Dawa ya CHADEMA yapatikana

Dawa ya CHADEMA yapatikana

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
mzee tupatupa mafanikio yenyewe ya kuonyesha yako wapi?
 
nitarudu......but vipi kuhusu Bukoba hawajatoa uamuzi
 
Wakifanya hivyo itapendeza.

Swali ni, Je wataweza?
 
Huo mradi wakuonyesha mafanikio walishauanza tangu mwaka jana lakini naona ulifeli,

Walijikuta wanaingia gharama kubwa sana kulipia matangazo yao kwenye vyombo vya habari huku wananchi wanazidi kuwakataa,

Tunawasubiri tena karibuni!
 
Hizo ni porojo na ndoto za Mchana kweupe!! afu ujue hao ni waalikwa ambao lazima wapewe posho angalau kwa kusema chochote.!!!!!! Watatuonyesha kwa vitendo gani? kwani hatuoni? Labda wawaonyeshe akina Obama wageni wa siku moja lakini tunaishi kwenye umaskini uliokubuhu, tunaishi kwenye ufisadi na tunaishi kwa hofu inatokayo kwa hao wanaowakata bwatu vidole, kung'oa kucha na kuteka watu mbalimbali.

Huyo aliyetoa mawazo hayo yeye katika kipindi chake tutamkumbuka kwa yapi? Hao jamaa wajue tu kwamba safari yao ndo ishafika wajiandae tu kwenda chobingo kama KANU ya Kenya.

Tumeonewa kiasi cha Kutosha, Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, Unyonge wetu ndio umetufikisha hapo. Hatudanganyiki? Peoples poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer?
 
Lakuvunda halina ubani! Eti Baraza la Wazee, kisa M/Kiti wao kaona vusasi vinamtokea puani huku li Chama likimuozea. Hivi kwa miaka miwili iliyo baki watafanya maajabu gani kiasi kwamba waTanganyika waweze kuyaona mafanikio kwa macho? Kwa CCM ya sasa tunayo ijua, kila mwenye madaraka yupo busy KUFISADI maana wanajua hii ndio lala salama.

Si tuliyaona kwenye awamu ya NNE jinsi watu walivyo jimilikisha kila kilicho kuwa kina wezekana!!

Huyo sijui Katapila alisha choka mbaya, hivyo hana lolote jipya zaidi ya kufurahia kukumbukwa angalau aweze kuhudhuria vikao kwenye hilo ghala lao la kujadili ujinga hapo Dodoma.
 
Huo mradi wakuonyesha mafanikio walishauanza tangu mwaka jana lakini naona ulifeli,

Walijikuta wanaingia gharama kubwa sana kulipia matangazo yao kwenye vyombo vya habari huku wananchi wanazidi kuwakataa,

Tunawasubiri tena karibuni!

Kwani lengo la Big results NOW NI NJE YA HUO MRADI WAO MWINGINE? Wahenga walishasema mfa maji haachi kutapatapa. Anguko linakuja kama usingizi. Je ni nanio ambaye alishawahi kujua muda, yaani dakika na sekunde ya kupata usingizi>? Sio mama wala baba kitandani hutawanyika kivyake. Waacha wafu wazikane wenyewe kwa wenyewe.
 
Hizo ni porojo na ndoto za Mchana kweupe!! afu ujue hao ni waalikwa ambao lazima wapewe posho angalau kwa kusema chochote.!!!!!! Watatuonyesha kwa vitendo gani? kwani hatuoni? Labda wawaonyeshe akina Obama wageni wa siku moja lakini tunaishi kwenye umaskini uliokubuhu, tunaishi kwenye ufisadi na tunaishi kwa hofu inatokayo kwa hao wanaowakata bwatu vidole, kung'oa kucha na kuteka watu mbalimbali.

Huyo aliyetoa mawazo hayo yeye katika kipindi chake tutamkumbuka kwa yapi? Hao jamaa wajue tu kwamba safari yao ndo ishafika wajiandae tu kwenda chobingo kama KANU ya Kenya.

Tumeonewa kiasi cha Kutosha, Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, Unyonge wetu ndio umetufikisha hapo. Hatudanganyiki? Peoples poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer?

Ahsante!!!!
 
Mafanikio mpaka yaoneshwe. Kama hayo ndio mawazo ya wazee wanaoaminiwa kuwa na busara na washauri, CCM kwisha habari yake.
 
hawawezi kufanya hivyo. hivi Nape Nnauye amesikia haya maoni ya mzee wetu?
 
Last edited by a moderator:
...ushauli mzuri lakini watakelezaji na muda ndo kikwazo...
 
nyie hamjui mafanikio wanayotaka kutuonyesha? Deep green, meremeta, kagoda, Epa, richmonduli, twin tower, iptl, dowans, mauaji ya mwangosi kutaja machache tu kuyataja magamba hoyee! Miaka 50 ya ufisadi
 
Dawa ya CHADEMA na wapinzani wengine imepatikana. Mjumbe mmoja wa Baraza la Wazee la CCM Taifa amependekeza kikaoni Dodoma kuwa dawa kuu ya wapinzani ni kuwaonesha wananchi mafanikio ya chama tawala kwa matendo. Mjumbe huyo ambaye alikuwa Makamu wa CCM Tanzania Bara amesema kuwa wapinzani kama CHADEMA hawatakuwa na la kusema ikiwa wananchi wataona mafanikio yaliyoletwa na CCM kwa macho yao wenyewe.

'Hakuna haja ya kutumia nguvu. Kuonesha tu kutatosha. Tukifanya hivi,chama chetu kitaimarika zaidi na kuzoa kura kwenye uchaguzi wowote. Tuachane na propaganda...tuitekeleze Ilani kwa matendo' alisema Mjumbe huyo

Ni matumaini yangu kuwa hata matumizi ya vyombo vya dola kuimarisha chama na kuusumbua upinzani sasa yatapungua au kukoma kabisa. Hakuna haja ya kukamata wala kushtaki wapinzani.CCM yetu yaweza kufanya jambo la kuonesha mafanikio kwa manufaa makubwa.Ni wakati sasa wa kufanya siasa kwa vitendo. Vyombo vya dola(kama alivyowahi kusema Mwenyekiti wa Taifa) havitakisaidia chama chetu cha Mapinduzi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Jamani tuache mzaha hivi kweli watanzania hawana macho ya kuona wenyewe hadi wasubiri waoneshwe hayo maendeleo? Au yamekuwa vijidudu vya malaria hayaonekani mpaka kwa kutumia darubini!!!
 
Tumeonewa kiasi cha Kutosha, Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, Unyonge wetu ndio umetufikisha hapo. Hatudanganyiki? Peoples poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer?
Serekali yangu haitokani na mimi ,haijui mimi ni nani na huijui mimi ninataka nini sina hali kwa kweli!
 
hizo ni porojo na ndoto za mchana kweupe!! Afu ujue hao ni waalikwa ambao lazima wapewe posho angalau kwa kusema chochote.!!!!!! Watatuonyesha kwa vitendo gani? Kwani hatuoni? Labda wawaonyeshe akina obama wageni wa siku moja lakini tunaishi kwenye umaskini uliokubuhu, tunaishi kwenye ufisadi na tunaishi kwa hofu inatokayo kwa hao wanaowakata bwatu vidole, kung'oa kucha na kuteka watu mbalimbali.

Huyo aliyetoa mawazo hayo yeye katika kipindi chake tutamkumbuka kwa yapi? Hao jamaa wajue tu kwamba safari yao ndo ishafika wajiandae tu kwenda chobingo kama kanu ya kenya.

Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha, unyonge wetu ndio umetufikisha hapo. Hatudanganyiki? Peoples poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer?
mia mia kamanda!!!!
 
Back
Top Bottom