BABU CHONDO
JF-Expert Member
- Jun 6, 2011
- 855
- 139
Kuna lori lililokuwa limebeba kontena limejaribu kupita daraja linalounganisha UKONGA {BANANA)- SEGEREA- KINYEREZI NA MBEZI limeharibika kabisa kwa kutumbukia na lori , kwa sasa foleni ni kubwa magari yote yanarudi, kwa wanaotoka mjini ni vyema kutumia njia ya VINGUNGUTI kwenda KINYEREZI, SEGEREA NA MBEZI,
Daraja limearibika sana.
NI VYEMA SHERIA IKACHUKUA MKONDO WAKE, haiingi akili mjinga mmoja kukata mawasilino wa watu wote kwenye njia muhimu kama hii.
Mfumo wa kudhibiti malori ya mizigo ni dhaifu sana nchini, madereva wangepewa route za kupita pale wanapotoa mizigo bandari na wanapoingiza mizigo hapa mjini kutoka mikoani,
Bila shaka jamaa wametumia mwanya wa polisi/trafic kutofanya kazi usiku kufanya huu utumbo, hivi kwa nini usiku kwa mji mkubwa kama Dar jeshi la polisi linalala mapema HIVYO?
pinda anatakiwa kuwajibika ndo aliruhusu wanaozidisha uzito kuendelea kuharibu barabara zetuMagufuli si alikuwa anadhibiti uzito/dimension za malori akaonekana kama mwanga? Sasa hivyo vibarabara vyote vinakwisha na fedha hakuna....ukizingatia mapato yanategemea vyanzo vilevile vya bidhaa haramu na pia halafu hazitoshi
Hapo kuna kibao kinachoonyesha gari mwisho tani kumi. Sasa sijui dereva alivaa miwani ya mbao? Na je wanasheria wa hapa jamvini hebu watuambie mwenye gari anaweza kuhusikaje na kesi kama hii ya uzembe wa dereva?
Waanguke tu sasa maana tumechoka
Mkuu hata mimi nimepita hapo jana asubuhi nikaona kibao kikionyesha mwisho Tani 10. Ni heri malori ya njia kuu kwasababu yanapimwa na ukizidisha uzito faini ama unaingia mfukoni kutoa rushwa lakini ni tofauti na Mijini ambako Milori inavunja sheria wazi wazi bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Na tatizo hili haliwezi kuisha kwa kuwatumia Matrafiki. Ni lazima Mamlaka za Miji/Jiji yaunde Vitengo ama ziingie Mkata na Makampuni kama Majembe kupambana na hawa wavunja sheria.
haya madaraja ya limits lakini madereva wetu shida sana, mwenye lorry anatakiwa afidie hasara kwa kweli
Faida ya kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu. Mizengwe Punda lazima awajibike.
Huu ni ujinga tena wa hali ya juu unajua kabisa gari mwisho kupita tani 10!hao jamaa walipe hilo daraja
Msikimbilie kumlaumu mwenye lori, kwani mkandarasi alipewa atengeneze la kubeba uzito gani?
Msikimbilie kumlaumu mwenye lori, kwani mkandarasi alipewa atengeneze la kubeba uzito gani?
Dereva atakuwa na akili ya pig. Utapitaje daraja lile na mzigo.mkubwa? ila pia sijajua kama mamlaka husika ziliweka kibao pale kutahadharisha kuhusu magari ya tani kubwa.
Sio madereva tu, tatizo wajenzi hawaweki mipaka ya UZITO wa magari yanayotakiwa kupita ktk madaraja au barabara zinapokamilika!