Dawa ya deni kulipa walimwengu

Dawa ya deni kulipa walimwengu

Raynavero

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
38,380
Reaction score
56,078
Habarini za weekend.

Leo naongelea wale wanaopenda kukopa kurudisha kwao mtihani!

Yaani mtu anakuja anapokua na shida, kwa unyenyekevu kama yuko ibadani anaomba umsaidie kiasi cha pesa na wewe tena ubinadamu kama mother Theresa unampa
kiroho safi ili asiumbuke mjini!

Siku zinaenda,mwezi,Mara miezi miwili hakumbushii wala kusema chochote,unaamua kujitoa mhanga unamuulizia vipi ile ishu sasa!
mambo magumu Ila njoo tarehe Fulani nikupe chako,ukienda humkuti,simu hapokei meseji hajibu!
Anakutumia meseji za kashfa ukimuulizia kuhusu pesa zako doohh!
Ulivyokua na shida ulikua mpole kama maji baridi!
Loohh!pesa yenyewe nyingii jamani!
Binadamu tujifunze uungwana tukumbuke shida sio siku moja kuna Leo na kesho unaazima cha Mtu kumbuka kurudisha kwa wakati au hata ukichelewesha basi uwe na lugha nzuri ili kesho ukopesheke!

Uungwana ni vitendo!!
 
Hii mbaya zaidi kama uliyemkopesha mko ofisi moja na unamwona anavyo kuwa na matumizi yasiyo na lazima, huku bado hajakulipa.
Cha kushangaza na siku ya kupokea mshahara unaijua na bado anakuambia hana hela.
Tujifunze jamani kukopa hakutaisha leo wala kesho tuwe na utu...hata mkopeshaji ana mahitaji kama ya mkopaji.

Pole geniveros.
 
Jifunze kuwajua watu wanaokuzunguka. Kama mtu anakopa na kurudisha bila shida huyo akija ata usiku wa manane amka na umpe anachohitaji kama kipo.Ukishawajua wasumbufu wao labda uwape bure, yaani bila kuwa na matumaini ya mrejesho.Wasumbufu wakitaka kukopa waambie huna/wazungushe kama wanavyokufanyia.
 
Mmoja kaniambia mwisho wa mwezi nakulipa, Leo tarehe 3 sijui mshahara kwao bado haujatoka
 
Ndo tatizo la kukopeshana kiholela hilo.hata dini inasema unapomkopesha mtu muandikishane na wawepo mashahidi.ukitaka mtu asikuzungushe kwenye malipo akija kukopa awe na dhamana na muandikishane unless ni pesa ndogo kama alfu 10 tu 50
 
Ogapa sana watu wanaomtanguliza mungu na kutaja baadhi ya maneno ambayo yapo katika vitabu vya dini ukipata hela labda umuweke ndani kwanza(kituo cha polisi)
 
Kati ya vitu ambavyo siwez nikufwatilia deni izo biashara zakuambiwa njoo kesho siziwez wengine sio wastaarab nn kukutukana juu,

bora nimnyime Tu kuliko kuanza kusumbuana kwa maneno yasiyo pendeza

kwani nimesema sikulipi usinsumbue na icho ki pesa chako ,
 
Halafu kuna wengine wanapokuzungusha namna hiyo wanakuwa wanajiona wajanja sana.

Ndo maana mimi sasa hivi nimeamua kuwa mchoyo tu.

Na nilivyo na msimamo sasa..hahaa.

Potelea mbali, ima fa ima!
Yaani sasa hv na mie nataka nianze roho mbaya,maana unamuazima kiubinadamu Ila kwenye kulipana jamani mpk mtoleane maneno mwingine anakuambia kabisa
Sikupi sasa utanifanyaje?!daah!
 
Hii mbaya zaidi kama uliyemkopesha mko ofisi moja na unamwona anavyo kuwa na matumizi yasiyo na lazima, huku bado hajakulipa.
Cha kushangaza na siku ya kupokea mshahara unaijua na bado anakuambia hana hela.
Tujifunze jamani kukopa hakutaisha leo wala kesho tuwe na utu...hata mkopeshaji ana mahitaji kama ya mkopaji.

Pole geniveros.
Kuna mtu namdai yani kaniambia hana hela juzi kanunua simu jamani loooh!!halafu ofisi mja daahhh!!
Inakera sana ujue yani wanaangalia matatizo yao ya kwake hawayafikirii!!
 
Kati ya vitu ambavyo siwez nikufwatilia deni izo biashara zakuambiwa njoo kesho siziwez wengine sio wastaarab nn kukutukana juu,

bora nimnyime Tu kuliko kuanza kusumbuana kwa maneno yasiyo pendeza

kwani nimesema sikulipi usinsumbue na icho ki pesa chako ,
wee acha tu anajibu hvyo hvyo!!
Tena hawa ndugu ndio hatari zaid ukiwakopesha!
Ndugu washanifilisi sina hamu natamani Julia!sijapewa hata mia!
 
Ndo tatizo la kukopeshana kuholela hilo.hata dini inasema unapomkopesha mtu muandikishane na wawepo mashahidi.ukitaka mtu asikuzungushe kwenye malipo akija kukopa awe na dhamana na muandikishane unless ni pesa ndogo kama alfu kumi au hata 50
Ubinadamu nao ndo unatugharimu sana,unampa mtu kiungwanvna unaamini hatokuangusha mwisho wa siku inakula kwako!
Mmoja kaniambia mwisho wa mwezi nakulipa, Leo tarehe 3 sijui mshahara kwao bado haujatoka
Kashakuachia manyoya huyoo!!
Jifunze kuwajua watu wanaokuzunguka. Kama mtu anakopa na kurudisha bila shida huyo akija ata usiku wa manane amka na umpe anachohitaji kama kipo.Ukishawajua wasumbufu wao labda uwape bure, yaani bila kuwa na matumaini ya mrejesho.Wasumbufu wakitaka kukopa waambie huna/wazungushe kama wanavyokufanyia.
Asante kwa ushauri nataka na mie niwe USO wa mbuzi
 
Halafu kuna wengine wanapokuzungusha namna hiyo wanakuwa wanajiona wajanja sana.

Ndo maana mimi sasa hivi nimeamua kuwa mchoyo tu.

Na nilivyo na msimamo sasa..hahaa.

Potelea mbali, ima fa ima!
Kwa hiyo katika ile request ya US$500 niandike maumivu?
 
Ubinadamu nao ndo unatugharimu sana,unampa mtu kiungwanvna unaamini hatokuangusha mwisho wa siku inakula kwako!

Kashakuachia manyoya huyoo!!

Asante kwa ushauri nataka na mie niwe USO wa mbuzi
Halafu elf15 ikakutoe thamani kweli, duh
 
Back
Top Bottom