Dar: Wanafunzi 4 wamefariki kwa kuzama baharini

Dar: Wanafunzi 4 wamefariki kwa kuzama baharini

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,197
Reaction score
64,639
Wanafunzi wanne wamefariki kwa kuzama kwenye mwambao wa bahari ya hindi wakiwa kwenye hafla ya kusheherekea matokeo yao ya mtihani. Wanafunzi wanne wa Shule ya Sekondari Kimbiji iliyopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wamepoteza maisha baada ya kuzama kwenye mwambao wa bahari ya hindi wakati wakiwa kwenye hafla ya kusheherekea matokeo yao ya mtihani wa Mocko wa kidato cha nne ambapo shule hiyo imeshika nafasi ya kumi kwa mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya kwanza kwa wilaya ya Kigamboni.

Tukio la kuzama kwa wanafunzi hao lilitokea siku ya jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kwa mujibu taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni Stephen Katemba, watoto hao walijumuika pamoja na walimu wao kwenye sherehe hiyo ambapo wakati wakiendelea kufurahia matokeo yao baadhi ya wanafunzi walikuwa wakicheza mpira kandokando mwa bahari kabla ya mpira huo kuingia baharini hali ambayo ilimlazimu mmoja wao kuufuata bila kujua kina cha maji na kusababisha aanze kuzama.

Aidha Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kuhimili maji alijaribu kuomba msaada kwa wanafunzi wenzake ndipo watatu walijaribu kwenda kumuokoa lakini bila mafanikio ambapo nao pia walikwama na wote wanne kufamaji.

Kufuatia hali hiyo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Seriklai za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo amefika shuleni hapo na kutoa pole za serikali kwa walimu, wazazi, pamoja na wanafunzi pamoja na kuagiza wakuu wote shule za sekondari na msingi nchini kuacha utamaduni wa kutoka na wanafunzi nje ya shule kufanya sherehe ya aina yoyote ile badala yake watumie maeneo ya shule zao.

Wanafunzi waliofariki kwenye tukio hilo ni Cecilia Paulo mkazi wa Keko, Selestine Malipesa wa Kimbiji, Agnetha Mlaki wa Kisemvule, Queen Leonard Mandala wa Mkuranga.

Chanzo: Channel ten
 
Woe ni wa kike?

Pumziko La Amani kwao na pole kwa Wafiwa..
 
Back
Top Bottom