Dar: Majambazi 8 wanaojihusisha na mtandao wa wizi wa magari wakamatwa na polisi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Kaimu Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lucas Mkondya, amesema watu hao wamekamatwa huko Kongowe mkoa wa Pwani wakiwa na gari moja aina ya Noah lenye namba T 455 DEP.

"Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao na kuwahoji wamekiri kuendesha mtandao wa wizi wa magari katika jiji la Dar es Salaam na sehemu nyingine za nchi na mpaka sasa wamekiri kuiba magari mengi". Amesema Mkondya.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao ili kupata taarifa za watu wanaowauzia magari hayo baada ya kuyaiba pamoja na mtandao mzima wa wizi huo ili kudhibiti wizi wa magari Dar es salaam.

"Tunaotaka kuwabaini hasa ni wanunuzi wa hayo magari lengo ni kusambaratisha mtandao huo ila lengo ni hao wanunuzi ambao ndio hasa tunawatafuta," amesema Mkondya.

IMG_2851.jpg
 
Huwa naamini, ninapokataa ni sehemu moja tu!"Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao na kuwahoji wamekiri kuendesha mtandao wa wizi wa magari katika jiji la Dar es Salaam na sehemu nyingine za nchi na mpaka sasa wamekiri kuiba magari mengi". Amesema Mkondya.

Yaani hii kauli huwa siiamini na kama ukitaka kuhakikisha Jaribu kuhudhuria
mahakamani usikie majibu yao.
 
Uteuzi at work.... Picha mbona haupewi au ndio kufukuzia nafasi ya Siro!.. Tukio kama hilo na magari hayo ni vyema tukaonyeshwa, yawezekana langu likaliona hapo...

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
Kuna picha ya hayo matukio?.. Magari, wahalifu n.k Ngoja niamini tu kibabe...



Sent from my Diamond Rose Iphone 32 GB using JamiiForums Mobile App
 
Hadi sasa nina Noah mbili...ya acacia na ya hawa wezi

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Halafu wakifika mahakamani wanakana. Maana wangegoma wangepigwa ndusu za vichwa na ingesemekana walivaa "baibui"! Hongereni" majambazi wa magari " kwa kukiri uhalifu!
 
Back
Top Bottom