidrokroliki aisidi hii lazima ipunguzwe makali (must be neutralized) kabla hujaweka chakula mdomoni, lasivyo pamoja na mambo mengine itakusababishia kiungulia na baadaye itaanza kutoboa kuta za tumbo na kukuletea vidonda vya tumbo.

sasa, inapunguzwaje makali?, kwa kunywa maji glasi mbili kila nusu saa kabla ya chakula. humu humu kwenye JF Doctor kuna post nafikiri page ya pili ina kichwa cha habari; ''Hatunywi maji ndiyo maana tunauguwa'', isome taratibu hasa sehemu ya chini inapoanza kuelezea kwanini unywe maji nusu au robo saa kabla ya chakula.

Chini utasoma namna ya kuitambuwa kiu:

NAMNA MPYA YA KUITAMBUA KIU:

Ikiwa 'mdomo uliokauka au kiu' siyo kiashiria kikuu cha mwili kuhitaji maji, ni vipi hasa viashiria vya mwanzo na sahihi vya mwili kupungukiwa maji?.


Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj na maoni ya kisayansi, kuna mafungu ya aina mbili tofauti ya hisia, yanayotoa ishara ya kiu ya eneo moja au mwili mzima.Mafungu haya yanajumuisha; Maono ya jumla ya kimawazo na zile ishara kubwa zaidi za dharura za sehemu moja au za jumla za kupungukiwa maji.

Ishara za kimawazo zinajumuisha baadhi ya viashiria vifuatavyo ambavyo vimepewa majina kama 'matatizo ya kisaikolojia', nazo ni: • Kujisikia umechoka (uchovu): sababu maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu.

 • Hasira bila sababu: maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu cha ubongo, mwili unapopungukiwa maji, ubongo unakosa nguvu kushughurika na hali mpya, mawazo na vitendo. Hasira inatokea kuwa ndiyo namna ya ubongo kujibu hali mpya zinazohitaji majibu, "Siwezi kufanya jambo hili”, sababu hauna nguvu za kutosha.

 • Woga na aibu: dr.Batmanghelidj amepata barua ya ushuhuda toka kwa mtu aliyekuwa akisumbuliwa na woga na aibu (agoraphobic) aliyejitibu kwa tiba ya maji.

 • Kujisikia umetengwa na usiyemkamilifu - huwezi kutimiza yale uyatakayo.

 • Kujisikia unaonewa.

 • Kichwa kizito uamkapo asubuhi: hakuna nguvu za kutosha kufungua mifumo ya mishipa ya fahamu.

 • Kukosa mantiki au sababu za maana unapoongea au kujibu na kukosa uvumilivu.

 • Kukosa usikivu na ufuatiriaji hasa kwa watoto na vijana; 'Uwezo wa akili wa mwanafunzi unapungua wakati kiasi cha maji mwilini kinakuwa chini ya wastani, kushuka kwa asilimia 2 tu ya uzito wa mwili sababu ya upungufu wa maji, kunapelekea matatizo ya usikivu na ufuatiriaji na uwezo mdogo wa kumbukumbu miongoni mwa wanafunzi'.

 • Kukosa usingizi mororo na kuota ndoto za kuogofya (nightmares).

 • Pumzi fupi, hatua za mwanzo za pumu, inashauriwa pia kunywa maji kabla ya michezo au mazoezi.

 • Utegemezi kwa vinywaji vya viwandani na vilevi (conditional reflex).

 • Kukata tamaa na hasira, ubongo hauna nguvu za kutosha kushughurika na matatizo mapya na unataka kuachana na mada (wacha lipite bwana, liwalo na liwe), ndiyo maana wahenga walipomwona mtu ana hasira, watampa glasi ya maji hata kiasi kidogo cha chumvi.

Kabla upungufu wa maji (dehydration) haujakudhuru kufikia hatua ya umaututi, Mwili utazitoa moja kati ya ishara hizi za pili kubwa na za dharura (emergency calls) za uhitaji wa maji mwilini zifuatazo; vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.

Ishara zingine ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu (BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, utipwatipwa na uzito kupita kiasi, kuzeeka mapema, na ishara nyingine nyingi.

Kumbuka kutembelea: Utangulizi | maajabu ya maji
Unaweza pia kunitumia sms katika 0769779533
 
Vin Diesel

Vin Diesel

JF Gold Member
Joined
Mar 1, 2011
Messages
8,698
Likes
1,243
Points
280
Vin Diesel

Vin Diesel

JF Gold Member
Joined Mar 1, 2011
8,698 1,243 280
Usinunue dawa hosp...lamba majivu utaona maajabu.
majivu ni alkaline so yanaenda ku neutralize acid....
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
29,894
Likes
15,362
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
29,894 15,362 280
duh, asanteni sana mwenzenu hata mimi nina hilo tatizo saaaana kiasi kwamba usiku mara nyingi huwa silali kabisa hadi night kali nadhani chakula kikishameng'enywa....thanks ila kwa maji nakunywa saaaaana hasa ya moto au vuguvugu kiasi kwamba hapa ofisini watu wananuna kwamba nawamalizia maji....kwa maji nakunywa sana
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
29,894
Likes
15,362
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
29,894 15,362 280
majivu ya nini mkuu? huku mjini labda majivu ya mkaa, yanafaa pia? asante
Usinunue dawa hosp...lamba majivu utaona maajabu.
majivu ni alkaline so yanaenda ku neutralize acid....
 
Kaitaba

Kaitaba

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2009
Messages
928
Likes
21
Points
0
Kaitaba

Kaitaba

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2009
928 21 0
habari wandug wana jf nina tatizo moja nikila maharage yaliyolala au yaliyoweka kwenye friji huwa nasikia kiungulia sana labda kama kuna mtu anayefahamu dawa yake huwa ni nini
tumia vidonge vya magnesium vitakusaidia
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,237
Likes
87
Points
135
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,237 87 135
duh, asanteni sana mwenzenu hata mimi nina hilo tatizo saaaana kiasi kwamba usiku mara nyingi huwa silali kabisa hadi night kali nadhani chakula kikishameng'enywa....thanks ila kwa maji nakunywa saaaaana hasa ya moto au vuguvugu kiasi kwamba hapa ofisini watu wananuna kwamba nawamalizia maji....kwa maji nakunywa sana
safi sana Elli kwa kunywa maji saaaaaana hasa ya moto au vuguvugu. Kunywa tu maji ni kazi rahisi kila mmoja anaweza kuifanya, bali kuna formula ya kunywa maji ambayo huyafanya maji kuwa zaidi ya dawa na si tofauti.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri. Ikiwa inakulazimu kukojowa kabla ya masaa mawili kupita baada ya kunywa maji, juwa kabisa kuwa utaendelea tu kuuguwa, bali ukinywa maji kwa formula sahihi hakuna ugonjwa utakaouguwa kwakuwa magonjwa ni ishara za mwili kupungukiwa maji.

Ili kujifunza zaidi, unaweza kusema ni kiasi gani cha maji unakunywa kwa siku, muda gani na ni chumvi gani unayotumia. Ahsante.
 
Kbd

Kbd

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2009
Messages
1,263
Likes
1
Points
133
Kbd

Kbd

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2009
1,263 1 133
Hata mimi nilikuwa na tatizo kama hilo ila sasa limepungua sana. Kuna wakati nilishawahi kunywa dawa zinaitwa NEXIUM (sijui kama nimepatia) ni nzuri sana ila ghali kipindi hicho tatizo lilipungua ila baada ya muda lilirudi. Ni kama mwezi sasa toka nigundue "dawa" ya rejareja. Mi ilifika kipindi nikila chochote baada ya dakika chache naanza kusikia kiungulia na kitanisumbua sana, ila sasa namshukuru Mungu shida imepungua sana sana. Huwa nikimaliza kula sinywi maji baada tu ya kumaliza, nasubiri zaidi ya lisaa limoja au zaidi ndio nakunywa maji...........na wala kiungulia hakipo kabisa. Hivyo nakushauri jaribisha hiyo.........ni haina malipo yaweza kukusaidia. (source ni mimi mwenyewe na wala sina ushauri ya kitabibu)
 
Eliezar Mlwafu

Eliezar Mlwafu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Messages
436
Likes
7
Points
35
Eliezar Mlwafu

Eliezar Mlwafu

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2013
436 7 35
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
M

Maamuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Messages
856
Likes
28
Points
45
M

Maamuma

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2008
856 28 45
Mkuu MziziMkavu njoo utoe msaada tafadhali.
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,249,419
Members 480,661
Posts 29,697,453