DART, Mwendo kasi Dar

tulu

Senior Member
Aug 30, 2016
197
145
Mi nashauri kipindi tunahuzuni kubwa namna hii ni vizuri tukachukua hata

Tunasubiria uchunguzi wa polisi kuhusu chanzo cha ajali hii ya Watoto wetu lakini hata zichukuliwe zaidi katika vyombo vyote vya usafiri nchini

Hii ni pamoja na ubora wa nagari yaliyo barabarani, Mwendo , na Sheria za barabarani

Nikianza na DART, dar Mwendo kasi mi huwa najiuliza mbona dar tumejisahau na kuamini haya magari kama yameshuka kutoka mbinguni hayatapata ajali hata siku moja

Nagari haya ya Mwendo kasi yanavojaza watu ni hatari sana , Kwa nn mpaka hatari itokee ndo tuwaajibishe watu

Dart wawajibishwe kabla ya kusababisha hatari, tusipokuwa makini na usafiri wa dart utatuletea huzuni ya kudumu mbeleni

Mamlaka za usafiri zitusaidievkilichotokea arusha kimenipa hofu hivi leo GARI la Mwendo kasi likianguka lina siti sijui hata 30 hazifiki limebeba watu karibu 80 wamesimama. Dar es Salaaam tunategemea nn kama siyo huzuni ya kuyisha kutokana na usafiri huu

Serikali itusaidie Kwa hili ikishindikana daladala zirudi ili mtu achague awahi kufika au asafiri Kwa usalama zaidi

Tuchukue hatua jamani taifa linatutegemea
 
Hatari kwelikweli, mara nyingi mpaka yatufike ndio tunaamka
 
Mkuu duniani si mahala salama leo hii utakwepa ajali ya mwendo kasi kesho utakufa na bodaboda
 
Labda tupiganie kwenye ubora, uzima Wa hayo magari na utimamu Wa madereva ila kwenye kusimamisha abiria ndio system yake hayo magari mkuu. Yametengenezwa kwa ajili ya abiria Wa kukaa na Wa kusimama
 
Back
Top Bottom