Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,113
- 1,658
Wana Jukwaa la JF Shalom Shalom, Assalamu aleykumu, Tumsifu Kristo Yesu.
Bila kuwapotezea mda wadau naomba msaada wa maelekezo kwa mwenye information kuhusu kampuni ya Zion medical ya huko Israel, kuwa ina tengeneza dawa aina ya Gommora ya kutibu H.iv.
Kumekuwa na matangazo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii kuitangaza hiyo dawa, huku ukiwatafuta wanakupa namba wakisema wao ni mawakala wako nchi ya Zambia, na wanakutumia dawa ukituma hela, dawa wanauza dollars 250 ya vidonge matumizi ni siku 21 na kuna ya sindano nadhani dollars 500.
Nina ndugu yangu ana changamoto ya H.i.v nilitamani kumnunulia ila nikaingia woga kufanya manunuzi bila kufanya udadisi na kwa watu wengine nisije tapeliwa, maana naogopa biashara ya kumtumia mtu hela huku simjui.
Nikaona nije hapa kwenye jukwaa huenda kuna wenye uelewa zaidi na jambo hili, pia wadau hivi kwa hapa Tanzania kuna ubalozi wa Israel?
Kama upo nikienda kwenye ubalozi wao kupata usaidizi wa kuunganishwa moja kwa moja na watoa dawa wa Zion medical kampuni. Je, inawezekana?
Asanteni sana.