DAR LUX yadhalilisha abiria wake

Hili swala la gari kutokupumzika kwa hapa Tz ni kawaida. Haswa kwa wamiliki wenye magari machache.....Gari inatoka Dar inafika Mwanza usiku. Kesho yake gari hiyo hiyo inageuza Dar ikiwa na madereva wale wale.
 
Wakuu hii mada yenu nimeifikisha kwenye group letu la wana dar lux(blue) whatsapp kwa kuwa wahusika wako kule nahakika watatupa majibu mazuri na ni watu wasio ficha na pia madereva wao pia wako kule watatoa majibu juu ya hii tuhuma
Mkuu hebu fikisha na hili.

Kuna Dar Lux inayokwenda Tunduma (Mimi nilipanda Jumatatu ya tarehe 10/10/2016 namba ya gari ni T568 DCW sina uhakika sana na hizi namba za mwisho CW sababu zimekorogwa sana kwenye tiketi hapa) gari ilifika Mbeya mida ya 2+ usiku lakini tulipofika nane nane mhudumu akatangaza kwamba hatosimama kituo kingine chochote mpaka Mbeya stand. Cha ajabu hawakuingia stand na sisi tulikuwa wageni Mbeya tukajikuta tunashushiwa Mbalizi baada ya abiria wazoefu kutuambia tulishapita Mbeya. Kumuuliza muhudumu akatuambia siku hizi gari za Tunduma hazingii Mbeya stand, tukamuuliza kwa nini aliatangaza wataingia stand na wakafanya kinyume chake? tukamuuliza tena kwa nini asingetangaza kwamba watu wanaoshukia Mbeya watawashusha angalau hata Simike? Matokeo yake akatujibu utumbo mtupu.

Mbali na changamoto hiyo huduma zao za ndani ya basi zilikuwa nzuri sana na hata kurudi tulirudi pia na basi ilo ilo. Warekebishe ilo tu.
 
Sasa abiria wanadhalilika vipi??...

Umesema Dar Lux wanadhalilisha abiria wao...Sijakuelewa
 
Mtoa mada eleza vizur abiria wamedhalilishwaje? Kwan wanazunguka na gari au wao wakifika gari inageuza na wengine!
 

Siku zinavyozidi kwenda janga la kushindwa kujieleza linaendelea hapa bongo
 

Jambo ambalo umeshindwa kulieleza hapo mwanzo
 


kwa hiyo gari linaweza kuanguka au kupata ajali kama halijaendeshwa. yaani gari liwe limepaki halafu lianguke lenyewe au ligongane na kuua watu
 
Hii ndio Tanzania!
Mtoa mada anataka Gari lipumzike! Kwa hiyo toka saa saba usiku mpaka saa kumi na mbili lalipoondoka lilikuwa linazurura Mwanza nzima?
 
Kuna kaugonjwa fulani watu wanaumwa humu,si kila mtu mwandishi wa habari.Yeye anamahanisha madereva wapumzike sio wakifika saa saba uck saa kumi na moja waanze tena safari na gari ile ile na madereva wale wale.Kesho wakiangusha magar mnajazana humu kuwatukana madereva.Hii nchi ina mapunguani wengi.
 
kwa hiyo gari linaweza kuanguka au kupata ajali kama halijaendeshwa. yaani gari liwe limepaki halafu lianguke lenyewe au ligongane na kuua watu
Usiwe mgumu kuelewa!
Dereva anachofanya ni kukamilisha mfumo wa gari kutembea, akiipa umeme starter itazungusha ingine, mfumo wa vilainishi ukiwa sawa ingine itazunguka (dereva hazungushi crankshaft kwa mikono yake) pump itawaka sambamba na sterter, itasukuma mafuta kwenda kwenye combustion chamber ambako piston zitafanya ule mkandamizo kwenye block ingine na nguvu itatengenezwa pale, (hii nguvu hatengenezi dereva)
Likiwaka dereva ataunganisha (mfumo) ingine na gearbox, hapo hapo gari litaanza kujongea.

LINAJONGE KUELEKEA MFUMO UNAVYO SUPPORT.

Anachofanya dereva ni kulielekeza kimfumo lijongee kwa mwelekeo anaoutaka.

Wakati linajongea mfumo umepaswa kuwa supportive kuufanya mjongeo kuwa sustainable.

Kwa mfano wakati wa kujongea tairi likachomoka ina maana mfumo wa gari unashindwa ku surport acceleration na gari litaanguka!! (dereva) hawi ameliangusha.

Au dereva akilielekeza gari korongoni halikadhalika hawi ameliangusha yeye, bali korongo litakuwa ni gape kwenye mfumo ku surport acceleration hivyo litaanguka lenyewe.

NAAMINI NIMEELEWEKA
 

Hata wewe hueleweki! ungetoa namba za hao unaotaka awapigie, sio kumwambia eti azisome ktk kioo cha gari, unadhani yupo humo kwenye gari tu anangoja nini?
 
Kama mtoa mada unawasemea madereva na wafanyakazi wa kwenye gari kuwa wazi na urekebishe kichwa cha habari ila ukisema abiria wanadhalilishwa unakosea na ni upotoshaji
 
Basi alitakiwa aseme hivyo mana alikuwa anakitu cha muhimu ila uwasilishaji ndo kachemka...ila Dar Lux wapo vizuri lakini kuna mikokoteni kama Najimunisa,Green Star(sijui bado lipo)..haya si ya kujiroga kupanda safari ya Mwanza
Mkuu mara ya mwisho umesafiri lini?
 
bado wewe ni mbumbumbu kama dereva ataendesha pasipo uangalifu ajali itatokea vipi? gari halijiongozi ila linaongozwa na dereva huyo ambaye anafika mwanza akiwa amechoka na kuamka na usingizi
 

Mie nimesafiri na Dar Lux Ni mazuri sana km yanayoelekea nairobi ,
Acheni kuchafua kampuni nzuri, usb cable kila kiti zinazofanya kazi sio magumashi km mabasi mengine,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…