Daraja la Magufuli kuwa la 6 kwa urefu barani Afrika

Bikirajohola

JF-Expert Member
Jun 11, 2022
356
632
Daraja la JP Magufuli linalojengwa Mkoa wa Mwanza, limetajwa kuwa refu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati huku likishika nafasi ya sita kwa bara la Afrika.

Daraja hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 48.9, linatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 3.2 na linagharimu Sh716.3 bilioni zilizotolewa na Serikali kwa asilimia 100.

Akizungumza leo Alhamisi, Julai 21, 2022 wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, Joseph Haule amesema Daraja la 6th October lililopo nchini Misri lenye urefu wa kilomita 20.5 ndilo linaloongoza katika orodha hiyo.

“Kama mnavyoona Tanzania sasa tunazidi kupaa, tumeona madaraja mengine mengi makubwa na mazuri yakichukua rekodi lakini sasa daraja hili ndilo litakalovunja rekodi nchini, Afrika Mashariki na Kati,” amesema.

Madaraja mengine marefu Afrika, amesema ni Third Mainland la Nigeria (kilomita 11.8), Suez Canal la Misri (kilomita 3.9), Kisiwa cha Msumbiji (kilomita 3.8), na Dona Ana la Msumbiji (kilomita 3.67).

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2024, licha ya changamoto zinazokabili utekelezwaji wake ikiwemo janga la Uviko 19, maji kuongezeka, na uwepo wa miamba chini ya maji.

Mhandishi Mshauri wa mradi huo kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Corporation, Abdulkarim Majuto amesema hadi sasa nguzo 22 kati ya 67 zimeshainuliwa na baadaye itamwagwa.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Paschal Ambrose amefafanua kuwa tayari mkandarasi amelipwa Sh223 bilioni, huku Mhandisi Mshauri akilipwa Sh3.29 bilioni, wakati Sh3.1 bilioni zimelipwa kama fidia kwa wananchi 165 waliopisha mradi.

Msongamano wa watu kusubiri vivuko na hivyo kuchelewa kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali ni miongoni mwa changamoto zitakazokabiliwa iwapo mradi huo utakamilika kwa mujibu wa Lameck Masunga mkazi wa Busisi mkoani humo.
 
Kwanza hili daraja lingeitwa Mama SSH Bridge kwa heshima yake kwa mambo mafupi aliyoyafanya Mama SSH hapa nchini. Mama legacy yake ni njema na kubwa sana tofauti na mwenzake ambaye ameacha legacy ya hovyo na aibu sana kwa vizazi vyetu.
 
Idea ya ujenzi nadhani ametoa Magufuli, Samia hayo Mambo hayajui,Jiwe kaacha mazuri mengi mfano SGR na haya madaraja

Serikali yake watu walitekwa na kupotea lakini isiwafanye msione kazi aliyofanya
 
Hakuna hata kapicha cha kusindikizia uzi?

Weka picha
32563472877_c718bedc95_z.jpg
IMG_20220509_100340.jpg
i7a8e481c28d1b9e7180c51c56cb23d2.jpg
 
Daraja la JP Magufuli linalojengwa Mkoa wa Mwanza, limetajwa kuwa refu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati huku likishika nafasi ya sita kwa bara la Afrika.

Daraja hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 48.9, linatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 3.2 na linagharimu Sh716.3 bilioni zilizotolewa na Serikali kwa asilimia 100.

Akizungumza leo Alhamisi, Julai 21, 2022 wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, Joseph Haule amesema Daraja la 6th October lililopo nchini Misri lenye urefu wa kilomita 20.5 ndilo linaloongoza katika orodha hiyo.

“Kama mnavyoona Tanzania sasa tunazidi kupaa, tumeona madaraja mengine mengi makubwa na mazuri yakichukua rekodi lakini sasa daraja hili ndilo litakalovunja rekodi nchini, Afrika Mashariki na Kati,” amesema.

Madaraja mengine marefu Afrika, amesema ni Third Mainland la Nigeria (kilomita 11.8), Suez Canal la Misri (kilomita 3.9), Kisiwa cha Msumbiji (kilomita 3.8), na Dona Ana la Msumbiji (kilomita 3.67).

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2024, licha ya changamoto zinazokabili utekelezwaji wake ikiwemo janga la Uviko 19, maji kuongezeka, na uwepo wa miamba chini ya maji.

Mhandishi Mshauri wa mradi huo kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Corporation, Abdulkarim Majuto amesema hadi sasa nguzo 22 kati ya 67 zimeshainuliwa na baadaye itamwagwa.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Paschal Ambrose amefafanua kuwa tayari mkandarasi amelipwa Sh223 bilioni, huku Mhandisi Mshauri akilipwa Sh3.29 bilioni, wakati Sh3.1 bilioni zimelipwa kama fidia kwa wananchi 165 waliopisha mradi.

Msongamano wa watu kusubiri vivuko na hivyo kuchelewa kwenda kwenye shughuli zao mbalimbali ni miongoni mwa changamoto zitakazokabiliwa iwapo mradi huo utakamilika kwa mujibu wa Lameck Masunga mkazi wa Busisi mkoani humo.
Hata lingekuwa la kwanza still haliwezi kuniletea unga nyumbani kwangu
 
Back
Top Bottom