Dar: Mkuu wa Mkoa, Amos Makala aagiza Mabasi yote kushushia abiria Stand ya Mbezi

Lakini jamani nafikiri ni kwa kipindi sasa, wote mnajua Tz imekuwa ni nchi ya kutolewa maagizo na viongozi, bila kuweka sheria au mipango na mikakati ya madhubuti kutatua changamoto husika, na hayo nafikiri muendelezo tu....Kwa hivyo labda msilalamike sana kuhusu hayo yanayojiri........na kazi iendelee.
 
Mkuu
Ili Stand ya mabasi iwe karibu na kila mkazi wa Dsm...ilitakiwa ijengwe wapi?
 
Siyo muda mrefu hilo agizo litatenguliwa aidha na yeye au mkuu wake
Katika wapumbavu, huyo RC ni wa kwanza, hivi hajui kuwa tatizo la usafiri wa daladala limepunguzwa na hayo mabasi?
Hivi hajui kwamba angeweza kuwatumia askari wa uhamiaji kudhibiti tatizo analolitaja bila kuwaathiri wananchi?
Hivi hajui anawaadhibu wananchi kwa makosa ya watu wengine?
Hivi hajui kuwa amezalisha tatizo juu ya tatizo?
Hivi amefanya lini utafiti kabla hafikia hayo maamuzi?
Kama amefanya utafiti wowote, je amewashirikisha wadau ambao ni wananchi?
Huyu ni RayC siyo RC kabisaaa!
 
Kama lengo ni kudhibiti wahamiajai haramu bado nafikiri lengo halitatimia maana mimi kama mhamiaji haramu si ninaweza shukia Mlandizi/Mkuranga/Bagamoyo/Msata na kupanda daladala itakayonifikisha niendapo?
 
Point lakini lugha kaliiiii
 
Nadhani hizi nafasi za uRC na uDC zina shida mahali.. Kama hazijalaaniwa basi zina maruhani.. Mtu akishakalia hicho kiti kurukwa na akili na kuongea mazonge anapokuwa mbele ya cameras ni jambo la dakika
Katiba mpya alafu ipate msimamia Sheria Kama bwana masase 16 nahisi nchii itanyooka
 
Ni jambo jema kwakuwa
  1. Inampa unafuu msafiri kutohangaika na mizigo mara mbili au zaidi
  2. Daladala ni za kugombania sana, hivyo wasafiri kuendelea na safari kwenda mjini inapunguza usumbufu wa kugombea daladala
Ndio hivyo mkuu.

Makala hapa kaingia chaka tamko haliwezi kutekelezwa
 

unabaki kusema mpumbavu na mjinga najua unaogopa kutukana

anafr...msng xxxh*##&@-+#??! nyok zake
 
Ndio hivyo mkuu.

Makala hapa kaingia chaka tamko haliwezi kutekelezwa
Huyo hajitambui, anategemea ushauri wa baadhi ya watu wanaonufaika na huo usumbufu, lakini anasahau "kuchanganya za kuambiwa na zake" kuna watu wanaweza kumshauri vibaya ili kumng'oa kwenye nafasi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…