Mkuu nani apewe muda na nani anakumbushwa? maana mkuu wa mkoa huo kasema uchafu ni kosa la mwanamke, sasa sijui hivyo vituo vinatumiwa na wanawake tu au ndio kukosa shukrani kwa mama? any way watajua wenyewe fine enough hakuna mwanamke alieficha sukari( kuhifadhi ni kuficha now days) kwa hilo basi angetupongeza.Jamani wapeni muda wajipange vizuri, lakini ni vizuri kuwakumbusha
hapa wanatakiwa wachangamkie kila changamoto wanayoiona na kuipata la si hivyo mambo yataenda arijojo maana watanzania ni wazee wa fursa watapata mahali pa kuacha mafurushi yao ya taka...........na waweke adhabu kali ili watu waogofye kufanya ujinga kama kule kilimanjaro ukitupa taka kimaandazi inakula upande wako
ninamaanisha miradi kama hii ama mradi wowote hata kama mradi ni wa mtu binafsi , unapouanzishalazima kuwe na changamoto nyingi .. lazima kuwa makini mwanzo ili kuweza kujiendesha vizuri na ninamaanisha kila changamoto wanayokutana nayo waiangalie kwa ukaribu na waitatue kwa haraka zikilundikana changamoto litakuwa tatizo kubwa sana mfano hapa inaonekana kabisa hivi vifaa vya kuhifadhia taka ni vidogo katika kituo wabadilishe waweke vikubwa kutokana na wingi wa abiria ......................... na nnyingene zoote hapo kituoni kuna staff mwenzangu anaishi huko anasema mkata tiketi ni mmoja haiwezekani wakati abiria ni wengi mno na isitoshe anasema hana change ukae pembeni hizi zishughulikiwe mapema kwamba ziko ndani ya uwezo wao...............Ni sawa ulivyosema kila changamoto inayojitekeza ishughulikiwe haraka.Kwa maoni yangu utekelezaji wa mradi huo una mapungufu makubwa na ya hatari sana kwa watumiaji wa huduma hiyo.Kwanza najiuliza bwana afya wa jiji na watoa leseni waliwezaje kuwapa idhini Dart kutoa huduma kama hizo bila kuwepo vyoo vyenye kufanya kazi kwenye vituo vya mradi?Walielewa wazi kuwa vituo vitakuwa na wateja wengi vituoni watakaohitaji huduma hiyo wakati wote.Chukulia mfano wa wagonjwa wa kisukari na wenye umri mkubwa haja ndogo kwao ni ya mara kwa mara.Kuweka vyumba vya vyoo visivyofanya kazi ni ujinga ule ule.Niliona chupa za maji zimejazwa mikojo na kuwekwa ndani na milango ya vyoo hivyo na uchafu mwingi unaoweza kuleta maambukizi kwa abiria.Ningekuwa mkuu wa mkoa ningesimamisha mara moja Dart kuendelea kutoa huduma hiyo hadi vyoo vifanye kazi.Changa moto nyingine hatari ni askari wa kudhibiti vibaka kuibia abiria vituoni na ndani ya mabasi kwa wakorofi na waharibifu wa miundo mbinu makusudi.Msije kushtukia dreva amekwidwa shati na mkorofi au mnywa viroba na kusababisha ajali mbaya gari likiwa kwenye mwendo kwani yale magari hayana conductors na yanabeba watu wengi.La mwisho mashine za tiketi kutegemea umeme wa tanesco usio na uhakika.Wangenunua mashine zenye njia mbili umeme na solar na wakafunga solar panels vituoni kote kama m-badala.