Dark Girls - Mbona tunajidharau? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dark Girls - Mbona tunajidharau?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chapakazi, May 28, 2011.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Juzi nilianzisha thread ikiongelea hii ishu. Wengi wakasema ni uongo. Sasa sijui ni wao ndio wanajidanganya maana naona ni ishu iliyo serious sana.
  Unaweza kuipata hapa:
  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/136549-je-ni-kweli.html
  Leo nimekutana na hii trailer ya Documentary itakayotoka mwishoni mwa mwaka huu.
  Nimeangalia na kushikwa na huzuni sana.
  Kuna rafiki yangu wa karibu amepost kwenye facebook baada ya kuona hii documentary na kusema:
  "i remember my auntie sayin, make sure u marry a light skin lady, your too dark and you dont want your children to be dark like you"

  Je Waafrika tuna shida gani? Mbona tunajidharau?

  [video=vimeo;24155797]http://vimeo.com/24155797[/video]
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Yaani..............
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tumeoshwa akili kiasi kwamba hatufikirii kwa uwezo wetu bali kwa mwongozo wa watu wengine!!Ni aibu kweli mtu kujikataa na asili yako namna hii!!
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  nafuu umekuja. Maana kwenye ile thread ya wakati ule ulisema: "...Nwy sioni ukweli wowote maana wadada kibao nao wako na wazungu!!!"
  Sasa unaamini ni kweli?
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ishu sio kua na mzungu au kua na mtu mweupe bali ni kile kinachomsukuma mtu kumchagua huyo mweupe!!Wapo hao wenye hayo mawazo ya kupata mtoto mwenye ngozi mng¬Ďaro na wanaoolewa kwa sababu tofauti kabisa!!
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  80%ya waafrica hawajiamini,angalia kati ya mabinti utakaokutana nao utaona nyele zao sio za kiafrica lugha tunazotumia ni kigeni,kwa maelezo sikiliza wimbo Other side wa Lucky Dube!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  mimi kinachoniudhi most....
  unakuta una mpenzi wako mswahili...
  unajitahidi kumfanya ajisikie yeye ni queen fulani hivi....

  but wakitokeza wazungu au waarabu....
  unakuta mdada wa kiswahili anakuwa mnyonge mnyonge hivi...
  i hate that
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Of course ishu sio kuwa na mzungu. Nadhani hujanipata vizuri! Kwenye ile thread nyingine tulikuwa tunazungumzia kuhusu wasichana wa kiafrica kuchukia pale ambapo mwanaume wa kiafrika anapotoka na mzungu. Na hii ni kwa sababu ni ngumu kwao kupata wazungu. Nikaongeza kuwa hii ni zaidi kwa wasichana walio na very dark skin.
  Wewe ndio ukajibu kuwa hakuna ukweli na hiyo statement....
  Sasa nadhani tukubali kuwa kuna ukweli!
  Mimi nakubaliana na wewe kuwa tumeoshwa akili. Kuna kitu kinaitwa subliminal message. Ijapokuwa definition yake inaweza isiendana in total na ninavyoeleza hapa, lakini nadhani mtaelewa picha.
  Mara nyingi ukiangalia movies, wasichana wazuri ni weupe. Ukiona picha ya Yesu, ni mzungu. Ukiangalia cartoons hasa kwa watoto, superhero ni mzungu. Hii inajenga perception kichwani kwa mtu kuwa white = good. Ni mbaya kweli! Na natumaini tutaweza kubadilisha hii. Ndio maana napenda Actors kama Denzel Washington, Samuel L Jackson, maana wana break hiyo pattern. Lazima tuanze kujenga image ya Black is beautiful!
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  This is the reason why I don't even think of living in Ist world countries. Wazungu wame wa brainwash hawa ndugu zetu na kuwafanya waone kila kitu walichonacho ni cha hovyo. Nadhani ndio maana hata huko US blacks ni failures in life kwa kuwa wamekuwa bullied maisha yao yote. I love my country. Na si skin tu hata mambo mengine.

  Nilisoma kitabu cha gifted hands, nikawachukia sana wazungu. Yaani hata walimu wanawashauri wanafunzi wa asili ya kiafrika wazingatie sana masuala ya arts si masomo mengine kama science. Maanake black waishie kuwa wasanii tu.

  Nadhani ndio maana kina Jay Zee wamekuwa wanatembelea sana Africa kwani wame learn kuwa its here where they belong.

  Ni ngumu sana kuishi kwenye nchi ambako unaonekana second class human being. Na ukisikia wanawananga dark skin usidhani wale ambao ni dark tu hata nusu point wana hali mbaya zaidi. Kwani wao ndio hawa belong popote. Wakienda kwa weusi hawa fit wakienda kwa wazungu hawafit. Na hii ni mpaka kwenye US administration. Kuna ile kuandika your race. Sasa ukiwa half ni ngumu. Maana kuna African Americans (zamani negro) white etc kuna dada alituambia ofisini ilibidi awaulize migration officers yeye anafit wapi!
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Exactly...
  Kuna ndugu yangu anafanya kazi ofisi moja hapo dar. Karudi kutoka nje. Kuna mzungu hapo ofisini. Kazi yake haileweki, lakini kajifanya ni boss wa hapo. Watu wanamuogopa kweli. Unakuta hana hata qualification.
  A bit off topic lakini angalia hii video uone hawa waandishi wanavyouliza maswali kipumbavu! Yani niliangalia nikashikwa na hasira! Ishu ya Dowans kuna maswali makubwa kibao, yeye anauliza kuhusu capacity! Kutokujiamini ni mbaya mno!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  mimi sipendi wanawake wazungu
  but huwa nafikiria kuoa mzungu ili tu
  waswahili wanafiki wanafiki wanikalie mbali kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo ukija home (Tanzania) unakutana na ufisadi kwa kijinga. Kwa hiyo choice ni:
  1) kubaguliwa na kupambana na ubaguzi, lakini kuishi maisha mazuri; au
  2) kuibiwa na kunyanyaswa kila siku bila maendeleo yeyote, lakini kuishi home!

  Mimi nachagua numba moja kila wakati maana nina uhakika wa kuweza ku-break hii chain ya ubaguzi!
  Tatizo hatutengenezi watu wanaojiamini!
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160

  Hiyo statement ya wasichana wakiafrika wanachukia mwafrika akitoka na mzungu kwasababu ni ngumu wao kupata mzungu siwezi kuafikiana nayo hata nikiwa nimelala!
  Ila mengine uliyosema ni kweli kabisa...kwa wale ambao akili zao sio indepent wanaamini weupe na uzungu ndio bora!!Binafsi naamini mimi ni bora kwahiyo hata aje mtu wa bluu hatonitisha....kinachotakiwa ni watu waanze kujiamini...otherwise tutakua kawa wale wamarekani wanaobleach watoto wao wadogo !
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ushamba tu...sindo wale wale wanaoacha wapenzi wao kwaajili ya wazungu then wanaishia kutumiwa n kuachwa!!
   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  hivi kuna mtu anam-date mtu kwa ajili ya skin color? kuna rafiki yangu toka tuko sec anasema lazma aolewe na mzungu.kakutana na kimeo cha kikaburu,akaenda kuishi s.africa,walim-frustrate na ubaguzi hadi akaingia kwenye drugs.by the time nduguze wamemrudisha home,kesha-data kabisa! i am more than my skin color,i am more than what meets ur eyes banaa,period!
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  kwa jinsi wasichana wa kiswahili wengi walivyo na low self esteem na iferior complex na wazungu na waarabu...
  hata kama kuna mambo hayapendi kama kutoa tigo n.k
  akiwa na mzungu sheria zote zinavunjwa
  anakubali kila kitu

  too sad...
   
 17. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Speaking from my heart, I don't find whites (wazungu) attractive being men or women. Ngozi yao inachakaa upesi na ndio maana magonjwa kama skin kansa yanawapata sana
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Mtu akikusema vibaya jua anakuogopa,wazungu wanajua mtu mweusi ni bora ndo maana wanatusakama!
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Poa, nadhani juu ya hiyo statement tutapingana. Kwa hiyo tuiweke kando.
  Ivi umeshawahi kujiuliza mababu zetu walitawaliwaje? Ilikuwaje wakadanganywa mpaka wakatoa ardhi yao? Na wao pia walijiona inferiors?
   
 20. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sikuwa ninajua kama hii pia ni tatizo huko Marekani. Na kwa kweli nimeona jinsi wamarekani weusi walivyo..kumbe wale tunaoneshwa kwenye Music Videos ni 'wamechaguliwa'..yaani ni mbegu bora..

  Maswali ninayojiuliza

  1) Kwa nini wametufanya tuamini hivyo? Yaani imekuwaje sisi tumeshindwa kuwafanya waamini kama tunavyotaka?
  2) Je ni kweli mbaguzi mkubwa hapa duniani ni mtu mweusi mwenyewe??
  Yaani huyo binti mdogo kabisa, anajua mtoto mweupe ndo mzuri, na mtoto mbaya ni mweusi..

  3) Je hii inatufanya tuamini kwamba wenzetu wenye ngozi wana akili kuliko wenye ngozi nyeusi.? Kwa nini waliweza kututawala na kutufanya watumwa...? Kwa nini hadi leo tunaendelea kuwanyenyekea na kujidharau machoni pao.? Je hii ni uumbaji au tatizo gani hasa?

  Nafikiri haya mambo yanaweza kwenda ndani zaidi..
  Sijui sisi waafrika tuna matatizo gani

  1. Tunapigana wenyewe kwa wenyewe
  2. Hatuwezi kujitawala (Angalia mashirika yanapokufa pale ambapo wazungu waliondoka na kutuachia)

  Je kuna uhalali wowote wa kuwatupia lawama na kuwahukumu wazungu katika mustakabali wetu..ikiwa ustaarabu unatushinda?

  Angalia mazingira ya Temeke ambako 'wenyeji' ndo wamejaa..Tazama ujengaji wetu, mifereji, na hata vyoo na mabafu..?? Yaani tunaishi utafikiri tumeambia mwisho wa dunia ni kesho..
  TATIZO letu ni nini hasa??
   
Loading...