David Mosha anatutafuta nini watu wa Moshi?

David Mosha anatutafuta nini watu wa Moshi?

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,346
Reaction score
9,846
Mungu atuepushie mtu huyu anayewaza fujo kila kukicha.
Mgombea huyu wa CCM Moshi mjini sasa amekuwa tatizo kwa wakazi wa Moshi.

Anasema yeye ni mzaliwa wa Moshi,eti hataki kuona bendera za Chadema Moshi...!!!!

Mtu huyu aliyeajiri mabaunsa kwaajili ya kupiga watu, mabaunsa wanaopiga mpaka Polisi na Bado Polisi wanambeba,wanamhusudu....!!!!

Nawauliza watanzania na watu wa Moshi,nawauliza hasa vijana wa Moshi,Mosha ni nani mpaka atunyime usingizi? Hawa mabaunsa wana nini mpaka watudhalilishe mbele ya wake na watoto wetu?

Mosha mwenyewe anajigamba kuwa hata kama akishindwa lakini atakuwa amewakomesha watu wa Moshi!

Wazee,vijana wenzangu,Wamangi...tukimchekea huyu bwana atatuaibisha.
Swali ni kuwa,tuko tayari kuaibishwaaa??

Mimi siko tayari!
 
watu waliopata utajiri chini ya utawala wa jk wana majivuno kweli.!!
biashara ya ..... imewainua sana
 
Yahaya amekata tamaa kabisa na ndio maana anafanya vituko.
Mfano juzi jumapili alienda kublock njia ya KDC kwenda kwa Ndesa mwishowe kaishia kutimliwa kwa aibu.
NB
Godless Lema timiza ahadi yako ya kutuletea machalii wa chugga maana huyu Yahaya amezidi sasa
 
Huyu mtu hafai kabisa kuwa kiongozi, kila kukicha anawaza vurugu tu, anaongoza kwa kutoa bendera za chadema, juzi ndo alikua chanzo kikubwa cha vurugu za RAU, Anahonga vijana na mabaunsa wawapige wafuasi wa chadema, kahonga ngazi zote za polisi mji mzima.

Moshi tulizoea kufanya chaguzi za amani miaka yote , ila tangu huyu mtu aje, watu tumekua na hofu ya maisha yetu pande zote za mji wa moshi,
 
Kama ni kweli ccm ijiangalie . Chama mkoa wakae nae aelekezwe siasa za kistaarabu.
Hata akikosa ubunge sasa bado anayonafasi nzuri 2020 bado yanki. Aweke base kwa sasa
 
Mwacheni jamani, mtu ana frustrations zake ni kama dubu mwenye watoto, ni kama nyati aliye jeruhiwa. Boss wake kajitangazia kufilisika, ameuza ma- petrol stations yake Arusha na sasa tunasikia kauza na Home Shoping Ceter sasa wadhani Mosha ana amani?? Huku Moshi, vijana wapumbavuuu na Malofaaa wakamlambia fedha yake yoote aliokuja nayo. Akidhani kura hununuliwa, watu wamelishwa kitu moto pale Kb mpaka wamekinai. Kumbe kula ccm kura CDM. Moshi, nimeipenda bure.
Lazima Mosha achanganyikiwe. Yahaya unaishi wapi, Yahaya eeeeeeh. Nazo kura hatuzikupi, yahaya eeeeeeh
 
Huyu ameanza kupanic, ni miongoni mwa wagombea walioambiwa watumie gharama zao wakishinda wapeleke invoice warudishiwe gharama walizotumia, sasa kama kaona dalili za kushindwa lazima apanic na kudhani ubabe utasaidia.
 
Back
Top Bottom