Dawa hii ya mitishamba ina walakini ichunguzwe

Ulijuaje na hao wawili wana shida ya namna hiyo?
 
I concur with u japo mie sio bwana mdogo. Nitakupataje ndg
ok sawa ndugu yangu unajua hizi mambo huwa mara nyingi zinashughulikiwa na vijana barubaru, njoo PM tu mkuu tuelezane tu
 
Haya madawa mengine tuwe waangalifu sana,sijawahi kusikia dawa inatibu multiple disease tena na magonjwa ya mishipa ya damu na moyo???? Akili za kuambiwa changanya na zako
Yani ni zaidi ya antibiotic kama kikombe cha babu
 
Kama ni nguvu za kiume anza jogging halafu mitandao imewaharibu utakuta hata hauna tatizo shida ni kusikiliza watu oh nafanya masaa ni uongo mtupu.
 
Napenda kujua elimu yako kama uliishia darasa la ngapi.
Pakiti inaonesha dawa imetengenezwa MBY-TZ yaani Mbeya Tanzania na namba za simu ni za mtengenezaji siyo za muuzaji. Nakushauri unapokuwa kwenye pombe usipende kununua vitu kwa ushabiki wa kilevi, dawa hiyo haina anuani kamili ya mtengenezaji, hata hivyo haujapata hasara kwani majani ya maharage au kunde ni mboga nzuri kwa ugali wa muhogo.
Mwisho ungemuomba mkaijaribu ubora wake kwani hapo Chako ni Chako vyumba vipo; Karibu kwenye chupa ya babu feri Dar es Salaam, bei ni rahisi shilingi elfu tatu tu.
 
Ungekuwa karibu ningejaribu na wewe!!!
 
Hizi namba zilizooneshwa hapo ni namba za huyo muzaji Subira wacha ujuha,ungeuliza kwanza kabla ya kutoa povu. We we umeishia darasa LA ngapi!!?
 
Haki ya Mungu ngono zinalimaliza taifa hili si kwa Std tu hata maradhi ya figo.
 
Pendelea kunywa mchemsho wa samaki kwa wingi mara kwa mara, fanya mazoezi walau nusu saa kwa siku, kunywa maji mengi kiasi cha zaidi ya lita mbili kila siku, kula matunda na mboga mboga kila mara kwenye menu yako, Asali+tende na maziwa iwe sehemu ya lishe yako nyumbani, Unga mboga zako mara kwa mara na karanga mfano msusa, mchicha, nyama nk..

Nenda kapiga gemu baada ya hapo, kama huoni tofauti yeyote ujue utakuwa na Kisukari, na magonjwa mengine hatari kwenye mwli wako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…