Darasa Huru: Ufundi Laptop (Beginners To Advanced)

Asante kwa uzi mzuri mkuu,
Pia samahani mkuu, unaweza kuelezea japo kwa kifupi
Hapo kwenye "virtual technology".
Kwa Lugha Rahisi Hii Ni Teknolojia Ambayo Laptop Yako Kufanya Kazi Vizur Kwa Baadhi Ya Apps Especially Games Na Emulator.

Inshort Kuna Apps Ili Zirun Inabidi Kuwe Na True Underlying Layer Kati Ya Hardware Na Software, Kazi Kubwa Yake, Ni Kufanya Emulation Ya Hardware. (Kuongeza Umilki Na Nguvu Yake Kwenye Kupewa Priority Katika Hardware)
 
Kwa Lugha Rahisi Hii Ni Teknolojia Ambayo Laptop Yako Kufanya Kazi Vizur Kwa Baadhi Ya Apps Especially Games Na Emulator.

Inshort Kuna Apps Ili Zirun Inabidi Kuwe Na True Underlying Layer Kati Ya Hardware Na Software, Kazi Kubwa Yake, Ni Kufanya Emulation Ya Hardware.
Nashukuru Sana mkuu,

Wacha niende kutia tiki kile kibox.
 
Nashukuru Sana mkuu,

Wacha niende kutia tiki kile kibox.
Don't do it Kama hujui virtualization vizuri, mtoa mada kakujibu vizuri sana na nakubaliana na majibu yake.
Lakin level ya application yake ni Zaid ya hayo maelezo. Na kwa baadhi ya bios ukienable hiyo virtualization option utashindwa kuboot kutoka kwenye os yako unayotumia muda huo mpaka utakapoweka OS nyngne ambayo itatumia hiyo option unayotiki Kama ni bare matel.


So far Asante mtoa mada umefanya wengine turud darasan
 
Mkuu hivi pc ambayo ipo connected kwenye local area network na iko restricted ku install program yeyote yaani unapo install program inadai administrator password.
Hicho kikwazo nakirukaje?
Hiyo password haiko kwenye hiyo PC unayotumia. Hiyo password iko kwenye server inayocontrol hiyo Local area network.
Kuweza kujua inawekwaje inabid ujue Mambo ya DNS na Active directory on Windows server.
Na hapo admin wa hiyo server huwa anatengeneza policy kwa watumiaji wote wa hiyo LAN.
Miongon mwa policy Kuna kuwa na nan anaweza fanya nn na kwa wakat gani.

Mfano hiyo program admin anaweza akaweka kwenye computer ya rafik yako na we ukaweza kuitumia Kama imewekwa kwako tu.
Kinachofanyika hapo ni kutengenezewa profiles zenu kenye Active directory.

Sidhani Kama Kuna haja ya kuendelea kuhangaika na hiyo password
 
Don't do it Kama hujui virtualization vizuri, mtoa mada kakujibu vizuri sana na nakubaliana na majibu yake.
Lakin level ya application yake ni Zaid ya hayo maelezo. Na kwa baadhi ya bios ukienable hiyo virtualization option utashindwa kuboot kutoka kwenye os yako unayotumia muda huo mpaka utakapoweka OS nyngne ambayo itatumia hiyo option unayotiki Kama ni bare matel.


So far Asante mtoa mada umefanya wengine turud darasan
Asante Sana mkuu,
 
Hii PC nilikuwa naitumia ofisini, kuna kipindi nilitoka kikazi, nikamuachia aliyekuwa anafanya kazi na mimi.

PC watu wa IT waliweka Administration password, na hii mimi niliongea na mtu wa IT baada ya kuambiwa jamaa anaitumia Laptop vibaya.

Huko nilikoenda nimeshindwa kurejea pale ofisini na Laptop yangu nimeenda kuichukua. Shida ipo hapa, siwezi kuinstall chochote pasipo hii password kuwepo, siwezi kumake baadh changes pasipo hiyo password na naogopa kupiga windows sababu sifanya partition na nna vitu vingi mno vya msingi.
Tafuta program inaitwa konboot, fata maelezo yake vizuri na pia tafuta latest version.
Hi kitu inaondoa password ya version yyt ya windows.....

Na unatumia kwenye flash au CD.


Kama computer yako inatumia version ya windows 7 au Vista au xp download ile inaitwa Hiren boot. Ndani ya Hiren boot Kuna konboot. Na utaitumia kirahisi zaidi.
Ila Kama unatumia kuanzia windows 8, 8.1 au 10, download konboot peke ake.
100% your work will be done.
Uwe tu makin namna ya kuitumia
 
Don't do it Kama hujui virtualization vizuri, mtoa mada kakujibu vizuri sana na nakubaliana na majibu yake.
Lakin level ya application yake ni Zaid ya hayo maelezo. Na kwa baadhi ya bios ukienable hiyo virtualization option utashindwa kuboot kutoka kwenye os yako unayotumia muda huo mpaka utakapoweka OS nyngne ambayo itatumia hiyo option unayotiki Kama ni bare matel.


So far Asante mtoa mada umefanya wengine turud darasan
Uko Sahihi Mkuu
 
Niwakumbushe tu wadau....
Usije kutamani kuweka password kwenye BIOS kirahisi rahisi then ikatokea umesahau ukadhani pia kuiondoa itakuwa kazi rahisi.

Si ajabu option zote zikashindwa kuondoa hiyo password ya bios na ukawapa watoto wachezee tu hiyo PC.

Technology imebadilika sana na version za BIOS ziko tofaut sana hata Kama manufacturer wa hiyo PC atakuwa ni huyo huyo. Computer ya Dell ya mwaka 2005 inaweza kutoa BIOS kwa kushortisha jumper lakin computer ya Dell 2015 isitoe BIOS password kwa njia hiyo au nyngne yyt ulowah kuisikia.

Chukua tahadhari.
 
Ok Boss Hio Sio Bios Admin Pasaword

Ni Password Ya Windows, Sasa Naomba Kujua Free Disk Space Kwenye Hdd Yako.

Kama Inawezekana Unaweza Kufanya Partition Kuikata Ukapata Partition Mpya Kubwa Ukahamisha Vitu Vya Msingi Then Una Install Windows Upya! Hapa Tunatumia Easeus Partition Master!

Au Unaweza Kutoa Ku Reset Kwa PCUnlocker, Ita Reset Admin Password Ya W8ndows Bila Shida.

Software Zote Hizi Crack Zinapatikana Torrent Na Ukubwa ani 100MB Kwa 75MB

Naomba Kujua Free Space Kwenye Hard Disk Yako????????

Karibu
Mkuu mimi naomba unisaidie pia procedure za kufanya Partition kwenye HDD.

Shukran.
 
TUIFAHAMU BIOS MENU NA UMUHIMU WAKE KWA SOFTWARE REPAIR

(PART 1 EP01)


View attachment 1244323

Habari Wanandugu.

Ni Ijumaa ya kwanza leo ya somo letu la laptop repair, na katika part 2 hii tutaangalia SOFTWARE Issues Tu.
Tujue Kidogo Nini Maana Ya Software Kwenye Laptop Au Computer Yoyote

Software Kwa Lugha Rahisi Ni Part Ya Computer Ambayo Huwezi Kuishika Na Mkono, Virtual Unakiona Lakini Huwezi Kukishika, Kama Vile Application, Themes, Cursor Etc
Software Ndio Inakupa Wewe Hali ya kuzungumza na computer, Kwa lugha nyingine ni USER INTERFACE.
Kwenye laptop repair practically, Software Inajumlisha, ALL Computer Apps, Operating System, BIOS, Etc.

Kwa Leo Tuangalie BIOS MENU Ambao Ni Msingi Mkubwa Wa Software Repair Na Kwa IT Professional Yoyote Hapa ndipo pa kuanzia kwenye software repair.

BIOS ni nini?
BIOS ni program iliyo na mahusiano mojamoja na laptop au computer yoyote kwa sababu ina chip iliyopo ndani ya motherboard, chip hiyo ndiyo inafanya kazi ya kuunganisha vifaa vyote vilivyopo ndani ya computer kufanya kazi kwa usahihi, kwa lugha sahihi huu ndiyo moyo wa software kwenye computer, hii ndio mwalimu mkuu wa software zote ikiwemo Operating System, Ukibonyeza Button ya kuwasha laptop anayeguswa na kutoa ruhusa ni bios na yeye ndio anaielekeza computer, Utachukua Software Wapi Either Kwenye HDD, USB Drive Au CD ROM,Etc.

BIOS Menu Ni Nini?
Ni Mpangilio Wa BIOS Katika Laptop Unaompa Ruhusa Mtumiaji Kufanya Chaguzi Mbali Mbali Kabla Ya Kufikia Katika Operating System.

Kipi Naweza Kukifanya Kwenye BIOS Menu?
  • Unaweza Kuiwekea Password Laptop Yako (Hii ni safe Zaidi kuliko ya windows)
  • Unaweza Kuangalia Taarifa Za Laptop Yako (System Info)
  • Unaweza kuiamrisha laptop yako ifuate windows kutoka kwenye Nini Mfano: HDD, USB Drive Au CD ROM
  • Unaweza Kufunga Matumizi ya Kifaa Kimoja Au Vingi Kwenye Laptop Yako, mfano: Port za USB, Speaker, Touchpad, WLAN Etc
  • Unaweza Kupunguza Nguvu za matumizi ya Laptop yako kwa kutumia menu ya Multiprocessing na Virtual Technology
  • Unaweza Kuangalia Life time na Status ya battery lako
  • Kubadili saa na kujua OS Ya Kwanza Kuwekwa Kwenye Laptop Yako.
  • Etc

NITAIPATAJE BIOS MENU?
Laptop zote zina bios menu tofauti, zinafanana baadhi kwa brand name mfano: DELL Nyingi Bios Ni F2 Na HP nyingi Bios Ni F9.
List Ya Bios Ipo Hapa Chini:

View attachment 1244326

  • Zima laptop yako
  • Bonyeza Key Kama Zinavyoonekana Hapo Juu (Hutegemea na BRAND YAKO)
  • Bonyeza kwa kuachia achia kama unaipiga ipiga mara nyingi maana mara nyingin hapa tunaotea
  • Unabonyeza pale laptop inapowaka na kuonyesha brand name (kuwa makini sio zote zinaonyesha brand name nyingine zinakuwa kwenye FAST BOOT)
  • Kama itagoma jaribu kwa kubonyeza huku ukiwa umeishikilia Function Key (Fn).

VILIVYOPO KWENYE BIOS MENU NA MATUMIZI YAKE

Hapa hutegemea na Bios Yenyewe Hapo Chini Nimetumia mfano wa Phoenix But Inaweza kuwa WARD Etc So Usikariri ila vingi vinafanana.

Tutumie mfano hapo chini.

View attachment 1244331

MAIN = Hapo utaakuta sifa za laptop yako au STEM INFORMATION
Utajua Size ya RAM, HDD, Processor Na Serial Number Ya Laptop
Sio muhimu sana kwa repair technician

ADVANCED = Hapa ni muhimu kwa technician kwa maana hapa utapata Option ya Kuzima Ports, Au WLAN au Fn Key Au Speaker, Na Touchpad Hapa Utapata Menu ya Kupunguza Nguvu Ya Pc Na Processor, Na Kwa Gamers Amba Ndio Kuna Virtual Technology, Pia Hpa ndio kuna SATA MODE Ya HDD Ukibadili Hii Windows Hauwez Run Kwa Mode Tofauti na uliyoweka wakat unafanya installation.

SECURITY = Hapa utapata menu ya kufunga Password Za Laptop Yako (BIOS PASSWORD, HDD PASSWORD, ADMIN PASSWORD).

BOOT: Hapa utapata menu ya kuiamrisha laptop wapi ikachukue windows wakat inawaka, hapa ni muhimu sana wakati unataka kufanya installation ya windows kwa kutumia external device kama USB FLASH, UEFI MODE NA LEGACY MODE Zinapatikana hapa.

MATATIZO YA BIOS NA UTATUZI WAKE
Kuna matatizo mengi ya laptop lakini yafuatayo ni common na nimekumbana nayo sana.

1. BIOS PASSWORD
Hili ni tatizo sana na huwa nacharge pesa nzuri kulitatua, hii ni ile password tuliyoiona pale juu ambayo inatokea kabla booting haijafanyika.
Ukiwasha PC Utaona Hivi
View attachment 1244332

JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI
Kuna njia nyingi za kutatua BIOS Hutegemea Brand na Model Ya Laptop na Skills Alizo nazo Technician
  • Kutumia Backdoor Password: hii ni common password ambazo zipo tayari kwenye bios kutoka kwa manufacture lengo la hizi ni kutumika wakat wa Emergency Ku Reset, Ili Kupata Hizi Password, Washa PC Nenda Kwenye BIOS Password Ingiza Randomly Psssword Zozote Mara 3, Then laptop itakuandikia SYSTEM DISABLE, Na itakupa namba Tano Copy Hizo Namba,Then Tafuta laptop nyingine nzima Nenda Kwenye Hii Site BIOS Master Password Generator for Laptops. Andika Disable code zako then Utapewa List ya Password Za Kujaribu Kufanya Reset.

  • Toa CMOS Battery.
  • Kama unaweza kufungua na kutoa CMOS Battery basi unaweza kufanya hivyo, Then ukawasha pc Unaweza Ukaitoa.
View attachment 1244337

  • CMOS Discharge.
  • Hii ni advanced kwa tech yoyote anatakiwa kuifanya lakini ni lazima kuwa makini kwa maana ukishindwa kujua PIN Out za CMOS unaweza kuiharibu motherboard, Hii Inafanywa kwa kutoa CMOS Battery na kutafuta CMOS Pin Out Kweny Board na kupigisha Short. Means Unawasha laptop then unagusanisha hizo pin kwa kutumia Tweezer, The PC Itajizima, Ukiwasha Itakuwa haina Tena Password, Mchezo Huu Tunaufanya Sana Kwa Toshiba Na ACER, Kumbuka Kila motherboard ina PIN OUT Zake, So Kuangalia Schematica Au Ku Google Hakuepukiki.
  • Mfano wa PIN OUT Huo hapo Chini:
View attachment 1244338

c) Kufanya Short Kwenye SCL na SDA Chip.

SCL na SDA chip inabid uzifanyie location kwa kutumia Schematic, Pia Utafanya Kama kwenye CMOS Discharge Hapa Utaangalia PIN out,

Mfano Hapo Chini.
View attachment 1244341

2. TOUCHPAD HAIFANYI KAZI, USB PORT HAZISOMI AU WLAN HAIFANYI KAZI.

Hili na nalo ni tatizo haswaa kwa laptop za TOSHIBA, Ukifanya Kutoa Tu CMOS Batterry Automatic CMOS Inafanya Reset, Mwisho wa siku inazima ToucHpad kwenye BIOS Menu.
USB Mode Pia Huwa Unazimwa 3.0, Mwisho wa siku Port Inakuwaga Umeme (5V) Lakini USB Device Haisomi Kabisa, Au WLAN.

SULUHISHO
Nenda Kwa BIOS Menu Upande Wa Advanced Then Angalia Kama Imezimwa Washa Na Epuka Kuchomoa CMOS Battery Mara Kwa Mara.

3. USB DEVICE HAIONEKANI WAKATI WA KUINSTALL WINDOWS KWA USB

Hii pia hutokea sana, haswaa kwa hizi laptop mpya, haijawahi kufanyiwa installation ya windows .
SULUHISHO
Nenda kwa Boot Menu Angalia Kama USB Boot Device Ipo Selected Au La, Then Iweke Iwe Your First Priority, Ukiwa unayafanya haya USB Flash Drive Yenye Windows Lazima Iwepo.

NB: Notice Za Session Hii Zipo Chini Hapo Kwa PDF.


MATATIZO YAPO MENGI, KAMA KUNA YOYOTE MWENYE NAYO AFANYE NYONGEZA HAPO NA KARIBUNI KWA DISCUSSION.

KUMBUKA KILA WAKATI, UKIWA UNAJIFUNZA LAPTOP REPAIR MWALIMU WAKO MKUU NI INTERNET


Tukutane Next Week Kwa Part 2 E02 Kama Mungu Akipenda.

Wasalaam.

Mtwara Smart.
Asante kwa nondo.
 
Ukiwa Unafanya Installation Ya Windows Au Baada??
Ukiwa unafanya new installation ya window yaani kwa mara ya kwnz, huwa napata shida pale kwny kugawa sizes za Drive C na Drive D

Assume nataka niwe na drive 2 tu au tayari zipo mbili nataka kuongeza ya tatu.
 
Tafuta program inaitwa konboot, fata maelezo yake vizuri na pia tafuta latest version.
Hi kitu inaondoa password ya version yyt ya windows.....

Na unatumia kwenye flash au CD.


Kama computer yako inatumia version ya windows 7 au Vista au xp download ile inaitwa Hiren boot. Ndani ya Hiren boot Kuna konboot. Na utaitumia kirahisi zaidi.
Ila Kama unatumia kuanzia windows 8, 8.1 au 10, download konboot peke ake.
100% your work will be done.
Uwe tu makin namna ya kuitumia
Ina free space ya 200GB, kwani mkuu hamna namna ya kuiondoa mpka kupiga windows?
 
Kwenye konboot pia Kuna feature inaitwa passwordless login. Ukichgua hiyo feature utaweza kuingia kwenye computer yenye password bila kutumia password yyt.
Ila ukizima na kuwasha tena ndio itadai. Unatumia hyo feature km hutak kubadili password
 
Back
Top Bottom