Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,345
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania, David Mataka amekutwa na hatia ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi 300m.
Kesi yake ilikuwa ikinguruma leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, tarehe ya hukumu itapangwa.
Habari zaidi zinawajia..
================
Kesi yake ilikuwa ikinguruma leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, tarehe ya hukumu itapangwa.
Habari zaidi zinawajia..
================
Usahihi: David Mataka amekutwa na kesi ya kujibu, hakukutwa na hatia bado.
Jana, mkuu Mphamvu aliweka uzi kwenye Jukwaa la Habari na Hoja kuwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) David Mataka amekutwa na hatia na hukumu itapangwa siku nyingine. Nikiwa na heshima kubwa kwa Mkuu Mphamvu na wengineo, naomba kuweka sahihi jambo hili katika mtazamo wa kisheria.
David Mataka na wenzake wanashtakiwa na Jamhuri kwa makosa ya kuisababishia hasara Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao wakiwa ATCL.Kilichofanyika jana ni kutolewa kwa uamuzi mdogo ikiwa washtakiwa (Mataka na wenzake) wana kesi ya kujibu au la.
Hii hufuatia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwasikiliza mashahidi wa upande wa Jamhuri. Mashahidi zaidi ya kumi walipelekwa Mahakamani hapo na Jamhuri na kusikilizwa. Kimsingi, jana akina Mataka walisomewa uamuzi mdogo ambao uliwaona kuwa wana kesi ya kujibu na hivyo wanapaswa kuanza kujitetea.
Wasingekutwa na kesi ya kujibu jana, wangeachiwa huru. Kwa sheria na taratibu za kimahakama hapa Tanzania, siku ya hukumu ndiyo ya kukutwa na hatia na kuhukumiwa. Ndiyo kusema, hukumu hailali. Akina Mataka wataanza kujitetea chini ya kiapo kuanzia tarehe 10 na 11 Disemba mwaka huu.