Daraja la Kigamboni ni White Elephant Project, Hatulihitaji!

Mkuu hatahivyo mawazo yako yanaweza kua sehemu ya utekelezaji wa kauli mbiu ya "pigeni mbizi"
 
Mkuu mwarobaini wa haya yote ni flying over, tutaruka sarakasi zote huku tukiwa kwenye vazi la kanzu na msuli pasipo kufanikiwa. Huko kenya mpaka leo bado wanazidi kuongeza flying over huku sisi huku sisi tiking'aa sharubu na upanuzi wa barabara wakati junction ni ileile moja ya mnara wa askari..!!
 
Hoja hii ni ngumu kupata mashiko kwani ni yakufikrika zaidi. Haina chembe za takwimu kuipa mwelekeo wa kutatua tatizo la usafiri kijiji Dar. Kujenga DART Mwenge-kivukoni ni kuongeza msongamano kwenye Kivuko cha Magogoni ambako abiria wote huduma kwenda Kigamboni. Kuwa na daraja la Kigamhoni itakunguza msongamano kwenye Kigula. Ujenzi wa daraja la Salender-Coco Beach ni kupunguza msongamano kwenye daraja la Salender ambalo ndio kiungo kikuu kwa watu kutoka kaskazini ya jiji kuingia City Centre ambako shughuli nyingi za kiserikali na kibiashara hufanyika. Kwa hiyo miradi hii miwili ni muhimu kuboresha usafiri na kupunguza muda unaopotea barabarani. Matokeo chanya ni kuboresha shughuli za kijamii na kiuchumi katika jiji la Dar es Salaam. Kwa hiyo ujenzi wa DART: Mandela-Buguruni-Kariakoo na Mwenge-Kivukoni ufanyike bila kuadhiri miradi ya yale madaraja mawili. Bahati Darajani la Kigamboni litafunguliwa mwezi Machi 2016.
 
Kupinga Daraja la Kigamboni kunatokana na mtu kutofahamu tabu na adha ya foleni wakati wa kusubiri kivuko, muda unaotumika ni mrefu na hiyo huwa kwa mtu anaetoka mjini kwenda Kigamboni na vice versa. Kigamboni kuna mahoteli, airstrips na recreation sites ambazo zinavutia wageni na wenyeji lakini ambao wanakatishwa tamaa kuzifikia kutokana na usumbufu wakati wa kuvuka.
Wakazi wengi wa Dar es salaam wanamiliki maeneo wanayoshindwa kuyaendeleza kutokana na ugumu wa kuyafikia na wengine wanashindwa kuanzisha makazi katika maeneo wanayomiliki kwa kuwa shughuli zao ziko center na kufika huko kwa wakati kunakwamishwa na foleni ya kupanda kivuko.
Kigamboni ni wilaya mpya ambayo inatarajiwa kuwa jiji jipya la kisasa, shughuli zote za kuliendeleza na kulikuza jiji na kufikia viwango vinavyotarajiwa, itahitaji mfumo mwanana wa usafirishaji wa vifaa na watu watakaoshiriki katika mchakato mzima wa kulijenga jiji hilo na daraja ni suluhisho muafaka wa kuyafanya yote hayo yawe rahisi.
Ukiachana na mradi wa mji mpya, tayari Kigamboni kuna miradi mingi mikubwa ya makazi mapya ya kisasa ambayo yanatarajiwa kuaccommodate maelfu ya wazalendo na wageni. Mifano mizuri ni: Dege eco Village, Avic Town, Mradi wa Nssf Mwongozo, Mradi wa Nssf Kibada, Mradi wa Nssf Tuangoma na midogo ya makazi Mwasonga ambayo iko katika maeneo matatu katika kijiji hicho.
Hivi kweli bado Daraja lisiwe na maana? Inaingia akilini kweli? Tafiti kabla ya kuzungumza.
 
Hujui ulisemalo hata kidogo, hujui shida waliyonayo watu wnaoishi huko, hujui makazi yalivyoendelezwa na yanavyoendelezwa huko. hufahamu miradi ya nssf, nhc za makazi na idadi ya watu walioko huko na wanaotarajiwa kuishi huko. Nenda kafanye utafiti halafu uje hapa useme kama msimamo wako ni ule ule au umebadilika
 
Dawa ni kujenga railways Toka kibaha hata ikiishia ubungo then ubungo waweke monorail za juu, waige mfano malaysia tu
 

Kwa kuongezea tu kigamboni hata makazi yake asilimia kubwa yamepimwa na manispaa enzi hizo temeke, maeneo kama kibada, gezaulole, mwongozo, mikwambe, toangoma etc yote yamepimwa na watu wanaajenga majumba ya kisasa kwenye sehemu zenye miundombinu ya kisasa. huko kimara sijui gondolamboto kupo ovyo ovyo alafu anataka kuendelezwe....hatari sana
 

Huyu amekurupuka, tumuelimishe
 
Kwa daraja la Kigamboni nitoe pongeze kwa NSSF kwa kuona mbali. Hizo ndo project ambazo tunazihitaji katika nchi yetu. Hii ni long term project.
 



Mimi siyo Great thinker na wala sijawahi na sitowahi kujitambulisha hivyo ila kama wewe unaona unastahili kuitwa hivyo hiyo ni juu yako!

Haya niambie hili daraja litapunguza msongamano wa kiasi gani kwenye huu Mji? Ni asilimia ngapi ya wakazi wa Dar watalitumia kila siku kwenda na kurudi kazini ikilinganishwa na gharama iliyotumiwa kulijenga?
[/QUOTE]

rafiki,
kwanza hili daraja linajengwa kwa hela za NSSF kwa asilimia kubwa na kias Serikali
pili kigamboni ina serve watu wa Kigamboni, Gazaulole,Kimbiji,Mwasonga,Kibada,Tua ngoma,Kongowe mpk Mkuranga
Tatu. Kigamboni ni Wilaya Kamili
nne. Hili daraja litahudumia zaid ya watu 100k kwa siku
tano: usilinganishe gharama as lumpsum na marejesho yakifanyika kidogo kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…