Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,023
- 26,377
Siku nchi hii ikiingia machafukoni huyu mzee atakuwa na mkono wakeNdo maana tunashauri uanzishe chama chako cha Muslim Brotherhood uendeleze harakati zako za kupigania uislam. Hapa JF hatutaki ulete hizo riwaya zako za chuki kugombanisha waTZ kidini. Hakuna mkristo hata mmoja huleta sera za udini humu. Nashauri moderators wakutoe humu maana mwisho wa siku unachochea vita za kidini
Masopakyindi,
Wewe si wa kwanza kughadhibika.
Wengi walichomwa na wanaendelea kuumia na khasa jinsi
nilivyoibadili historia ya TANU na kuandika ukweli kama
ulivyostahili kuandikwa.
Sasa ni mwaka wa 18 kitabu cha Abdul Sykes kipo mtaani
hajatokea wa kuandika kupinga kitabu changu kila siku ni
maneno tu hamjaweza kuandika chochote.
Andika hayo ya upande wa pili unayoyajua wewe tusome.
Toleo la Kiingereza tumefanya matoleo mawili tunakwenda
la tatu In Sha Allah.
Tolea la Kiswahili tuko toleo la tatu tunakwenda toleo la nne.
Utamu wa andiko/chapisho lolote ni kuona "impact" yoyote kwa hadhira uliyoiandikia....Kwa idadi ya machapisho unayojigamba nayo na mwitiko wa wale uliowaandikia ni vitu viwili tofauti...Kiukweli hakuna anayejishughulisha nayo kama fanani alivyokusudia, "It's Totally Mision Failed"
Chapisho limesalia kuwa "Reference" kwenye MADA mbalimbali za Radio Iman pekee ambako wasikilizaji wake nia walewale!
Mazigazi,Siku nchi hii ikiingia machafukoni huyu mzee atakuwa na mkono wake
Sent from my HUAWEI Y360-U31 using JamiiForums mobile app
Mzee mi binafsi nakuheshimu sana kwa umri wako.Mazigazi,
Labda nami nikuulize toka lini au umesikia nchi gani imeingia katika vurugu
kwa sababu katokea mwandishi akasahihisha historia ya taifa hilo?
Nchi zinaingia matatani kwa sababu nyingine si kwa kurekebisha historia.
Pascal,Mkuu Maalim nimefarijika sana na posti yako hii, Mungu akubariki sana na kumbariki huyo Mseminari Mwalimu Paulo, kwa kikiona kipaji chako, na kumfuata Mama yako kumshauri wakupeleke shule, ambayo ndio imekuwezesha kufika hapo ulipo sasa!. Just imagine bila Mwalimu Paulo, ungekuwa wapi na ile ilmu ya Madrassa pekee?!.
Hoja ya "shukrani ya punda mateke inakuja kwa jinsi unaushadadia udini as if Misheni ndio chanza na sababu za kuzorota kwa Waislamu kielimu, kumbe sababu unaijua ila kamwe huisemi, na wengi wa Waislamu walielimika sana Tanzania wa enzi hizo, walisomea shule za misheni, na hawakuitegemea elimu ya madrasa pekee!.
Mkuu Maalim nakii wazi kuwa pamoja na udini wako, lakini angalau wewe ni mstaarabu sana ka Waarabu!, itumie ilmu yako, na ushawishi wako, kuwatuliza wafuasi wako wa humu jamii forums pale unapowaona wamevuka mipaka!. Kitendo cha wewe maalim wao kuwa mstaarabu, uliyestahaabishwa na elimu ya mission, wafunze na wenzio humu ili angalau wakaibiane na wewe!.
Naamini unanielewa nazungumzia nini!.
Ahasanta.
Pasqwa!.
Kagodoro,Ivi gazeti la leo sindio limesema Dau anahisa Newcastle united ya england....na utajiri wa bilion 100.
Bado anasifiwa tena..kwa mbwembwe....kweli...common sense is uncommon pia sometimes
Naona wengi sasa wameshatambua udhaifu mkubwa wa mtoa mada Mohammed Said.
Hata akiiona jiwe atataka ushauri wa wazee wa DSM na jinsi muonekano wake ulivyo kiislamu.
Kitu ambacho ni kosa kwa mustakabali wa nchi.
Mohammed Said haamini kuwa watanzania wengine wasio waislamu wanafikra za umoja wa nchi hii bila kubagua dini, kabila rangi au sehemu anayotka.
(NB Jiwe hilo kama litakuwa na dhahabu patakuwa hapotshi)
Na ikibainika ni kweli utaendelea kumwandikia pambio mswahili mwenzako Wa kariakoo.Kagodoro,
Si kila liandikwalo ni kweli.
Tusubiri uchunguzi wa vyombo vya sheria.
Mazigazi,Na ikibainika ni kweli utaendelea kumwandikia pambio mswahili mwenzako Wa kariakoo.
Mazigazi,Mzee mi binafsi nakuheshimu sana kwa umri wako.
But haya unayoyahubiri yanatutia mashaka vijana Leo Wa Taifa hili tufuku.
Napata wakati mgumu sana nikitafakari juu unachoandika na kukihubiri kama kina malengo mema ya nchii hii .
Tafadhali mzee usijaribu kutupeleka huko unakotaka wewe maana ni dhahiri bila shaka si kwema.
Magumu tunayopitia kama taifa yanatutosha sana hatuhitaji mengine hayo utakayo.
Chonde chonde Lionee huruma Taia hili maskini.
Nashauri ujikite katika mambo yenye tija yatakayotuleta pamoja sisi waTanzania kama taifa badala kujaribu kutubagua kwa historia zako za kibaguzi .
Wako ujenzi Wa Taifa
Mazigazi.
Sent from my HUAWEI Y360-U31 using JamiiForums mobile app
Unarudia kutetea hoja mfu!Msopakyindi,
Nimenyambua sehemu ya jibu kutoka kwa Pasco.
Hebu soma:
''Udini wa Tanzania uliandikwa kwa mara ya kwanza na P van Bergen
mwaka wa 1981.
Kisha akafatia John Sivalon 1992.
Sivalon ndiye aliyeandika maneno mazito sana.
Yeye kaeleza nani mdini katika nchi yetu kwa kutaja majina
Hamza Njozi akahitimisha kwa kuwajadili wote wawili 2002 na serikali
ikakipiga marufuku kitabu chake.''
Ikiwa hujasoma rejea hizi zisome kuna mengi.
Masopakyindi,Unarudia kutetea hoja mfu!
Na kama hoja kama hizo zingekuwa na mashiko, basi hata Ramadhani Dau asingeweza kufika alipofika na hata kupewa Taasisi nyeti na kubwa kama NSSF.
Watu wenye mawazo kama yako ndio yanarudisha nyuma umoja na mustakabali wa nchi katika kujenga umoja.
Tupe mawazo yako juu ya ISIS na anzishwaji wa Caliphate huko Syria na Iraq.Masopakyindi,
Najua uzito wa kusema yale Bergen aliyogundua na akaandika
katika kitabu chake ''Religion and Development in Tanzania.''
Umoja unatanguliwa mbele na haki sawa kwa wote.
Masopakyindi,Tupe mawazo yako juu ya ISIS na anzishwaji wa Caliphate huko Syria na Iraq.
Mkuu elewa kinachobishaniwa hapa.Watanzania,
Hivi ni nani aliyewaloga!? Ninyi ambao ukweli ukiwekwa wazi mnatokwa na mapovu bure.
Mnakataa kukubali kazi nzuri iliyofanywa na Dr. Dau kwa sababu ya itikadi? !!
Intergrity, intelligence and patriotism of Dr.Dau I'd unquestionable. Watu kama hawa kwa nchi zingine huwa ni assets kubwa, wanathaminiwa na kuenziwa, nyinyi mnaleta propaganda hapa!!
Wakati mwingine mtu unakuwa na chuki hadi unashindwa kuficha hisia zako..najaribu ku imagine, laity mradi huu wa daraja la Kigamboni ungefeli au kukwama kwa sababu yoyote iwayo, mngekuwa sasa hivi mnasema kitu gani. Nayazingatia maneno yalosemwa na walosema ''ukiijua sababu ajabu huondoka ''
MchukiaUonevu,Watanzania,
Hivi ni nani aliyewaloga!? Ninyi ambao ukweli ukiwekwa wazi mnatokwa na mapovu bure.
Mnakataa kukubali kazi nzuri iliyofanywa na Dr. Dau kwa sababu ya itikadi? !!
Intergrity, intelligence and patriotism of Dr.Dau I'd unquestionable. Watu kama hawa kwa nchi zingine huwa ni assets kubwa, wanathaminiwa na kuenziwa, nyinyi mnaleta propaganda hapa!!
Wakati mwingine mtu unakuwa na chuki hadi unashindwa kuficha hisia zako..najaribu ku imagine, laity mradi huu wa daraja la Kigamboni ungefeli au kukwama kwa sababu yoyote iwayo, mngekuwa sasa hivi mnasema kitu gani. Nayazingatia maneno yalosemwa na walosema ''ukiijua sababu ajabu huondoka ''