Dawa ya deni kulipa walimwengu

Dawa ya deni kulipa walimwengu

Kwa nini ukopeshe?? Kuna watu ama taasisi znahusika na kukopesha na kudai madeni.

Kukopesha bila riba ni kuingilia biashara za watu na mabenki.

Sishauri mtu asiyena uzoefu wa kukopesha na kudai akopeshe
 
kuna watu wanaona vya wenzao sijui mavi
kuna mkaka ofsini ni ndugu yake boss wangu kijana ana hela jamani anaweza kuja na burungutu la hela ukamuomba mia tano ya soda atachomoa tu mia tano yaani
Wewe ndio wale unaomba 10,000 likitoka bundle la 1m unabadili dau 'fanya 50,000 basi'
 
Ukitaka kuondoa kero ya omba omba mkopeshe hela. Halipi na hatarudi kukusumbua tena.
 
Tena sikuhz wadaiwa wanalugha yao utafikiri wameambiana utasikia "JAMAA ANABANA ASE PESA IMEKUA NGUMU NIVUMILIE" KLMY wakat unakopa hukujua pesa ni ngumu, kuna siku pesa imekua rahs.
 
Kuna mtu namdai yani kaniambia hana hela juzi kanunua simu jamani loooh!!halafu ofisi mja daahhh!!
Inakera sana ujue yani wanaangalia matatizo yao ya kwake hawayafikirii!!
Shost unahangaika nini, siku hizi hakuna kukopeshana kienyeji na mwendo wa kuandikishana tu, inasaidia sana hasa pale unapomkamata na askari...narudia baadhi ya watu ambao sio walipaji bila Polisi hupewi hela ako ( japo utamkatia genji askari aliyefanikisha)
 
Mi nilikuwa nalia kama mtoto mdogo zamani, askari msimbazi best yangu ndo akanipa maunjanja, nisikopeshe mtu, mosi bila kuandikishana, collateral ni muhimu, mashahidi sio lazima...sasa nakopesha hela na riba juu kama sina akili nzuri, ole wako unirushe sasa! Utaenda kulipa zaidi ya nilizokukopesha Polisi!!
 
Yaani muda mwingine unajikuta ukimuona unayemdai mpaka hasira zinapanda.
Akiwa na shida sasa atalia wee mpaka utamuonea huruma kwenye kulipa sasa ndo issue tena hadi vibaya utajibiwa.
Mbaya zaidi uwe hujui kudai ndio hupewi kabisaa.
Kuna mmoja ni mtu mzima kanizidi nilimkopesha hata si hela nyingi ila sasa mwaka umeisha silipwi.Tena mwanzo kila tukikutana alikuwa ananambia nskumbuka lakini siku hizi hata hagusii.
Nimeamua kumuacha sitamuuliza ila siku akipata shida nitamkumbushia ili ajue dawa ya deni kulipa
 
Halafu wengine sijui wapoje yaani anaweza akurushe au akuzungushe wee lakini akija tena kukopa unajikuta unampa wakati ulishaapa hutomkopesha tena.
Hapo ndio nachokaga kabisa yaani unabaki unajiuliza imekuwaje nikampa?
 
Kuna mmoja nilimkopesha mwez wa tano,,,mpka leo hajanilipa.nmeamua nsimkumbushe teeena,laki mbili kitu gan bhana#
 
Daaah!! Hadi umenikumbusha machungu.
 
Yaani sasa hv na mie nataka nianze roho mbaya,maana unamuazima kiubinadamu Ila kwenye kulipana jamani mpk mtoleane maneno mwingine anakuambia kabisa
Sikupi sasa utanifanyaje?!daah!
Hii mie nishajiapiza weeh lakini wapi!!
 
Back
Top Bottom