Hakuna solution ya kudumu ktk port ya Dar isipokuwa kujengwa kwa port nyingine yenye uwezo mkubwa zaidi nje ya jiji sehemu zenye fukwe kuelekea Bagamoyo..
Kinywa cha babndari yetu ni kidogo sana na bandari haiwekzi kuongezeka ikiwa tatizo ni kinywa chake..chukulia tu bus lenye mlango mmoja hata siku moja haliwezi kuchukua uharaka wa aina yoyote kufupisha muda wa kuchukua abiria 50... hakuna solution isipokuwa kubomoa huo mlango au kuongeza mlango mwingine..
Hii nafasi ya Bandari ya sasa na mandhari yake hakika ni ktk kuufikiria mji mpya wa Dar ambao unahitaji zaidi nafasi kubwa iliyochukuliwa na Bandari.. Mauzo ya sehemu hiyo tu iwe viwanja kwa Mahotel na majumba ya high rise ikiwa ni pamoja na maofisi, maduka Apartment na condos itarudisha fedha kibao za mtaji utakao tumika ktk ujenzi wa bandari mpya.. Mji wetu utapendeza na masalio ya Bandari yatumike kwa cruiser shipline ambazo zitakuwa zikimiminika nchini kuleta Watalii, Yatch clubs, michezi ya maji na bustani safi zinazoambaa pwani. Pia barabara ya nguvu Blvd kandokando ya fukwe toka Kurasini hadi O'bay zikiungana na daraja la Kigamboni..Haya ndio maendeleo tunayoyatazamia.
Nimefurahi sana kuona tangazo jipya la Tanzania CNN, baaabu kubwa! hakika inaonyesha wazi message za Jf zimeanza kugonga mahala pake..