Data centre: Kifo ninachoenda kuua benki za kigeni nchini

luckman

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,211
371
Habari za muda,

Naomba nichukue fursa hii niyaseme machache sana ambayo naona kama hayataangaliwa kwa kina kirefu kuna hatari sana ya Banks nyingi sana kufunga biashara zake hapa nchini.

Nadhani kwa wale wanaofatilia, siku za nyuma Benki Kuu ilitoa maelekezo kwa Commercial Banks zote nchini kuwa na Secondary Data Centre nchini badala ya kuwa na primary data centre moja ambayo ipo Kwenye nchi inayotoka Bank husika, hili ni jambo zuri sababu lengo ni kulinda data za mteja wetu na kuwa na control locally.

Zoezi hili lazima turudi nyuma tulitazame kwa mapana na marefu na tufikirie tena kama ni sahihi kwa kipindi hiki, kabla ya kujikita Kwenye hoja yeneyewe. Ili kuweka kumbukumbu sawa lazima tukubali kwamba tulichelewa kufanya mambo mengi sana ndani ya sector hii lakini isiwe sababu ya kupandikiza project juu ya project tena ambazo zote ni requlatory, banks zinaumia sana sababu gharama zake ni kubwa sana.

Multinational banks ni nyingi kuliko local banks na ndo zimeajiri Watanzania wengi sana na hizi banks baadhi zimebreak even baadhi bado hazijaweza kutengeneza faida na jitihada zimeendelea kufanyika ili atleast ziweze kutengeneza faida, reports za hili nina uhakika benk kuu wanazo, nadhani huu ulikuwa wakati mzuri sana kwa Benki Kuu kutengeneza mazingira mazuri ya hizi banks kuweza kufanya biashara kwa uhuru na Kwenye fair completion ground.

Labda tuangalie gharama zake ambazo Kwenye benki husika ni kama sunk cost sababu hazina jambo lolote zinaongeza zaid ya cost Kwenye vitabu vya bank, gharama za haraka sana ili kulocalise data centre, yaani kuwa na secondary data hapa nchini sio chini ya Tzs 10bil ambazo kwa namna nyingine Benki Kuu wanazilazimisha benki zitumie ili kuwa na Secondary Data Centre nchini, na hii ni kwa banks zote haijalishi unatengeneza faida au hasara kiasi gani, tuna kila sababu ya kushauri mamlaka zote zinazohusika kuliangalia hii sababu mchango wa hizi banks ni mkubwa sana katika soko la Tanzania.

1. Hawa wameajiri Watanzania kwa asilimia 99.9
2. Wanalipa kodi nyingi mbalimbali kwa serikali
3. Wafanyakazi wao wanalipa PAYE
4. pesa za hawa wafanyakazi zineenda Kwenye mifuko ya jamii na hii mifuko imetumikakwa kiasi kikubwa sana kuemdesha miradi ya serikali

Nashauri tena, madhara ya hii data centre ni makubwa sana Kwenye long run, turudi Kwenye meza ya mazungumzo na kulitazama hili kwa mapana sana.

Najua bank kama DTB washapigwa penalty ya TZS 1BIL sababu ya hii data centre, Bank kuu wanatakiwa kuweka miundo mbinu mizuri sana ili banks zifanya kazi kwa uhuru wenye kufuata sharia badala ya kufrustrate bank.

Ni maoni yangu kama mtanzania wa kawaida, lengo ni kujenga na si kubomoa.
 
hiyo data center ya 10bil ina nini hasa?
bei ya super computers/servers zinajulikana,
gharama za fiber internet zinajulikana
gharama za automatic power back-up zinajulikana.

gharama kubwa itakuja kwenye software licence, ambapo na yenyewe haiwezi kuwa kubwa kiivyo.

In total hata bil 1 haifiki, ikizidi sana labda bil 2.
Hizo bil 10 zinakuja vipi?
 
Back
Top Bottom