Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Lengo la DART lilikuwa ni kuleta usafiri ulio bora kwetu wana Dar, na kila mwana Dar anafahamu kwamba daladala siyo usafiri bora bali ni bora usafiri, sasa kwa kuwa Dart imeanza ningeshauri daladala ziondolewe sasa hivi msipofanya hivyo hamtakuja kuweza kuziondoa tena kwani bado zitaendelea kupata wateja hali itakayopelekea zoezi la kuwaondoa huko mbele kuwa gumu kama siyo kushindikana kabisa, kitakachotokea ni kwamba zitaleta ushindani kwa DART na sidhani kama ninyi au siye wana Dar tunalitaka hilo, hivyo mnapaswa muwaondoe leo na sasa hivi vinginenvyo miaka 5 baadaye tutakuwa bado tuna daladala!
Na hivyo kupelekea zoezi hili kuwa limeshindwa!
Tuithibitishie Dunia kwamba sisi WatanZania tunaweza kuamua jambo na kulifanya kwa ufasaha vinginevyo miaka 10 baadaye Dunia itasema kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo ni standard Dunia nje ya Afrika lkn hayawezekeni Afrika kama vile huu mradi wa DART hivyo ni lazima ufanikiwe kwanza kwa ajili yetu na pia kama heshima kama Waafrika kwamba tunaweza kuendesha mambo kwa mpangilio na ustadi mkubwa kama Dunia nje ya Afrika tu, na kwamba siyo kila mradi mkubwa unaoanzishwa Afrika unakufa!