Darasa la wanafunzi 278 lina dawati moja huko Mbozi Mbeya

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
NTUNGWA.jpg

Katika hali isiyo ya kawaida Wanafunzi 275 wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Itete wilayani Mbozi mkoani Songwe wanalazimika kukaa chini wakati wa masomo kutokana na uhaba wa madawati shuleni hapo.

Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Mkoloma, darasa la kwanza lenye wanafunzi 278 lina dawati moja pekee lililopelekwa shuleni hapo na mzazi wa mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka mtoto wake akae chini.

Uwepo wa dawati hilo moja unatoa fursa kwa mtoto wa mzazi huyo kuteua rafiki zake wengine wawili kukalia dawati hilo wakati wa masomo hivyo wanafunzi wengine 275 hulazimika kukaa chini.

Mwalimu Mkoloma amebainisha hayo kwenye mkutano wa wazazi na wadau wa elimu shuleni hapo uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuelimisha jamii juu ya dhana ya Sera ya Elimu bure pamoja na kujadili changamoto inayoikabili shule hiyo ikiwemo mlundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na uhaba wa madawati.

Amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 2000 wa kuanzia darasa la awali hadi la saba na wanafunzi wa darasa la kwanza pekee wapo 278 kati yao ni wanafunzi watatu tu ndio wanaokaa katika dawati moja lililotengenezwa na mmoja wa wazazi wa mtoto ambaye alifika shuleni hapo na kukuta mwanae anakaa chini wakati akisoma.

Mkuu huyo wa shule alisema kwa sasa uhitaji wa madawati shuleni hapo ni madawati 463 kwani kwa sasa shule ina madawati 248 ambayo yamegawanywa katika vyumba vya madarasa 11,hivyo kuiomba serikali na jamii kulitazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi haraka iwezekanavyo ili kunusuru watoto hao kutofanya vibaya kitaaluma.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Mussa Mlele alisema wao kama wazazi wamesikitishwa na hali hiyo hivyo kuwataka wazazi wenzake kuungana pamoja ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo la madawati shuleni hapo badala ya kungoja serikali akisema wanaoumia ni watoto wao wazo lililoungwa mkono na wananchi wenzake.
 
View attachment 327307

SITAACHA KUSEMA UKWELI MPAKA SIKU NIFE..HUYU WA SASA NI MNAFIKI..MPENDA SIFA NA MUIGIZAJI KULIKO WOTE WALIOTANGULIA..USHAURI WANGU AACHE TU KUPENDA MISIFA NA APUNGUZE UNAFIKI KWA WATANZANIA..NA ZILE TRILIONI ANAZODAI KILA SIKU KUWA KAZIKUSANYA MBONA HATUONI AKIZIFANYIA KAZI KAMA HII YA KUNUNUA MADAWATI...
 
View attachment 327307

Katika hali isiyo ya kawaida Wanafunzi 275 wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Itete wilayani Mbozi mkoani Songwe wanalazimika kukaa chini wakati wa masomo kutokana na uhaba wa madawati shuleni hapo.

Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Mkoloma, darasa la kwanza lenye wanafunzi 278 lina dawati moja pekee lililopelekwa shuleni hapo na mzazi wa mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka mtoto wake akae chini.

Uwepo wa dawati hilo moja unatoa fursa kwa mtoto wa mzazi huyo kuteua rafiki zake wengine wawili kukalia dawati hilo wakati wa masomo hivyo wanafunzi wengine 275 hulazimika kukaa chini.

Mwalimu Mkoloma amebainisha hayo kwenye mkutano wa wazazi na wadau wa elimu shuleni hapo uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuelimisha jamii juu ya dhana ya Sera ya Elimu bure pamoja na kujadili changamoto inayoikabili shule hiyo ikiwemo mlundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na uhaba wa madawati.

Amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 2000 wa kuanzia darasa la awali hadi la saba na wanafunzi wa darasa la kwanza pekee wapo 278 kati yao ni wanafunzi watatu tu ndio wanaokaa katika dawati moja lililotengenezwa na mmoja wa wazazi wa mtoto ambaye alifika shuleni hapo na kukuta mwanae anakaa chini wakati akisoma.

Mkuu huyo wa shule alisema kwa sasa uhitaji wa madawati shuleni hapo ni madawati 463 kwani kwa sasa shule ina madawati 248 ambayo yamegawanywa katika vyumba vya madarasa 11,hivyo kuiomba serikali na jamii kulitazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi haraka iwezekanavyo ili kunusuru watoto hao kutofanya vibaya kitaaluma.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Mussa Mlele alisema wao kama wazazi wamesikitishwa na hali hiyo hivyo kuwataka wazazi wenzake kuungana pamoja ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo la madawati shuleni hapo badala ya kungoja serikali akisema wanaoumia ni watoto wao wazo lililoungwa mkono na wananchi wenzake.

Hiyo ndiyo lasting impression na legacy ya Mkwere!
 
Mbeya mjikomboe, serikali ya ccm si ya kutegemewa kabisa! Pitisheni hata mchango kwa wanakiji pamoja na wafadhili mkishirikiana na viongozi wenu kama madiwaani na mbunge
 
mh Tanzania yetu hii sijui tutatoka lini na sasa ni elimu bure huyo mzazi aliyepeleka dawati nadhani atakuwa ameelewa vizuri kuhusu elimu bure
 
Mbeya mjikomboe, serikali ya ccm si ya kutegemewa kabisa! Pitisheni hata mchango kwa wanakiji pamoja na wafadhili mkishirikiana na viongozi wenu kama madiwaani na mbunge
mkuu hatupo tayari kuchangia coz tulishaambiwa bure tena bure kwelikweli...kila mwezi serikali inatangaza kwenye vyombo vya habari imekusanya matrioni ndo wakati wake sasa huu izipeleke huko shuleni kununua madawati
 
Acheni upuuzi. Ninyi mko kwenye miti tele. Mnataka tutozwe kodi Dar mletewe huko? Hebu Diwani wenu na mbunge wawajibike acheni kutusumbua na domestic issues zenu.
 
Simpatii picha huyo dogo mwenye dawati jinsi anavyoheshimiwa na wenzake.

Hii Tabia ya kukurupuka na porojo za kuwahadaa wananchi ili uonekane wa maana itaendelea kuwadhalilisha ccm kila siku.
 
mkuu hatupo tayari kuchangia coz tulishaambiwa bure tena bure kwelikweli...kila mwezi serikali inatangaza kwenye vyombo vya habari imekusanya matrioni ndo wakati wake sasa huu izipeleke huko shuleni kununua madawati
Wazo lako ni zuri sana! Hakuna haja ya kuchangia maendeleo ya watoto wenu. Hapo anayeumia ni nani?
 
igeni wachaga,sio kila kitu kufanyia had kujengewa vyoo.nashindwa nini kujichanga? mwisho mtataka mletewe had nguo za shule
 
mkuu kwani ni kazi ya mbunge kununua hayo madawati...tunachotaka makufuli apeleke yale matrioni yake anayotangaza kila Siku wameyakusanya ili wakanunue madawati
Kwani mbunge ana kazi gani? Mbona kama una hasira na bwana magu? Na mwisho wa siku wanaoumia ni watoto wetu, so hatumkomoi magufuli.
 
mkuu hatupo tayari kuchangia coz tulishaambiwa bure tena bure kwelikweli...kila mwezi serikali inatangaza kwenye vyombo vya habari imekusanya matrioni ndo wakati wake sasa huu izipeleke huko shuleni kununua madawati
mkuu kuitegemea serikali hii ni shida na pia itawaathiri watoto na wakazi wa mbeya! Fanyeni mnachoweza kufanya ikibidi tafuteni wafadhili nyie wenyewe watoto wenu wasome kwa kujisikia
 
Kwani mbunge ana kazi gani? Mbona kama una hasira na bwana magu? Na mwisho wa siku wanaoumia ni watoto wetu, so hatumkomoi magufuli.
Mbunge ni mwakilishi wa wananchi bungeni. Hiyo kazi ya kununua madawati vitabu nk ni ya serekali sio Mbunge. Huyo jamaa huko sahihi kabisa hapo wa kulaumiwa ni magu na serekali yake
 
Anawawakilisha katika nini? Na serikali ni nani?
 
halmashauri si huwa kuna mafundi? na misitu ya serikali si ipo? tunashindwa nini kutengeneza madawati!! Ndalichako si nakuuliza? hii ni tatizo lako, ongea na wenzako msolve.
 
Back
Top Bottom