Ndiyo, inawezekana mwanaume akawa na erection (uume kusimama kawaida kabisa) lakini asiwe na hamu ya tendo (sexual desire/libido). Hii hali inatokea kwa sababu erection ni zaidi ya mchakato wa mishipa ya damu na neva, wakati hisia za ngono zinategemea ubongo, homoni na hali ya kisaikolojia.
Sababu kuu zinazoweza kupelekea hali hiyo:
1. Kisaikolojia β msongo wa mawazo, huzuni, wasiwasi, depression, migogoro ya kifamilia/kihisia. Pia kujichua kwa muda mrefu.
2. Homoni β kupungua kwa testosterone au matatizo ya mfumo wa endocrine.
3. Dawa na afya ya mwili β baadhi ya dawa (mfano antidepressants, dawa za presha, dawa za usingizi) hupunguza libido. Hata magonjwa hayo huweza kuleta hiyo hali hatakama haujaanza kutumia dawa.
5. Sababu za kimazingira/kihisia β kuchoka, stress ya kazi, kukosa usingizi ( kama nilivyogusia kwenye mada #2) au kukosa mvuto na mwenza kutokana na sababu za kissikolojia kama uzuri, hadhi, afya n.k
Nb: morning erections β kawaida kabisa kwa mwanaume mwenye mishipa na neva zenye afya. Haziashirii lazima kuwa na hamu ya tendo, bali zinaonyesha mfumo wa damu na mishipa unafanya kazi vizuri, ingawa hormones huusika kwenye mchakato wa hisia
Kama erection ipo lakini hamu haipo, tatizo mara nyingi ni libido siyo mfumo wa mishipa ya uume.
Fanya vipimo vya homoni (testosterone, prolactin) na pia tathmini ya kisaikolojia/stress na sababu zinaendana na hizi.
Hali hii inatibika kutegemea chanzo chake β ikawa ni stress, inarekebishwa kisaikolojia; ikawa ni homoni, dawa/tiba inaleta mabadiliko hasa za asili.
Post ya vyakula vinavyo ongeza hamu ya tendo
link