David Beckham yupo Tanzania

Habari wana JF, nimeona picha instagram David Beckham yupo na watoto wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

Hapa ndiyo serikali yetu upande wa utalii inapofail, ingekua wenzetu Kenya mtu kama Beckham wangetangaza ujio wake kwa kiasi kikubwa.

Mwenye taarifa yoyote kuhusu ujio wake anaeza akatoa maelezo.
 
waulize wakazi wa kipawa waliiona hiyo ndeg wakat inakuja
 
Kama kaja kutalii tu haina haja ya kumtangaza, acha ainjoi privacy na familia yake. Angekuja kwa madhumuni mengina kama vile kupromoti soka au ziara ya kikazi angetangazwa. kama kaja kimyakimya wacha akae kimyakimya na ataondoka kimyakimya. kwanza ni mtu wa kawaida tu, kuna wabongo wengi tu hawamjui wala hawajawahi sikia jina hili.
 
Tanzania bado inaushamba mkubwa kibiashara ukilinganisha Kenya!
 
Ndio maana kuna Google. Kutowahi kwako kulisikia jina la Beckham hakumfanyi Beckham kuwa mtu wa "kawaida."

Kuna watu wengi hawawafahamu Einstein na Newton. Hata mimi siwafahamu ila naelewa sio watu wa "kawaida."
 
kama unaamini beckam si mtu wa kawaida nenda kampokee basi. Usipende kuabudu watu
 
Ndio maana kuna Google. Kutowahi kwako kulisikia jina la Beckham hakumfanyi Beckham kuwa mtu wa "kawaida."

Kuna watu wengi hawawafahamu Einstein na Newton. Hata mimi siwafahamu ila naelewa sio watu wa "kawaida."
Mimi nilivyoisoma comment yake imebidi nicheke tu na kukaa kimya.
 
Nilimuona na nikampiga na ile sweet smile yake, na kumtajia jina alipachikwa enzi hizo. picha naona uvivu kurusha. Nilirushia wa karibu yangu hukoooo

Juu ya utaliiii, subirini Kenya waibe picha kutangaza yupo nchini kwao.

Hata siwasemi hao wa utaliii, wengi hawajui mengi. Wanabidi wajiongeze kijiditali pia hata kuwa na staff wanaofanya kazi fulani fulani...naona uvivu kuzitaja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…