Hivi kwa nini kazi za maendeleo zisifanywe kwa dedication. Kila mwaka raisi afanye emphsis katika jambo moja. Kama:
1.Mwaka wa kwanza labda uwe wa kutekeleza ujenzi wabarabara na madaraja nchi nzima hivyo 80% ya fungu la budget liende huko ili mambo yote yawe yanamalizika kwa wakati.
2.Mwaka wa pili uwe wa kuboresha elimu tu ikiwa ni kutengeneza mazingira bora ya elimu nchi nzima kwa kuweka vitendea kazi km madawati,vitabu,kujenga vizuri shule pamoja na nyumba za walimu labda na kuzingatia vizuri maslahi ya walimu kwa 80% ya budget.
3.Mwaka wa tatu uwe wa kuboresha viwanda, na kusimamia maswala ya nishati ya umeme ili uwe ya uhakika zaidi ili kuondosha kabisa adha ya kukatika kwa umeme kunakosababisha watu washindwe kufanya kazi zao kwa uhakika.Kupitia mikataba yote mibovu na kuiweka sawa ili tuweze kunufaika na rasilimali za nchi yetu.
Yote ya yote vitu vifanyike katika utaratibu sahihi.
Hivi haya yanashindikana kweli wana jf wenzangu?