Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 33,977
- 67,600
Suguye ndiyo nani?Huduma za kiroho katika Kanisa la The
Word of Reconciliation Ministries (WRM) la Kivule- Matembele ya pili, jijini Dar es Salaam zimesitishwa huku ulinzi wa Jeshi la Polisi ukiimarishwa ili kuzuia huduma yoyote isifanyike.
Huduma ya kanisa hilo lililo chini ya Nabii Nicolaus Suguye imezuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita, huku waumini zaidi ya 4,000 wakidai kupewa maelekezo ya kutakiwa
kutafuta maeneo mengine ya kuabudu.
Vyanzo vinaeleza kanisa hilo lilikuwa ni miongoni mwa taasisi ambazo hazijapata usajili rasmi, isipokuwa barua ya usajili wa awali inayoruhusu kufanya huduma sehemu moja bila kualika
wageni kutoka nje, kufungua matawi na kufanya
makongamano huku Serikali ikifanya uchunguzi wa mwenendo wake.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema kwa sasa anayelalamikia si yeye (Suguye) kwani yeye anajua kanisa halina usajili na anajua
kwa nini amefungiwa.
Mwananchi tangu juzi na jana iliwatafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na naibu wake, Jumanne Sagini ambao taasisi za dini ziko chini ya wizara yao, lakini hawakupokea simu na wakati mwingine zilizimwa.
Msemaji wa wizara hiyo, Christina Mwangosi alipokea simu mara moja na alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo aliomba apigiwe baadaye.
Hata hivyo, alipotafutwa baadaye hakupokea tena na mwandishi alipofika ofisi za msajili wa taasisi hizo jijini Dar es Salaam alikutana na maofisa waliomwambia hawawezi kulizungumzia suala hilo isipokuwa msemaji.
Suguye, anayetambuliwa na waumini wake kama nabii, alianza kutoa huduma za kiroho mwaka 1998 kabla ya kuanzisha kanisa hilo mwaka 2007.
Udini awamu ya sita inatisha sanaHuduma za kiroho katika Kanisa la The

Kama hajakamilisha usajili, sioni kama kuna udini hapo..!!Udini awamu ya sita inatisha sana
Matapeli wanaosajiliwa na serikali?Hawa matapeli wamechachama kwerikweri
Ova
Siyo utaratibu mpya. Makanisa yote yanasajiliwaUsajili? Dunia ina mambo, yaani kumuabudu Mungu hadi usajili? Labda kama ni chama cha siasa au NGOs za kiharakati.
Suguye wewe unamjua?Kama tumeruhusu uwepo wa nyumba za ibada zisizosajiliwa,basi kumfungia huyu jamaa ambaye ameanza kutoa huduma hapo matembele mwisho tangu miaka ya 2007 hadi sasa basi itakuwa siyo haki wakimfungia Leo baada ya miaka yote hiyo.
Wasitake kuanza kutugawa watanzania kwa kigezo Cha udini.
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Mpumbavu mmoja unaongea hivyo...Naomba serikali ichukuwe mfano wa Kagame kuhusu makanisa.
Ni nabii,, mtu mmoja mcheshi sana, mtu wa watu,, kama una shida yeyote iwe ni ya kifedha, kiafya, unataka gari, nyumba,, mwone huyo nabii😄Suguye ndiyo nani?
Hakuna udini hapo,Hawa manabii inabidi wawe jera,ni wezi tuUdini awamu ya sita inatisha sana
Hawezi kuendesha huduma muda wote huo bila kibali, ni vita ya kiuchumi tu hapo.Kama hana kibali sio kulifunga ni kumpa mda atafute kibali