Darbrew (Chibuku) Yasitisha Uzalishaji

Darbrew (Chibuku) Yasitisha Uzalishaji

Huyu Mzungu nimemuelewa sana
Huyo mzungu yupo sahihi, unatengeneza vipi uchumi wa kati wakati unaua middle income earners na makodi yasiyo na kichwa wala miguu. Mfano, mfanyakazi anakatwa PAYE kila mwezi na wakati huo huo analipia VAT kwenye kila bidhaa na huduma anayotumia, hapo hapo kila siku anawindwa na trafiki atoe pesa ya kubrashia viatu. Eti tunatengeneza uchumi wa kati. PATHETIC
 
Kampuni ya kusindika pombe ya Kiasili Darbrew maarufu kama Chibuku iliyopo Ubungo imesitisha uzalishaji wa pombe hiyo tangu mwezi huu kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu na soko kudorora.

Darbrew ni kampuni inayomilikiwa na TBL 60% na halmashauri ya jiji 40%.

Tayari asilimia 80% ya wafanyakazi hao wameshapewa barua ya kuachishwa kazi na kupewa malipo yao.

Ikumbukwe kuwa Kampuni hii ni moja ya kampuni 10 zilizokuwa zinaongoza kwa ulipaji wa kodi mzuri nchini.

Rejea:
Dar Brew (Chibuku) yapunguza wafanyakazi 60 - JamiiForums

Zubaa uliwe: Chibuku inalipa kodi kubwa zaidi ya dhahabu na makampuni ya simu - tz yetu noma - JamiiForums
Tanzania ya viwanda inawezekana, na inaanza na wewe,
Uchumi wa Tanzania (wa kwenye makaratasi) unakua kwa kasi,
Vile vile CCM inazidi kukubalika kwa kuendelea kushinda majimbo na kata mbalimbali,

Tanzania bana, dah
 
Napita hapa daily pako kimy'aa. Kama kunamsiba vile aisee!
 
Kampuni ya kusindika pombe ya Kiasili Darbrew maarufu kama Chibuku iliyopo Ubungo imesitisha uzalishaji wa pombe hiyo tangu mwezi huu kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu na soko kudorora.

Darbrew ni kampuni inayomilikiwa na TBL 60% na halmashauri ya jiji 40%.

Tayari asilimia 80% ya wafanyakazi hao wameshapewa barua ya kuachishwa kazi na kupewa malipo yao.

Ikumbukwe kuwa Kampuni hii ni moja ya kampuni 10 zilizokuwa zinaongoza kwa ulipaji wa kodi mzuri nchini.

Rejea:
Dar Brew (Chibuku) yapunguza wafanyakazi 60 - JamiiForums

Zubaa uliwe: Chibuku inalipa kodi kubwa zaidi ya dhahabu na makampuni ya simu - tz yetu noma - JamiiForums
Matapu tapu ruksa kusitisha maana hata watumiaji wake ni kuduchu ila OG bear watu wangechonga sana humu
 
Hii pombe nlikuwa naisikia kwa mwalimu wangu wakati huo hivi alc yake ni % ngpi
 
Back
Top Bottom