Wakuu, naomba kujua ni dawa ipi nzuri na ina kinga za
kutosha kwa meno? Nilikuwa sina tabia ya kuangalia lebo
lakini sasa inanibidi kwani kuna dawa nilitumia meno yakawa na
ganzi.
Pole ndugu -kusema kweli hakuna cha colgate wala sensodyne na ndugu zake.Ngoja tuelimishane kidogo- kufa ganzi kwa meno ni dalili za
1.matatizo ya fizi
2.Hatua za awali za kutoboka kwa meno
3.Kurika kwa Meno(Attrition)
MATATIZO YA FIZI
Yawezekana kati ya meno na fizi kuna mgando mweusi au njano bila shaka umefanya jitihada za kuutoa bila mafanikio au kinywa kina harufu mbaya au kila usafishapo meno kwa mswaki damu zinatoka katika fizi-dalili hizi na hali hii inasababishwa na bacteria ambao hawatolewi vema mara zote usafishapo menoi.Hali hii inapoachwa bila matibabu kwa muda mrefu sumu za bacteria huaribu umahiri wa fizi na kuacha sehemu ya meno inayofunikwa na fizi wazi hivyo kusababisha meno kufa ganzi au kusisimuka mara baridi iingiapo kinywani.
2.Hatua za awali za kutoboka kwa Meno
Jino kuuma lina hatua zake-hatua za mwanzo kabisa ni ganzi pindi unapokunywa/kula vitu baridi chachu au moto.hatua ya pili ni mchanganyiko maumivu/ganzi ulapo/unywapo vitu baridi,chachu au moto.Hali hii inasababishwa na tindikali itolewayo na bacteria wanapotumia mabaki ya sukari(carbohydrates).
3.Meno kurika(attrition)
Meno yana sehemu ya nje kama kioo inaitwa Enamel Inayofuata inatwa Dentin kisha Pulp ambapo kuna mishipa ya fahamu na damu-mabadiliko ya unene wa sehemu ya nje (enamel)husababisha sehemu ya pili Dentin kuwa wazi hali isiyotakiwa kwan kuna mawasiliano kati ya Pulp na Dentin.Hali yaweza sababishwa na;
1.Kutafuna meno wakati tume sinzia-Hali hii husababishwa na Msongo wa mawazo,Kung'oa meno au ajari iliyosababisha kubadilika kwa milinganyo ya taya.
2.Kuugua au ujauzito unaosababisha kutapika kupita kiasi(tumboni kuna tindikali).
3.kupiga mswaki kwa nguvu as if unaondoa Super glue ktk meno!
Dawa gani utumie.
1.NI VIZURI KUMWONA DAKTARI WA KINYWA NA MENO.
2.FUNDISHO -Unaposikia ganzi/maumivu katika meno maana yake uwiano wa Kutoka kwa madini katika jino(Demineralization)Kurudi kwa madin katika jino(Remineralization) haupo.Dawa pekee ya kurekebisha hali hiyo ni FLOURDE.Utaihisi kama pipi kifua vile ila FLOURIDE ni sumu kiwango salama ni 500-1500 parts per million(
ppM).
UNUNUAPO DAWA YA MENO SOMA INGRIDIENTS ktk box mara nyingi maandishi madogo sijui kwa nini-Pamoja na ingredients nyingi utaona katika mabano
500ppM au
1000ppM au 1450ppM-Dawa kwa watoto isizidi 500ppM.
Dawa pia zina sub-brand Hasa utaona zimeandkwa
WHITENING au
SENSITIVE kuwa makini na BLAHBLAH WHITENING ni kama zina dawa ya kuondoa madoa au zina msasa ndani yake Sasa fikiria meno yakisagana yenyewe ni inshu Je ukisugua kwa msasa.SINSITIVE zipo vizuri maana zina FLOURDE yakutosha.
Ndugu yangu usiangalie Trade name angalia ingridients.