Dar: Madereva wa Uber wailalamikia Uber kwa manyanyaso

Dar: Madereva wa Uber wailalamikia Uber kwa manyanyaso

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,333
Reaction score
15,823
Habari wakuu,

Madereva wanaofanya biashara ya Uber(Madereva wa Mtandaoni) jijini Dar Es Salaam, Wamekutana katika Viwanja vya Leaders Club kuongelea matatizo yao.

IMG_20180918_112557.jpg


Kikubwa wanacholalamikia ni;

1. Kufungia madereva bila kusikilizwa. Yaani mtu akilalamikiwa na mteja, anafungiwa maisha bila kusikilizwa wakati ndo sehemu yao ya kupatia mkate.

2. Uber wanawapa Bei ndogo sana

3. Upatikani vibali kuwa mgumu, vibali vya jiji vya gharama kubwa. Havipatikani jiji wala Uber. Vibali madereva wanapewa vichochoroni na bila risiti. Madereva Taxi wanalipa elfu 46, lakini vibali vya jiji (jiji Uber) wanalipa elfu 80.

4. Ufanyaji kazi ni masaa 12 tu ukomo.

4. Makato makubwa sana. Yaani dereva anakatwa 25% ya malipo aliyetoa mteja. Taxify wanachukua 15% Movin wanachukua 5%.

IMG_20180918_112721.jpg


Kwanini Uber 25%? Ndo maana tupo hapa...

6. Kauli za kukera.. Uber kodi, mapato tunalipa sisi. Ukilalamika unaambiwa zima au ondoka/acha kazi. Hamna sheria inambana

7. Vibali vya jiji Uber walishajitolea kulipia, lakini unapoenda kukichukua unalipia elfu 80.

8. Usalama mdogo kwa Madereva wa Uber, tunatekwa na Uber hawatoi msaada. Mtu anasajili email ya uongo na namba ya simu kisha anajisajili Uber kumbe ni mwizi.

9. Uber hawana mikataba kwa madereva wao hapa nchini.

10. Uber wanatuita Partner lakini hatushirikishwi kwenye maamuzi

11. Usumbufu wa Trafiki, YONO, Jiji na ukamakati kiholela wa Magari ya Mitandaoni kuwa mkubwa sana.

12. Polisi hawakosi kosa, wapewe maelekezo.

YONO ni raia, raia hawatakiwi kukamata raia mwenzao. Sasa basi!

Kiongozi wa SUMATRA amewashauri waanzishe chama na kujisajili kwenye Trade Union yenye uwezo kisheria wa kuwapigania.

Wakili wa Kujitegemea, James Marenga kawapongeza kwa umoja wao na malengo yao.

IMG_20180918_113812.jpg


MARENGA ANASEMA:
Inatakiwa tujue tunafanya kazi na watu wa namna gani, lakini kama wameruhusiwa kuja kufanya kazi nchini, hivyo wapo kisheria.

Tatizo ninyi mnaingia kwenye kudownload App bila Kusoma terms and rules na mume-accept wote mliodownload App ya Uber.

Hii ni biashara huru. Sasa kwa huu umoja manake mnataka mkae chini muwaambie na mkubalieni makubaliano mapya tofauti na yale ya online.

Sheria ya mikataba ipo, kwa umoja wenu mkiamua kurudi kwenye taxi au muendelee na uber. Hivyo ni jambo jema. Ninyi ni umoja wa wafanya biashara. Nyie sio wafanyakazi.

Uber wanasema utaratibu wa kubadilisha malipo upo juu yao. Na kama unatumia App yao, ulikubali hilo.

Siri ya biashara ya mtandao ni ya wale walioianzisha. Lazima mkae chini, nguvu zenu mziweke kwenye utaratibu wa sheria ndio itakao wasaidia.

Hiyo kufungiwa maisha mlikubali kwenye terms zilizo kwenye App yao. Hivyo chagueni viongozi wenu watakaowawakilisha wakutane na viongozi wa Uber ili muingie terms mpya tofauti na zile zilizo kwenye Application yao.
 
uber anapiga faida kubwa kuliko wenyw magari au madereva wanaomfanyia kazi..
 
shida watanzania hatuna umoja... hivi kundi lote likijitoa uber na kupiga taxify... wateja hatutawafata huko taxify kweli
Hayo mavikao ni kupotezeana muda tu na sijui ni nani wamamsimulia hizo case zao. Biashara huria inakuruhusu kuhama ili maisha yaendelee. Mbona wanawake tunawaacha na kutafuta wengine?
 
Ww jisajili uba ela yao usiwape wala nini kama mm navyofanya nakula vichwa kama kawa na pesa yote nachukua mimi yani gari langu vibali nikate mm tena pesa niwape wao we thubutu awapati kitu hapa.
 
Ww jisajili uba ela yao usiwape wala nini kama mm navyofanya nakula vichwa kama kawa na pesa yote nachukua mimi yani gari langu vibali nikate mm tena pesa niwape wao we thubutu awapati kitu hapa.

huo ndio ujanja...japo mbeleni watakufungia..

ila jamaa nao wanyonyaji.. yaani wachukue 2500 kwa kila 10,000 unayolipwa.. huku hawanunui mafuta, service ya gari wala matairi hawakuchangii
 
Mida hii Madereva wa wa Uber,Taxify nk wanaotia huduma ya usafiri kupitia Online App za Uber na Taxify wamomea punguzo kubwa la nauli kwa wateja.
Mda huu kikao kikubwa kinaendelea Maeneo ya Leader Club.
 
Mida hii Madereva wa wa Uber,Taxify nk wanaotia huduma ya usafiri kupitia Online App za Uber na Taxify wamomea punguzo kubwa la nauli kwa wateja.
Mda huu kikao kikubwa kinaendelea Maeneo ya Leader Club.

Utatupa mtejesho mkuu.

Biashara ya Uber na Taxify imekuwa ngumu ghafla.
 
Nilijua tu huu utaratibu kwa bongo yetu bado sana watuachie tu bajaj zetu, sie bila kusukumana na kuburutana ni ngumu mno! Uber na Taxify ziko nchi kibao na hakuna mgomo hapa kwetu ndo vurugu kila kukicha
 
Hakuna biashara ya ajabu ajabu kama Uber. Eti umbebe abiria Mlimani City kwenda Makongo Juu, unapitisha gari yako kwenye ile mimawe weeee, full ac upambane na ile milima hadi huko porini kisa 6,000. Kutoka huko unarudi tupu, unachukua 3,000 unaenda kuosha gari maana si kwa mivumbi ile na uharibifu wa gari.

Ukienda Makongo Juu mara 9 kwa siku kama gari ni yako ni lazima upate kichaa. Ni vile tu wenye magari yao hawajui madereva wanayapeleka wapi na wapi.
 
Back
Top Bottom