DAR: Meya wa Jiji ataka nyumba za kulala wageni (gesti) zifungwe kamera

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,681
39,012
2016-05-08-11-53-11--1708143328.jpeg

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameshauri kufungwa kwa kamera maalumu za CCTV kwenye nyumba zote za kulala wageni na hoteli ili kuimarisha ulinzi.Ushauri huo wa Mwita unakuja baada ya siku sita kupita , kutokea kwa tukio la mwanamke mmoja kufariki dunia akiwa gesti.

Mwita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), alisema mamlaka husika wakiwamo wamiliki wa hoteli na nyumba hizo waliangalie suala hilo kwa jicho la tatu kwani litasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia matukio kama hayo.“Kamera hizi zisifungwe chumbani bali zifungwe maeneo ya nje na mapokezi kwenye jingo husika.Hii ni njia sahihi ya kupambana na matukio kama haya maana hili lipo hivi linaweza kutoke lingine zaidi ya hili,” alisema Mwita ambaye alishika madaraka hayo Machi 22mwaka huu.Mbali na hilo, Mwita alisahauri pia kuboreshwa kwa mfumo usalama katika maeneo mbalimbali ili kuzuia vitendo kama hivyo vya kinyama vinavyokatisha uhai wa binadamu.Hata hivyo , Mwita aliwaomba viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam, kuendelea kutoa elimu kwa umma ili wakazi wa jiji hilo kumrudia Mungu na kuachana na vitendo vya kinyama.

Pia meya huyo amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimnukuu yeye kuwa ameshauri wamiliki wa gesti kuwapiga picha wageni wanaokwenda kulala kwenye nyumba hizo.

Hivi karibuni mwanamke huyo jina limehifadhiwa alikutwa amefariki dunia kwenye gesti Bray iliyopoa maeneo Kimara , manispaa ya Kinondoni huku chanzo cha kifo bado hakijawekwa wazi hadi uchunguzi utakapokamilika na maiti huyo amehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

Source; Mwananchi
 
Huo ni upeo mdogo sana wa mh.mayor kufikiri nadhani itafutwr namna nyingine ya kuongez ulinzi kwenye nyumba za wageni na sio cccam coz privacy za watu zitahidhiwa vipi? Si wote wanao panga guest ni wabaya inamna kama mtu na mkewe wapo humo guest basi operators wawe mahuhuda wa wanacho kifanya wanandoa hao?? Nadhana mizuka ya mh sugu naiona hapa.
Nadhani hujafahamu mantiki ya cctv, hazifungwi kwenye vyumba vya kulala, Lakini lazima ziwepo reception zote na milango yote ya kuingilia, hili lipo kwenye hotel karibu zote kubwa hata hapa mjini, Ila kwa guest za huku kwetu kwa mtogole, tandika Ndio hakuna na hawataki, kwa sababu wanajua Yale mambo yetu tena
 
Huo ni upeo mdogo sana wa mh.mayor kufikiri nadhani itafutwr namna nyingine ya kuongez ulinzi kwenye nyumba za wageni na sio cccam coz privacy za watu zitahidhiwa vipi? Si wote wanao panga guest ni wabaya inamna kama mtu na mkewe wapo humo guest basi operators wawe mahuhuda wa wanacho kifanya wanandoa hao?? Nadhana mizuka ya mh sugu naiona hapa.

Hapana. kama umewahi kufika nchi nyingine hass Marekani na Ulaya. Kamera zinafungwa nje kwenye njia ya kuingia katika vyumba. Kamera ni muhimu sana kwa usalama
 
Kuna baadhi ya hoteli/gesti hilo linafanyika labda wazidi tu kuwaelimisha wenye guesti ili waone umuhimu wa kufunga hizo kamera
 
Dah.. ningekuwa mimi ningependekeza ziwekwe kila chumba. Mkitoka salama wote mnaenda security mnaifuta clip yenu au mkitaka copy kwa ajili kumbukumbu mnailipia kidogo cha msingi EFDs ziwepo ili serikali isikose haki yake
 
Hata wakifunga bado sioni umuhimu wake zinaweza kufungwa ila matukio yatazidi kutokea tu! Kuna ile video ililetwa hapa jamaa alivamiwa na majambazi na kuuwawa akiwa getini wale wezi walisha dakwa?
 
kwa sababu matukio ya vifo yameshamiri gesti.
Matukio yapo mengi siyo gesti peke yake hata kwenye mahoteli makubwa kuna wahalifu pia hizo kamera zinatakiwa kufungwa kwenye mahoteli sehemu muhimu kama kwenye lift, parking, na kwenye njia za waenda kwa miguu mahotelini.
 
Huo ni upeo mdogo sana wa mh.mayor kufikiri nadhani itafutwr namna nyingine ya kuongez ulinzi kwenye nyumba za wageni na sio cccam coz privacy za watu zitahidhiwa vipi? Si wote wanao panga guest ni wabaya inamna kama mtu na mkewe wapo humo guest basi operators wawe mahuhuda wa wanacho kifanya wanandoa hao?? Nadhana mizuka ya mh sugu naiona hapa.
Hivi mwenye upeo mdogo ni meya au wewe!
Nimeamini nyani haoni kundule!

Umejidhalilisha wewe na kizazi chako!!
 
Duh, upeo wako mdogo sana ndugu, aliyekwambia CCTV cameras zinaungwa ndani ya vyuma ni nani?!
 
Huo ni upeo mdogo sana wa mh.mayor kufikiri nadhani itafutwr namna nyingine ya kuongez ulinzi kwenye nyumba za wageni na sio cccam coz privacy za watu zitahidhiwa vipi? Si wote wanao panga guest ni wabaya inamna kama mtu na mkewe wapo humo guest basi operators wawe mahuhuda wa wanacho kifanya wanandoa hao?? Nadhana mizuka ya mh sugu naiona hapa.

CCTV zinafungwa koridoni, na kwenye main entrance na getini. Naamini ndivyo alivyo maanisha.
Ila sasa itakuwa taflani kwa sie wachepuki
 
Back
Top Bottom