Dar mawasiliano magumu jamani!

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Dar kuna sehemu haina mawasiliano! Send to a friend

KAMPUNI za simu nchini zimetakiwa kuweka minara yao Kata ya Msongola eneo Kiboga, Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Rai hiyo ilitolewa na wakazi wa eneo hilo kwa Mwenyekiti wa Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala, Angelina Malembeka, wakati alipokuwa akipokea kero za wananchi.

Walisema tangu kuingia kwa mawasiliano ya simu za mkononi, eneo hilo halina mnara hata mmoja hali inayopelekea kutopata huduma hiyo ya mawasiliano.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Hassan Soud, alisema tatizo la mawasiliano kwenye kata hiyo ni la muda mrefu, hali inayopelekea kuchelewa kwa maendeleo eneo hilo.
Kwa upande wake, Malembeka alisema hali hiyo haivumiliki na kwamba, ni aibu ndani ya Dar es Salaam kutokuwa na mawasiliano kwa sababu ya minara.

“Tatizo hili la kutokuwapo na minara na kuwafanya wakazi wa hapa Kiboga kuwa na mawasiliano ya kuungaunga ni aibu, kwani Msongola ni sehemu ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, naahidi kulishughulikia kwa jinsi ya kipekee ili limalizike haraka,” alisema.

Kuhusu barabara, Malembeka alisema wiki hii katapila zipita kwa baadhi ya barabara maafuru kusawazisha ili ziweze kupitika kwa mwaka mzima.

SOSI: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom