Dark days 17/03/20...

Mkuu asante kwa kudadavua, mimi naomba kuuliza,

1. Dini ya Judaism enzi hizo kabla kuvunjwa lile hekalu la pili na kuondoshwa kwao 70 AD, Kuhani Mkuu alikuwa akisimamia mambo mbalimbali kwenye dini hiyo kwa mjibu Wa Torati,

1. Je hivi sasa 2024 Kuhani Mkuu wanaye?

2. Miongoni mwa kazi za Kuhani Mkuu ni kufanya upatanisho wa taifa na Mungu mara moja kwa mwaka kwa kuingia pakatifu pa patakatifu kwa damu ya mnyama, je kwa kwa sasa wanafanyaje upatanisho na hawana patakatifu pa patakatifu?
 
Israel kwenye biblia walitabiriwa kwenda ulaya kama adhabu na watarudi sasa unavyosema wale sio wayahudi unatumia kigezo kipi

Wanasema wale ni wayahudi sababu dna zao zinafanana wenzako wanatumia dna wewe unatumia hisia
 
Waarabu ni watoto was japhet na wazungu ni watoto was Shem,weusi ni.watoto wa Ham!source Book of enoch!
 
Waarabu ni watoto was japhet na wazungu ni watoto was Shem,weusi ni.watoto wa Ham!source Book of enoch!
Vipi kuhusu wachina, wahindi, wajapani n.k??? Tumepewa akili na maarifa tutumie vizuri na siyo kuendeshwa na mihemko, papara na hisia za kidini!

Kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa jinsi dunia lilivyopiga hatua kubwa, hivi vitabu vya kidini vitapitwa na wakati muda siyo mrefu!

Walichobakiza ni kuunganisha matukio na nukta ili yafanane na wakati huu tulionao, ila itafika mwisho!
 
Hii thread ninachoipendea huwa ipo katika nyanja zote, kidini kihistoria kimedani kijasusi kiasiasa na kimaendeleo, tunampongeza mwanzisha mada na haswa wachangiaji ambao tupo hapa tokea siku ile uzi huu ulipo anzishwa.

Huu uzi utadumu na kudumu na utakuwa marejea na hata ushahidi hapo kesho, kesho sio mbali ipo siku ukweli utajidhirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…