David Beckham akutwa akiendesha gari huku akitumia simu, afungiwa miezi sita

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
David Beckham amepigwa marufuku kuendesha gari kwa miezi sita baada ya kupatikana akitumia simu wakati akiendesha gari.

Kapteni huyo wa zamani wa England amekiri makosa.

Mahakama imearifiwa amepigwa picha na raia akiwa ameshikilia simu wakati akiendesha gari lake aina ya Bentley 'taratibu' katika foleni.

Beckham, mwenye umri 44, ametozwa faini ya £750, ameagizwa alipe £100 gharama ya kesi na malipo ya ziada ya £75 katika siku saba zijazo.

Jaji katika mahakama hiyo amemuambia hata kama kasi ya gari ilikuwa taratibu kwenye foleni 'hakuna kisingizio' chini ya sheria.

Mwendesha mashtaka amesema: "Badala ya kutazama mbele na kuangalia barabara alionekana akitazama mapajani mwake.'

Wakili wa Beckham Gerrard Tyrrell amesema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United " haikumbuki siku hiyo au tukio hilo".

Aliongeza: "Hakuna utetezi wa kilichotokea, lakini mtazammo wake ni kwamba hakumbuki."

Tyrrell ameiambia mahakama kwamba Beckham hufurahia kuendesha gari.

"Huwapeleka watoto shuleni kila siku na mara nyingine hurudi kuwachukua anapoweza, na kuwanyima hilo ni jambo ambalo hana budi kulikubali," amesema

Ni kinyume cha sheria nchini Uingereza kushika simu wakai unaendesha gari. Mtu anaweza kuadhibiwa kwa kupunguziwa pointi kwenye leseni na kutozwa faini ya £200 - lakini kutokana na uzito wa makosa unaweza kufikishwa mahakamani na ukahukumiwa adhabu kali zaidi.

IMG_20190510_105051.jpeg
 
... sheria nzuri sana hii; iwe introduced Bongo maana huko mabarabarani madereva na simu ni vituko vitupu.
 
Wenzetu wana weledi, ingekuwa huku kwetu hakimu angeomba kupiga selfie na kesi akaishia hapo
 
"Ingekuwa huku...ingekuwa bongo..." Hizi kauli zinachosha sijui kama na huko huwa wanasema "ingekuwa afrika..."!!!
 
... sheria nzuri sana hii; iwe introduced Bongo maana huko mabarabarani madereva na simu ni vituko vitupu.
Mm naamini ipo nakumbuka diamond alilipa faini kwa kurekodiwa kaachia usukani na nge nge zake.
Pili kuna yule dereva wa wimbo wa darasa.

Sema tu hata huko uingereza kwenyewe naamn ni wachache sana wanaoshitakiwa ukilinganisha na wanaofanya hivyoo. Hata beckam mwenyewe nahisi siyo Mara ya kwanza coz hata hakumbuki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom