Ajali ya Juzi Mbeya iliyohusisha bus kuwagonga wanafunzi waliokuwa wanakimbia barabarani imeondoa vijana wetu 6 na wengine majeruhi. Ajali hii imetokea alfajiri tarehe 26.07.2025
Ajali kama hii ilitokea Mtwara ilihusisha school Bus kuingia mtaroni na kusababisha wanafunzi 8 kufariki na mwalimu 1 na dereva 1 kufariki. Ajali hii ilitokea siku kama hiyo alfajiri ya tarehe 26.07.2022
Itakumbukwa pia wanafunzi wa Sabodo January 2014 wakati wanakimbia mchakamchaka asubuhi waligongwa na gari na kusababisha vifo vya wanafunzi 4 hukohuko Mtwara.
Hizi ni tarehe mbaya kwa historia za ajali Tanzania. Tuendelee kuchukua hatua za tahadhali hasa kufanya mazoezi kwenye kingo za barabara.